056-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila za Kuwa na Njaa na Maisha ya Kujinyima, na Kukusuru Kichache Katika Chakula na Vinywaji na Mavazi na Kujitenga na Maisha ya Fakhari na Kuacha Matamanio
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب فضل الجوع وخشونة العيش والاقتصار عَلَى القليل من المأكول والمشروب والملبوس وغيرها من حظوظ النفس وترك الشهوات
056-Mlango Wa Fadhila za Kuwa na Njaa na Maisha ya Kujinyima, na Kukusuru Kichache Katika Chakula na Vinywaji na Mavazi na Kujitenga na Maisha ya Fakhari na Kuacha Matamanio
قَالَ الله تَعَالَى:
فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ أَضَاعُوا الصَّلَاةَ وَاتَّبَعُوا الشَّهَوَاتِ ۖ فَسَوْفَ يَلْقَوْنَ غَيًّا ﴿٥٩﴾ إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ وَلَا يُظْلَمُونَ شَيْئًا ﴿٦٠﴾
Wakafuata baada yao waovu, walipoteza Swalaah na wakafuata matamanio; basi watakutana na adhabu motoni. Isipokuwa yule aliyetubu na akaamini na akatenda mema; basi hao wataingia Jannah na wala hawatodhulumiwa chochote. [Maryam: 59-60]
فَخَرَجَ عَلَىٰ قَوْمِهِ فِي زِينَتِهِ ۖ قَالَ الَّذِينَ يُرِيدُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا يَا لَيْتَ لَنَا مِثْلَ مَا أُوتِيَ قَارُونُ إِنَّهُ لَذُو حَظٍّ عَظِيمٍ ﴿٧٩﴾ وَقَالَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ وَيْلَكُمْ ثَوَابُ اللَّـهِ خَيْرٌ لِّمَنْ آمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا وَلَا يُلَقَّاهَا إِلَّا الصَّابِرُونَ ﴿٨٠﴾
Akawatokea watu wake katika pambo lake. Wale wanaotaka uhai wa dunia wakasema: Ee laiti tungelipata mfano wa yale aliyopewa Qaaruwn, hakika yeye ana bahati kuu. Na wale waliopewa elimu wakasema: Ole wenu! Thawabu za Allaah ni bora zaidi kwa yule aliyeamini na akatenda mema. Na wala hazipati isipokuwa wenye kusubiri. [Al-Qaswasw: 79-80]
ثُمَّ لَتُسْأَلُنَّ يَوْمَئِذٍ عَنِ النَّعِيمِ ﴿٨﴾
Kisha bila shaka mtaulizwa Siku hiyo kuhusu neema. [At-Takaathur: 8]
مَّن كَانَ يُرِيدُ الْعَاجِلَةَ عَجَّلْنَا لَهُ فِيهَا مَا نَشَاءُ لِمَن نُّرِيدُ ثُمَّ جَعَلْنَا لَهُ جَهَنَّمَ يَصْلَاهَا مَذْمُومًا مَّدْحُورًا ﴿١٨﴾
Yeyote anayetaka (starehe za dunia) ipitayo upesi upesi Tunamharakizia humo Tuyatakayo, na kwa Tumtakaye. Kisha Tutamjaalia Jahannam aingie na kuungua hali ya kuwa mwenye kushutumiwa na kufukuziliwa mbali. [Al-Israa: 18]
Hadiyth – 1
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : مَا شَبعَ آلُ مُحَمّد صلى الله عليه وسلم مِنْ خُبْزِ شَعِيرٍ يَوْمَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ حَتَّى قُبِضَ . متفقٌ عَلَيْهِ .
وفي رواية : مَا شَبعَ آلُ محَمّد صلى الله عليه وسلم مُنْذُ قَدِمَ المَدِينَةَ مِنْ طَعَامِ البُرِّ ثَلاثَ لَيَالٍ تِبَاعاً حَتَّى قُبِضَ.
Kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: "Haikushiba familia ya Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mkate wa shayiri siku mbili mfululizo hadi ameaga dunia (hali ilikuwa hivyo)." [Al-Bukhaariy na Muslim].
