052-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ubora wa Matarajio Mema
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب فضل الرجاء
052-Mlango Wa Ubora wa Matarajio Mema
قَالَ الله تَعَالَى:
وَأُفَوِّضُ أَمْرِي إِلَى اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ﴿٤٤﴾
Na naaminisha mambo yangu kwa Allaah. Hakika Allaah ni Mwenye kuona waja Wake. [Ghaafir: 44]
فَوَقَاهُ اللَّـهُ سَيِّئَاتِ مَا مَكَرُوا ۖ ﴿٤٥﴾
Basi Allaah Akamlinda na maovu ya yale waliyoyapangia njama. [Ghaafir: 45]
Hadiyth – 1
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم، أَنَّهُ قَالَ : (( قَالَ الله (عزّ وجلّ) : أَنَا عِنْدَ ظَنِّ عَبْدِي بِي ، وَأَنا معه حَيْثُ يَذْكُرنِي ، وَاللهِ ، للهُ أفْرَحُ بِتَوبَةِ عَبْدِهِ مِنْ أحَدِكُمْ يَجِدُ ضَالَّتَهُ بالفَلاَةِ ، وَمَنْ تَقَرَّبَ إلَيَّ شِبْراً ، تَقَرَّبْتُ إِلَيْهِ ذِرَاعاً ، وَمَنْ تَقَرَّبَ إِلَيَّ ذِرَاعاً ، تَقَرَّبْتُ إِلَيْهِ بَاعاً ، وَإِذَا أقْبَلَ إِلَيَّ يَمْشِي أقْبَلْتُ إِلَيْهِ أُهَرْوِلُ )) متفقٌ عليه ، وهذا لفظ إحدى روايات مسلم . وتقدم شرحه في الباب قبله.
Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema kuwa: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: Amesema Allaah ('Azza wa Jalla): "Hakika Mimi namchukulia mja kwa anavyonichukulia, Nami nipo pamoja naye pale anaponitaja. Naapa kwa Allaah! Allaah ana furaha zaidi kwa toba ya mja Wake kuliko mmoja wenu anayempata ngamia wake aliyepotea jangwani. Na yeyote anayekuja karibu Nami kwa shibiri, Mimi nakuja karibu yake kwa dhiraa. Yule anayekuja karibu Nami kwa dhiraa, Mimi nakuja kwake kwa kiasi cha pima moja. Na anayekuja Kwangu kwa kutembea, Mimi nakuja kwake kwa kukimbia." [Al-Bukhaariy na Muslim]. Na hii ni lafdhi moja wapo ya riwaayah ya Muslim. Na imepokewa katika Swahiyh mbili: "Nami niko pamoja naye anaponikumbuka na kunitaja."
Hadiyth – 2
وعن جابر بن عبد الله رضي الله عنهما : أنه سمع رسول الله صلى الله عليه وسلم قبلَ مَوْتِه بثَلاثَةِ أيّام ، يقولُ : (( لاَ يَمُوتَنّ أحَدُكُمْ إِلاَّ وَهُوَ يُحْسِنُ الظَّنَّ بالله (عزّ وجلّ) )) رواه مسلم .
Na imepokewa kutoka kwa Jaabir bin 'Abdillaah (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) kuwa yeye amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kabla ya mauti yake kwa siku tatu akisema: "Asife mmoja wenu isipokuwa atarajie mema na mazuri kutoka kwa Allaah ('Azza wa Jalla)." [Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أنس رضي الله عنه، قَالَ : سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( قَالَ الله تَعَالَى : يَا ابْنَ آدَمَ ، إنَّكَ ما دَعَوْتَنِي وَرَجَوْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ عَلَى مَا كَانَ مِنْكَ وَلاَ أُبَالِي . يَا ابْنَ آدَمَ ، لَوْ بَلَغت ذُنُوبُك عَنَانَ السماءِ ، ثُمَّ اسْتَغْفَرْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ وَلاَ أُبَالِي . يَا ابْنَ آدَمَ ، إِنَّكَ لَوْ أتَيْتَنِي بِقُرَابِ الأَرْضِ خَطَايا ، ثُمَّ لَقَيْتَنِي لاَ تُشْرِكُ بِي شَيْئاً ، لأَتَيْتُكَ بقُرَابِها مَغْفِرَةً )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa amemsikia Rasuli wa Allaahu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema kwamba Allaah Ta'aalaa amesema: "Ee binadamu, hakika wewe kila unapoendelea kuniomba na kunitarajia, basi Nitakusamehe dhambi ulizonazo wala sijali. Ee binadamu, hata kama dhambi zako zikifika mpaka mawinguni, kisha ukaniomba msamaha, Nitakughufiria. Ee binadamu, hakika wewe lau wanijia na makosa yenye kujaa ardhi kisha ukanikabili Mimi na hali hunishirikishi na kitu chochote, basi Nitakupa mfano wake maghfira." [At-Tirmidhiy, na alisema ni Hadiyth Hasan.