049-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuwahukumu Watu kwa Dhahiri ya Mambo na Kumwachia Allaah Siri Zao

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

 

باب إجراء أحكام الناس عَلَى الظاهر وسرائرهم إِلَى الله تَعَالَى

049-Mlango Wa Kuwahukumu Watu kwa Dhahiri ya Mambo na Kumwachia Allaah Siri Zao

 

Alhidaaya.com

 

 

قَالَ الله تَعَالَى:

فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَخَلُّوا سَبِيلَهُمْ ۚ ﴿٥﴾

Lakini wakitubu, na wakasimamisha Swalaah na wakatoa Zakaah, basi iacheni njia yao (huru). [At-Tawbah: 5]

 

 

Hadiyth – 1

وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( أُمِرْتُ أنْ أُقَاتِلَ النَّاسَ حَتَّى يَشْهَدُوا أنْ لاَ إلهَ إلاَّ الله ، وَأنَّ مُحَمَّداً رَسُول الله ، وَيُقيمُوا الصَّلاةَ ، وَيُؤتُوا الزَّكَاةَ ، فَإِذَا فَعَلُوا ذلِكَ عَصَمُوا مِنِّي دِمَاءهُمْ وَأمْوَالَهُمْ إلاَّ بحَقِّ الإسْلاَمِ ، وَحِسَابُهُمْ عَلَى الله تَعَالَى )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nimeamrishwa kupigana na watu mpaka wakubali kuwa hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Rasuli wa Allaah, kusimamisha Swalaah, na kutoa Zakaah.Wakifanya hivyo zitahifadhika damu zao na mali yao isipokuwa kwa haki ya Uislamu, na hesabu yao iko kwa Allaah Ta'aalaa." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي عبدِ الله طارِق بن أشَيْم رضي الله عنه، قَالَ : سَمِعْتُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( مَنْ قالَ لاَ إلهَ إلاَّ الله ، وَكَفَرَ بما يُعْبَدُ مِنْ دُونِ اللهِ ، حَرُمَ مَالُهُ وَدَمُهُ ، وَحِسَابُهُ عَلَى الله تَعَالَى )) رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwa Abu 'Abdillaah Twaariq bin Ushaym amesema: "Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mwenye kusema Laa ilaaha illa-Allaah, na akakufuru vyote vinavyoabudiwa kinyume na Allaah, atahifadhiwa mali na damu yake, na hesabu yake itakuwa kwa Allaah Ta'aalaa." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي معبد المقداد بن الأسْود رضي الله عنه ، قَالَ : قُلْتُ لرسول الله صلى الله عليه وسلم: أرَأيْتَ إنْ لَقِيتُ رَجُلاً مِنَ الكُفَّارِ ، فَاقْتتَلْنَا ، فَضَرَبَ إحْدَى يَدَيَّ بِالسَّيْفِ ،   فَقَطَعَها ، ثُمَّ لاذَ مِنِّي بِشَجَرَةٍ ، فَقَالَ : أسْلَمْتُ لِلهِ ، أأقْتُلُهُ يَا رَسُول الله بَعْدَ أنْ قَالَهَا ؟ فَقَالَ : (( لا تَقْتُلهُ )) فَقُلْتُ : يَا رَسُول الله ، قَطَعَ إحْدَى يَدَيَّ ، ثُمَّ قَالَ ذلِكَ بَعْدَ مَا قَطَعَهَا ؟! فَقَالَ : (( لا تَقتُلْهُ ، فإنْ قَتَلْتَهُ فَإنَّهُ بِمَنْزِلَتِكَ قَبْلَ أنْ تَقْتُلَهُ ، وَإنَّكَ بِمَنْزِلَتِهِ قَبْلَ أنْ يَقُولَ كَلِمَتَهُ التي قَالَ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Ma'bad Al-Miqdaad bin Al-Aswad (Radhwiyah Allaahu 'anhu) ya kwamba, nilimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Waonaje nikikutana na mtu miongoni mwa makafiri. Tukapigana, naye akanikata mkono wangu kwa upanga, kisha akajificha kutoka kwangu nyuma ya mti, akasema: 'Nimesilimu kwa ajili ya Allaah.' Je, naweza kumuua Ee Rasuli wa Allaah baada ya kusema maneno hayo? Akasema: 'Usimuue.'Nikasema: 'Ee Rasuli wa Allaah! Ameukata mkono wangu mmoja, kisha akasema maneno hayo baada ya kuukata?' Akasema: 'Usimuue, kwani utakapofanya hivyo atakuwa katika nafasi yako kabla ya kumuua. Na hakika wewe utakuwa katika nafasi yake kabla ya yeye kutamka kauli yake hiyo." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 4