Na katika riwaayah nyingine: "Haikushiba familia ya Muhammad (Sawalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuanzia afike Madiynah kwa chakula cha ngano kwa siku tatu mfululizo mpaka ameaga dunia."
Hadiyth – 2
وعن عروة ، عن عائشة رضي الله عنها ، أنّها كَانَتْ تقول : وَاللهِ ، يَا ابْنَ أُخْتِي ، إنْ كُنَّا نَنْظُرُ إِلَى الهِلاَلِ ، ثُمَّ الهِلالِ : ثَلاَثَةُ أهلَّةٍ في شَهْرَيْنِ ، وَمَا أُوقِدَ في أبْيَاتِ رسول الله صلى الله عليه وسلم نَارٌ . قُلْتُ : يَا خَالَةُ ، فَمَا كَانَ يُعِيشُكُمْ ؟ قالت : الأَسْوَدَانِ التَّمْرُ وَالمَاءُ ، إِلاَّ أنَّهُ قَدْ كَانَ لرسول الله صلى الله عليه وسلم جِيرَانٌ مِنَ الأَنْصَارِ ، وكَانَتْ لَهُمْ مَنَائِحُ وَكَانُوا يُرْسِلُونَ إِلَى رسول الله صلى الله عليه وسلم مِنْ ألْبَانِهَا فَيَسْقِينَا . متفقٌ عَلَيْهِ .
Na imepokewa kutoka kwa 'Urwah, kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa yeye alikuwa anasema: "Naapa kwa Allaah! Ee kijana wa dadangu, tulikuwa tunaona mwezi, kisha mwezi mwingine, na kisha mwezi mwengine: Miandamo mitatu katika miezi miwili na hakukuwa kukiwashwa moto katika nyumba za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)." Nikasema: "Ee halati yangu! Mlikuwa mkila nini?" Akasema: "Vitu Vyeusi viwili: Tende na maji isipokuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na majirani wa ki-Answaar ambao walikuwa wakimletea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) maziwa tuliokuwa tukinywa." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أَبي سعيد المقبُريِّ ، عن أَبي هريرة رضي الله عنهما: أَنَّهُ مَرَّ بِقَومٍ بَيْنَ أيدِيهمْ شَاةٌ مَصْلِيَّةٌ ، فَدَعَوْهُ فَأبَى أنْ يأْكُلَ . وقال : خرج رسول الله صلى الله عليه وسلم مِنَ الدُّنْيَا وَلَمْ يَشْبَعْ مِنْ خُبْزِ الشَّعيرِ . رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Abuu sa'iyd Al-Maqburiyy kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba mara moja alipita baina ya watu waliokuwa wakichoma mbuzi, walimuita lakini alikataa kula. Akasema: "Aliondoka Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) duniani na wala hakushiba hata siku moja makte wa mtama." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 4
وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : لَمْ يَأكُلِ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم عَلَى خِوَانٍ حَتَّى مَاتَ ، وَمَا أكَلَ خُبْزاً مُرَقَّقاً حَتَّى مَاتَ . رواه البخاري .
وفي رواية لَهُ : وَلاَ رَأى شَاةً سَمِيطاً بعَيْنِهِ قَطُّ .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: "Hakula Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya meza mpaka akafariki. Na wa hakula mkate mzuri na laini mpaka akaaga dunia." [Al-Bukhaariy]
Katika riwaayah nyengine: "Wala hakumuona kabisa mbuzi mzima aliyechomwa."
Hadiyth – 5
وعن النعمان بن بشير رضي الله عنهما ، قَالَ : لَقَدْ رَأيْتُ نَبيَّكُمْ صلى الله عليه وسلم ، وَمَا يَجِدُ مِنَ الدَّقَلِ مَا يَمْلأُ بِهِ بَطْنَهُ . رواه مسلم .
