047-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Alama za Upendo wa Allaah kwa Waja Wake na Kuhimizwa Kujipamba Nayo na Kuitafuta

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

 

باب علامات حب الله تَعَالَى للعبد والحث عَلَى التخلق بِهَا والسعي في تحصيلها

047-Mlango Wa Alama za Upendo wa Allaah kwa Waja Wake na Kuhimizwa Kujipamba Nayo na Kuitafuta

 

Alhidaaya.com

 

قَالَ الله تَعَالَى:

 

قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣١﴾

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Aal-'Imraan: 31]

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَن يَرْتَدَّ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّـهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ أَذِلَّةٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ يُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوْمَةَ لَائِمٍ ۚ ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٥٤﴾

Enyi walioamini! Yeyote atakayeritadi miongoni mwenu kutoka Dini yake, basi Allaah Ataleta watu (badala yao) Atakaowapenda nao watampenda; wanyenyekevu kwa Waumini, washupavu juu ya makafiri; wanafanya jihaad katika njia ya Allaah na wala hawakhofu lawama za mwenye kulaumu. Hiyo ni fadhila ya Allaah Humpa Amtakaye. Na Allaah ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote. [Al-Maaidah: 54]

 

 

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( إنَّ الله تَعَالَى قَالَ : مَنْ عَادَى ليَ وَلِيّاً ، فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالحَرْبِ ، وَمَا تَقَرَّبَ إِلَيَّ عَبْدِي بِشَيءٍ أَحَبَّ إِلَيَّ مِمَّا افْتَرَضْتُ عَلَيهِ ، وَمَا يَزالُ عَبْدِي يَتَقَرَّبُ إِلَيَّ بِالنَّوَافِلِ حَتَّى أُحِبَّهُ ، فَإِذَا أحْبَبْتُهُ ، كُنْتُ سَمْعَهُ الَّذِي يَسْمَعُ بِهِ ، وَبَصَرَهُ الَّذِي يُبْصِرُ بِهِ ، ويَدَهُ الَّتي يَبْطِشُ بِهَا ، وَرجْلَهُ الَّتِي يَمْشِي بِهَا وَإنْ سَألَنِي أعْطَيْتُهُ ، وَلَئِن اسْتَعَاذَنِي لأعِيذَنَّهُ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah Ta'aalaa amesema: "Mwenye kumfanyia uadui rafiki yangu basi Nimemtangazia vita. Hajikurubishi Kwangu mja Wangu kwa kitu ninachokipenda zaidi kuliko nilichomfaradhishia, Na mja haachi kujikurubishi kwangu kwa Sunnah mpaka Nimpende. Ninapompenda, Ninakuwa sikio lake analosikilizia, na jicho lake analoonea, na mkono wake anaoshikia, na mguu wake anayotembelea, Akiniomba Nitampa, na akijilinda kwangu Nitamlinda." [Al-Bukhaariy]

 

