053-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kujumuisha Baina ya Hofu na Matarajio
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب الجمع بين الخوف والرجاء
053-Mlango Wa Kujumuisha Baina ya Hofu na Matarajio
اعْلَمْ أنَّ المُخْتَارَ لِلْعَبْدِ في حَالِ صِحَّتِهِ أنْ يَكُونَ خَائفاً رَاجِياً ، وَيَكُونَ خَوْفُهُ وَرَجَاؤُهُ سَواءً ، وفي حَالِ المَرَضِ يُمحَّضُ الرَّجاءُ ، وقواعِدُ الشَّرْع مِنْ نصُوصِ الكِتَابِ والسُّنَةِ وغَيْرِ ذَلِكَ مُتظاهِرَةٌ عَلَى ذلك .
Imam An-Nawawiy anasema: "Mja wa Allaah anatakiwa ajue ya kwamba inapendeza kwake akiwa katika hali ya siha nzuri awe ni mwenye kuwa na hofu kwa Allaah Ta'aalaa na matarajio. Na hofu yake na matumaini yake yawe sawa sawa. Na anapokuwa mgonjwa anatakiwa awe na Imani thabiti pamoja na matarajio yaliyo makubwa zaidi. Katika hili kanuni za sheria ya Kiislamu zipo wazi kabisa kwa naswi (maandiko) katika Kitabu (Qur-aan) na Sunnah na nyinginezo."
قَالَ الله تَعَالَى:
فَلَا يَأْمَنُ مَكْرَ اللَّـهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْخَاسِرُونَ ﴿٩٩﴾
Basi hawaaminishi mipango ya Allaah isipokuwa watu wenye kukhasirika. [Al-A'raaf: 99]
إِنَّهُ لَا يَيْأَسُ مِن رَّوْحِ اللَّـهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْكَافِرُونَ ﴿٨٧﴾
Hakika hawakati tamaa na faraja ya Allaah isipokuwa watu makafiri. [Yuwsuf: 87]
يَوْمَ تَبْيَضُّ وُجُوهٌ وَتَسْوَدُّ وُجُوهٌ ۚ ﴿١٠٦﴾
Siku nyuso zitakuwa nyeupe na nyuso (nyingine) zitakuwa nyeusi. [Aal-'Imraan: 106]
إِنَّ رَبَّكَ سَرِيعُ الْعِقَابِ وَإِنَّهُ لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٦٥﴾
Hakika Rabb wako ni Mwepesi wa kuakibu, na hakika Yeye bila shaka ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Al-An'aam: 165]
إِنَّ الْأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ ﴿١٣﴾ وَإِنَّ الْفُجَّارَ لَفِي جَحِيمٍ ﴿١٤﴾
Hakika Waumini watendao mema kwa wingi bila shaka watakuwa katika neema (taanasa, furaha n.k). Na hakika watendao dhambi bila shaka watakuwa katika moto uwakao vikali mno. [Al-Infitwaar: 13-14]
فَأَمَّا مَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ ﴿٦﴾ فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ ﴿٧﴾ وَأَمَّا مَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ ﴿٨﴾ فَأُمُّهُ هَاوِيَةٌ ﴿٩﴾
Basi yule itakayekuwa mizani yake nzito. Huyo atakuwa katika maisha ya kuridhisha. Na yule itakayekuwa mizani yake khafifu.Basi makazi yake ni Haawiyah. [Al-Qaari-'ah: 6-9]
Hadiyth – 1
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( لَوْ يَعْلَمُ الْمُؤمِنُ مَا عِنْدَ الله مِنَ العُقُوبَةِ ، مَا طَمِعَ بِجَنَّتِهِ أَحَدٌ ، وَلَوْ يَعْلَمُ الكَافِرُ مَا عِنْدَ الله مِنَ الرَّحْمَةِ ، مَا قَنَطَ مِنْ جَنَّتِهِ أحَدٌ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Lau kama Muumini atajua ile adhabu kamili ya Allaah, hangetamani yeyote Pepo Yake. Na lau kafiri angejua kwa ukamilifu wake rehema aliyonayo Allaah, asingekata tamaa yeyote na Pepo Yake." [Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أَبي سعيد الخدرِيِّ رضي الله عنه: أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( إِذَا وُضِعَتِ الجنازةُ واحْتَمَلَهَا النَّاسُ أَوِ الرِّجَالُ عَلَى أعناقِهِمْ ، فَإنْ كَانَتْ صَالِحَةً ، قالتْ: قَدِّمُونِي قَدِّمُونِي ، وَإنْ كَانَتْ غَيْرَ صَالِحَةٍ ، قالتْ : يَا وَيْلَهَا ! أَيْنَ تَذْهَبُونَ بها ؟ يَسْمَعُ صَوْتَها كُلُّ شَيْءٍ إِلاَّ الإنْسانُ ، وَلَوْ سَمِعَهُ صَعِقَ )) رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Itakapokuwa tayari jeneza na ikabebwa na watu juu ya mabega yao, akiwa ni mtu mwema atasema: 'Nipelekeni mbele, nipelekeni mbele. Na ikiwa si mwema, atasema: 'Ole wake! Mnanipeleka wapi?' Sauti yake inasikika na kila kitu isipokuwa mwanadamu na lau angesikia (mwanadamu) basi angezimia." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 3
وعن ابن مسعود رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( الجَنَّةُ أقْرَبُ إِلى أحَدِكُمْ مِنْ شِرَاكِ نَعْلِهِ ، وَالنَّارُ مِثْلُ ذلك )) رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uud (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (SWalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Pepo ipo karibu sana na mmoja wenu kuliko kamba zake za viatu na Moto ni mfano wa hivyo." [Al-Bukhaariy]