وعن أُسَامة بن زيدٍ رضي الله عنهما ، قَالَ : بعثنا رَسُول الله صلى الله عليه وسلم إِلَى الْحُرَقَةِ مِنْ جُهَيْنَةَ فَصَبَّحْنَا القَوْمَ عَلَى مِيَاهِهِمْ ، وَلَحقْتُ أنَا وَرَجُلٌ مِنَ الأَنْصَارِ رَجُلاً مِنْهُمْ ، فَلَمَّا غَشَيْنَاهُ ، قَالَ : لاَ إلهَ إلاَّ الله ، فَكفَّ عَنْهُ الأَنْصَاري ، وطَعَنْتُهُ برُمْحِي حَتَّى قَتَلْتُهُ ، فَلَمَّا قَدِمْنَا المَدِينَةَ ، بَلَغَ ذلِكَ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ لِي : (( يَا أُسَامَة ، أقَتَلْتَهُ بَعْدَ مَا قَالَ لا إلهَ إلاَّ اللهُ ؟! )) قُلْتُ : يَا رَسُول الله ، إِنَّمَا كَانَ متعوِّذاً ، فَقَالَ : (( أقَتَلْتَهُ بَعْدَ مَا قَالَ لا إلهَ إلاَّ اللهُ ؟! )) فما زَالَ يُكَرِّرُهَا عَلَيَّ حَتَّى تَمنْيَّتُ أنِّي لَمْ أكُنْ أسْلَمْتُ قَبْلَ ذلِكَ اليَوْمِ . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية : فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( أقالَ : لا إلهَ إلاَّ اللهُ وقَتَلْتَهُ ؟! )) قُلْتُ : يَا رَسُول الله ، إِنَّمَا قَالَهَا خَوْفاً مِن السِّلاحِ ، قَالَ : (( أَفَلاَ شَقَقْتَ عَنْ قَلْبِهِ حَتَّى تَعْلَمَ أَقَالَهَا أمْ لا ؟! )) فمَا زَالَ يُكَرِّرُهَا حَتَّى تَمَنَّيْتُ أنِّي أسْلَمْتُ يَوْمَئذٍ .

Na imepokewa kutoka kwa Usamah bin Zayd (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) amesema, alitutuma Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwenda al-Huraqah, tuliwaamkia asubuhi, tukawashambulia tukawashinda. Mimi na mtu mmoja miongoni mwao, tulipompata akasema: 'Laa ilaaha illa Allaah,' Ansari akamwacha, mimi nikamchoma kwa mkuki wangu nikammuua . Tuliporudi taarifa zikamfikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), naya akaniambia, "Ee Usamah! Umemuua baada ya kuwa amesema, "Laa ilaaha illa Allaah."  Nikasema: "Alikuwa akijisalimisha tu." Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliendelea kulirudia hilo mpaka nikatamani heri nisingekuwa Muislamu kabla ya siku ile." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Katika riwaayah nyingine: Alisema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Amesema Laa ilaaha illa Allaah, nawe ukamuua?" Nikasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Hakika amesema hilo akihofia silaha." Akasema: "Je, uliupasua moyo wake mpaka ukajua kuwa amesema hilo kweli au la." Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliendelea kulirudia hilo mpaka nikatamani nisingekuwa nimesilimu wakati ule.

 

 