 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( إِذَا أَحَبَّ اللهُ تَعَالَى العَبْدَ ، نَادَى جِبْريلَ : إنَّ الله تَعَالَى يُحِبُّ فُلاناً ، فَأَحْبِبْهُ ، فَيُحِبُّهُ جِبريلُ ، فَيُنَادِي في أَهْلِ السَّمَاءِ : إنَّ اللهَ يُحِبُّ فُلاناً ، فَأحِبُّوهُ ، فَيُحِبُّهُ أهْلُ السَّمَاءِ ، ثُمَّ يُوضَعُ لَهُ القَبُولُ في الأرْضِ )) متفق عليه . وفي رواية لمسلم : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( إنَّ الله تعالى إذا أحب عبداً دعا جبريلَ ، فقال : إنّي أُحِبُّ فلاناً فأحببهُ ، فيحبُّهُ جبريلُ ، ثمَّ ينادي في السماءِ ، فيقول : إنَّ اللهَ يحبُّ فلاناً فأحبوهُ ، فيحبُّهُ أهلُ السماءِ ، ثمَّ يوضعُ لهُ القبولُ في الأرضِ ، وَإِذَا أبْغَضَ عَبْداً دَعَا جِبْريلَ ، فَيَقُولُ : إنّي أُبْغِضُ فُلاناً فَأبْغِضْهُ . فَيُبغِضُهُ جِبريلُ ثُمَّ يُنَادِي في أَهْلِ السَّماءِ : إنَّ الله يُبْغِضُ فُلاناً فَأبْغِضُوهُ ، ثُمَّ تُوضَعُ لَهُ البَغْضَاءُ في الأَرْضِ )) .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaah Ta'aalaa anapompenda mja anamuita Jibriyl na kumwambia: "Hakika Allaah Ta'aalaa anampenda Fulani, hivyo nawe mpende." Hivyo Jibriyl anampenda mtu huyo na baada ya hapo anatangaza kwa watu wa mbinguni kwamba: 'Hakika Allaah anampenda fulani, kwa hivyo nanyi nyote mpendeni.' Hapo watu wa mbinguni wanampenda mtu huyo. Kisha anawekewa kukubaliwa na watu wa ardhini. [Al-Bukhaariy na Muslim]. Na katika riwaayah ya Muslim: Amesema Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Hakika Allaah Ta'aalaa anapompenda mja, anamuita Jibriyl, na kumwambia: "Hakika Mimi nampenda fulani, nawe mpende." Hivyo Jibriyl anampenda mtu huyo na baada ya hapo anatangaza mbinguni kwa kusema: 'Hakika Allaah anampenda fulani, kwa hivyo nanyi nyote mpendeni.' Hapo watu wa mbinguni nao pia wanampenda mtu huyo. Kisha anawekewa kabuli (kukubaliwa) na watu wa ardhini. Na Allaah anapomchukia mtu yeyote anamuita Jibriyl na kumwambia: "Hakika Mimi namchukia fulani, nawe mchukie." Hivyo Jibriyl ('Alayhi salaam) anamchukia mtu huyo na baada ya hapo anatangaza kwa watu wa mbinguni kwamba: "Hakika Allaah anamchukia fulani, kwa hivyo nanyi nyote mchukieni." Hapo watu wa mbinguni nao pia wanamchukia mtu huyo. Kisha anawekewa chuki na watu wa ardhini." 

 

 

 

Hadiyth – 3

وعن عائشة رضي الله عنها : أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم بعث رجلاً عَلَى سَريَّة فَكَانَ يَقْرَأُ لأَصْحَابِهِ في صَلاَتِهِمْ فَيَخْتِمُ بـ ( قُل هُوَ الله أَحَدٌ ) ، فَلَمَّا رَجَعُوا ذَكَرُوا ذلِكَ لرسول الله صلى الله عليه وسلم، فَقَالَ : (( سَلُوهُ لأَيِّ شَيْءٍ يَصْنَعُ ذلِكَ )) ؟ فَسَألُوهُ فَقَالَ : لأَنَّهَا صِفَةُ الرَّحْمانِ فَأَنَا أُحِبُّ أنْ أقْرَأ بِهَا . فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( أخْبِرُوهُ أنَّ اللهَ تَعَالَى يُحِبُّهُ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiyah Allaahu 'anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah alimchagua mtu kuongoza kikosi cha Sarriyah kuwaongoza wenzake katika vita. Akawa katika Swalaah zake zote alizokuwa akiswalisha wenzake akimalizia na (قُل هُوَ الله أَحَدٌ). Waliporudi (Madinah), Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alielezwa hilo, naye akawaambia: "Muulizeni ni kwa sababu gani anafanya hivyo?" Wakamuuliza, naye akasema: "Kwa sababu humo ndani zipo sifa za Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma), nami napenda kuzisoma." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Mpeni habari ya kwamba Allaah Ta'aalaa anampenda." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

 

Share