048-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Onyo kwa Wenye Kuwaudhi Watu Wema, Wanyonge na Masikini
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب التحذير من إيذاء الصالحين والضعفة والمساكين
048-Mlango Wa Onyo kwa Wenye Kuwaudhi Watu Wema, Wanyonge na Masikini
قَالَ الله تَعَالَى:
وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ بِغَيْرِ مَا اكْتَسَبُوا فَقَدِ احْتَمَلُوا بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا ﴿٥٨﴾
Na wale wanaowaudhi Waumini wa kiume na Waumini wa kike bila ya kuwa wamechuma kosa, basi kwa yakini wamejibebea usingiziaji mkuu wa dhulma na dhambi bayana. [Al-Ahzaab: 58]
فَأَمَّا الْيَتِيمَ فَلَا تَقْهَرْ ﴿٩﴾وَأَمَّا السَّائِلَ فَلَا تَنْهَرْ ﴿١٠﴾
Kwa hivyo basi yatima usimuonee.Na mwombaji usimkaripie. [Adhw-Dhwuhaa: 9-10]
وأما الأحاديث ، فكثيرة مِنْهَا :
حديث أَبي هريرة رضي الله عنه في الباب قبل هَذَا : (( مَنْ عَادَى لِي وَليّاً فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالحَرْبِ )) .
ومنها حديث سعد بن أَبي وقاص رضي الله عنه السابق في باب ملاطفة اليتيم ، وقوله صلى الله عليه وسلم: (( يَا أَبَا بَكْرٍ ، لَئِنْ كُنْتَ أغْضَبْتَهُمْ لَقَدْ أغْضَبْتَ رَبَّكَ )) .
Ama Hadiyth ni nyingi, miongoni mwa hizo ni zifuatazo: Toka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu): "Yeyote atakayefanya uadui na rafiki yangu basi Nimetangaza vita naye."
Na Hadiyth ya sa'ad bin Abi Waqqaas (Radhwiyah Allaahu 'anhu): Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ee Abu Bakr! Ikiwa umewakasirisha, hakika utakuwa umemkasirisha Rabb wako."
Hadiyth – 1
وعن جندب بن عبد الله رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( مَنْ صَلَّى صَلاةَ الصُّبْحِ ، فَهُوَ في ذِمَّةِ الله ، فَلاَ يَطْلُبَنَّكُمُ الله مِنْ ذِمَّتِهِ بِشَيْءٍ ، فَإنَّهُ مَنْ يَطْلُبُهُ مِنْ ذِمَّتِهِ بِشَيْءٍ يُدْرِكْهُ ، ثُمَّ يَكُبُّهُ عَلَى وَجْهِهِ في نَارِ جَهَنَّمَ )) رواه مسلم .
Na imepokewa kutoka kwa Jundub bin 'Abdillaah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuswali Swalaah ya Asubuhi yupo katika dhima (himaya) ya Allaah. Hivyo jihadharini Allaah Kuwadai katika dhimma yake chochote, Kwani Anayemtaka dhimmayake atamdiriki, kisha Kumtupa katika Moto wa Jahanam." [Muslim]
Na katika Riwaayah: "Atakayeswali Swalaah ta asubuhi katika Jamaa."