Hadiyth – 5

وعن جندب بن عبد الله رضي الله عنه: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم بَعَثَ بَعْثاً مِنَ المُسْلِمينَ إِلَى قَومٍ مِنَ المُشرِكينَ ، وَأنَّهُمْ التَقَوْا ، فَكَانَ رَجُلٌ مِنَ المُشْركينَ إِذَا شَاءَ أنْ يَقْصِدَ إِلَى رَجُل مِنَ المُسْلِمينَ قَصَدَ لَهُ فَقَتَلَهُ ، وَأنَّ رَجُلاً مِنَ المُسْلِمِينَ قَصَدَ غَفْلَتَهُ . وَكُنَّا نتحَدَّثُ أنَّهُ أُسَامَةُ بْنُ زَيْدٍ ، فَلَمَّا رَفَعَ عَلَيهِ السَّيفَ ، قَالَ : لا إلهَ إلاَّ اللهُ ، فَقَتَلهُ ، فَجَاءَ البَشيرُ إِلَى رَسُول الله صلى الله عليه وسلم فَسَألَهُ وَأخبَرَهُ ، حَتَّى أخْبَرَهُ خَبَرَ الرَّجُلِ كَيْفَ صَنَعَ ، فَدَعَاهُ فَسَألَهُ ، فَقَالَ : (( لِمَ قَتَلْتَهُ ؟ )) فَقَالَ : يَا رَسُول اللهِ ، أوْجَعَ في المُسلِمِينَ ، وَقَتَلَ فُلاناً وفلاناً ، وسمى لَهُ نَفراً ، وَإنِّي حَمَلْتُ عَلَيهِ ، فَلَمَّا رَأى  السَّيفَ ، قَالَ : لا إلهَ إلاَّ اللهُ . قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم:  (( أقَتَلْتَهُ ؟ )) قَالَ : نَعَمْ . قَالَ : (( فَكَيفَ تَصْنَعُ بلاَ إلهَ إلاَّ اللهُ ، إِذَا جَاءتْ يَوْمَ القِيَامَةِ ؟ )) قَالَ : يَا رَسُول الله ، اسْتَغْفِرْ لِي . قَالَ : (( وكَيفَ تَصْنَعُ بِلا إلهَ إلاَّ الله إِذَا جَاءتْ يَوْمَ القِيَامَةِ ؟ )) فَجَعَلَ لاَ يَزِيدُ عَلَى أنْ يَقُولَ : (( كَيفَ تَصْنَعُ بِلا إلهَ إلاَّ الله إِذَا جَاءتْ يَوْمَ القِيَامَةِ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Jundub bin 'Abdillaah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alituma Waisilamu kwa watu wa washirikina. Nao wakakautana, ikawa mtu katika washirikina akimkusudia mtu katika Waislamu anamkusudia na anamuua, Nakuwa mtu miongoni mwa Waislamu anakusudia kutaka kumuua, Tulikuwa tunahadithia kuwa huyo Usamah bin Zayd. Aliponyanyua upanga wake, yule mtu alisema: 'Laa ilaaha illa Allaah,' naye akamuua. Akaja mwenye kuleta bishara kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), akamuuliza akampa habari hadi akampa ya mtu yule alichofanya, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimuita Usaamah akamuuliza, akasema: "Kwa nini umemuua?" Akasema: "Ee Rasuli wa Allaah!, Ameumiza Waislamu, amemuua fulani na fulani akataja watu, Hivyo, nilimwendea na alipouona upanga ndipo alipotamka, 'Laa ilaaha illa Allaah'." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Je, umemuua?" Akasema: "Ndio." Akasema: "Siku ya Qiyaamah utasema kitu gani kwa kutamka kwake Laa ilaaha illa Allaah?" Akasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Niombee maghfirah." Akasema: "Siku ya Qiyaamah utasema kitu gani kwa kutamka kwake Laa ilaaha illa Allaah?" Na akawa hazidishi kauli yake: ""Siku ya Qiyaamah utasema kitu gani kwa kutamka kwake Laa ilaaha illa Allaah?" [Muslim]

 

 

Hadiyth – 6

وعن عبد الله بن عتبة بن مسعود ، قَالَ : سَمِعْتُ عمر بن الخطاب رضي الله عنه، يقولُ : إنَّ نَاساً كَانُوا يُؤْخَذُونَ بِالوَحْيِ في عَهْدِ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، وَإنَّ الوَحْيَ قَدِ انْقَطَعَ ، وإِنَّمَا نَأخُذُكُمُ الآن بما ظَهَرَ لَنَا مِنْ أعمَالِكُمْ ، فَمَنْ أظْهَرَ لَنَا خَيْراً أمَّنَّاهُ وَقَرَّبْنَاهُ ، وَلَيْسَ لَنَا مِنْ سَرِيرَتِهِ شَيْء ، اللهُ يُحَاسِبُهُ فِي سَرِيرَتِهِ ، وَمَنْ أظْهَرَ لَنَا سُوءاً لَمْ نَأمَنْهُ وَلَمْ نُصَدِّقْهُ وَإنْ قَالَ : إنَّ سَرِيرَتَهُ حَسَنَةٌ . رواه البخاري .

Toka kwa 'Abdillaah bin Mas'uwd amesema: "Nimemsikia 'Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiyah Allaahu 'anhu) anasema: "Watu walikuwa wakihukumiwa kwa Wahyi wakati wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), Wahyi umekatika, sasa tunawahukumu kwa amali zenu zilizotudhihirikia, Hivyo mwenye kutudhihirishia kheri tutamuamini na kumkaribisha, na si juu yetu kuchunguza chochote katika siri zake, Allaah atamhesabu katika siri zake, Na anayotudhihirishia uovu hatutomuamini wala hatumsadiki japo atasema: Hakika niya yangu ni nzuri." [Al-Bukhaariy]

 

 

 

 

Share