Na imepokewa kutoka kwa an-Nu'maan bin Bashiyr (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba amesema: "Hakika nimemuona Nabiy wenu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye hakuweza kupata hata tende mbaya ambazo zitamshibisha." [Muslim]
Hadiyth – 6
وعن سهلِ بن سعد رضي الله عنه، قَالَ : مَا رَأى رسول الله صلى الله عليه وسلم النَّقِيَّ مِنْ حِين ابْتَعَثَهُ الله تَعَالَى حَتَّى قَبضَهُ الله تَعَالَى . فقِيلَ لَهُ : هَلْ كَانَ لَكُمْ في عَهدِ رسول الله صلى الله عليه وسلم مَنَاخِلُ ؟ قَالَ : مَا رَأى رسول الله صلى الله عليه وسلم مُنْخُلاً مِنْ حِينَ ابْتَعَثَهُ اللهُ تَعَالَى حَتَّى قَبَضَهُ اللهُ تَعَالَى ، فَقِيلَ لَهُ : كَيْفَ كُنْتُمْ تَأكُلُونَ الشَّعِيرَ غَيْرَ مَنْخُولٍ ؟ قَالَ : كُنَّا نَطحَنُهُ وَنَنْفُخُهُ ، فيَطيرُ مَا طَارَ ، وَمَا بَقِيَ ثَرَّيْنَاهُ . رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Sahl bin Sa'ad (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Hakuona mkate wa unga safi tangu Allaah Ta'aalaa Alipomtuma mpaka Allaah Ta'aalaa alipomfisha. Akauliza: "Je, katika zama za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mlikuwa na chekeche?" Akasema: "Hakuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kichungio tangu Allaah Ta'aalaa Alipomtuma hadi Allaah Ta'aalaa alipomfisha." Akauliza: "Mlikuwa mkila vipi shayiri isiochekechwa?" Akasema: "Tulikuwa tukiitwanga na kuipulizia, hupeperuka zinazopeperuka na kilichobaki tunakanda." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 7
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : خرجَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم ذَاتَ يَوْمٍ أَوْ لَيْلَةٍ ، فَإذَا هُوَ بأَبِي بَكْرٍ وَعُمَرَ رضي الله عنهما ، فَقَالَ : (( مَا أخْرَجَكُمَا مِنْ بُيُوتِكُما هذِهِ السَّاعَةَ ؟ )) قَالا : الجُوعُ يَا رسول الله . قَالَ : (( وَأنَا ، وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ ، لأخْرَجَنِي الَّذِي أخْرَجَكُما ، قُوما )) فقَامَا مَعَهُ ، فَأتَى رَجُلاً مِنَ الأَنْصَارِ ، فَإذَا هُوَ لَيْسَ في بيْتِهِ ، فَلَمَّا رَأَتْهُ المَرْأَةُ ، قالت : مَرْحَبَاً وَأهلاً .فقال لَهَا رسول الله صلى الله عليه وسلم:(( أيْنَ فُلانُ ؟ )) قالت : ذَهَبَ يَسْتَعْذِبُ لنَا المَاءَ . إِذْ جَاءَ الأَنْصَارِيُّ ، فَنَظَرَ إِلَى رسول الله صلى الله عليه وسلم وَصَاحِبَيْهِ ، ثُمَّ قَالَ : الحَمْدُ للهِ ، مَا أَحَدٌ الْيَوْمَ أكْرَمَ أضْيَافاً مِنِّي ، فَانْطَلَقَ فَجَاءهُمْ بِعِذْقٍ فِيهِ بُسْرٌ وَتَمْرٌ وَرُطَبٌ ، فَقَالَ : كُلُوا ، وَأَخَذَ الْمُدْيَةَ ، فَقَالَ لَهُ رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( إيْاكَ وَالْحَلُوبَ )) فَذَبَحَ لَهُمْ ، فَأكَلُوا مِنَ الشَّاةِ وَمِنْ ذَلِكَ العِذْقِ وَشَرِبُوا . فَلَمَّا أنْ شَبِعُوا وَرَوُوا قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم لأَبي بَكْر وَعُمَرَ رضي الله عنهما : (( وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ ، لَتُسْأَلُنَّ عَنْ هَذَا النَّعِيمِ يَوْمَ القِيَامَةِ ، أَخْرَجَكُمْ مِنْ بُيُوتِكُمُ الْجُوعُ ، ثُمَّ لَمْ تَرْجِعُوا حَتَّى أصَابَكُمْ هَذَا النَّعيمُ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Alitoka Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) siku moja au usiku, akakutana na Abuu Bakr na 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhummaa) Akasema: "Nini kilichowatoa katika majumba yenu saa hii?" Wakasema: "Njaa ee Rasuli wa Allaah." Akasema: "Naapa kwa ambaye nafsi yangu iko mkononi Mwake, mimi pia kimenitoa nyumbani kwangu kilichowatoa nyie, simameni" Wakasimama pamoja naye Akaja mtu wa Ki-Answaar, lakini hakuwa nyumbani kwake. Mkewe alipowaona, alisema: "Karibuni sana." Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamuuliza: "Fulani yuko wapi?" Akasema: "Amekwenda kututekea maji." Mara akarudi yule Answaar akamwangalia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na rafiki zake, kisha akasema: "Alhamdulillaah." Hakuna leo mwenye wegeni watukufu kuniliko." Akatoka na kurudi huku amekuja na kitagaa chenye tende mbivu na mbichi. Akasema: "Kuleni naye" akachukua kisu kuwachinjia mbuzi. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: "Usichinje mwenye maziwa." Wakala mbuzi waliochinjiwa, wakala na tende na kunywa maji. Waliposhiba na kukata kiu, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaambia Abu Bakr na 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): "Naapa kwa ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake, Mtaulizwa neema hii Siku ya Qiyaamah. Lililowatoeni majumbani mwenu ni njaa, lakini kabla ya kurudi (majumbani kwenu) mmepata neema hii." [Muslim]
Hadiyth – 8
وعن خالد بن عُمَيْر العَدَوِيِّ ، قَالَ : خَطَبَنَا عُتْبَةُ بنُ غَزْوَانَ ، وَكَانَ أمِيراً عَلَى البَصْرَةِ ، فَحَمِدَ الله وَأثْنَى عَلَيْهِ ، ثُمَّ قَالَ : أَمَّا بَعْدُ ، فَإِنَّ الدُّنْيَا قَدْ آذَنَتْ بِصُرْمٍ ، وَوَلَّتْ حَذَّاءَ ، وَلَمْ يَبْقَ مِنْهَا إِلاَّ صُبَابَةٌ كَصُبَابَةِ الإنَاءِ يَتَصَابُّهَا صَاحِبُهَا ، وَإِنَّكُمْ مُنْتَقِلُونَ مِنْهَا إِلَى دَارٍ لاَ زَوَالَ لَهَا ، فَانْتَقِلُوا بِخَيرِ مَا بِحَضْرَتِكُمْ ، فَإِنَّهُ قَدْ ذُكِرَ لَنَا أنَّ الحَجَرَ يُلْقَى مِنْ شَفِيرِ جَهَنَّمَ فَيَهْوِي فِيهَا سَبْعِينَ عَاماً ، لاَ يُدْرِكُ لَهَا قَعْراً ، وَاللهِ لَتُمْلأَنَّ أَفَعَجِبْتُمْ ؟! وَلَقدْ ذُكِرَ لَنَا أنَّ مَا بَيْنَ مِصْرَاعَيْنِ مِنْ مَصَارِيعِ الْجَنَّةِ مَسيرَةُ أرْبَعِينَ عَاماً ، وَليَأتِيَنَّ عَلَيْهَا يَوْمٌ وَهُوَ كَظِيظٌ مِنَ الزِّحَامِ ، وَلَقَدْ رَأيْتُنِي سَابعَ سَبْعَةٍ مَعَ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، مَا لَنَا طَعَامٌ إِلاَّ وَرَقُ الشَّجَرِ ، حَتَّى قَرِحَتْ أشْدَاقُنَا ، فَالتَقَطْتُ بُرْدَةً فَشَقَقْتُهَا بَيْنِي وَبَيْنَ سَعْدِ بْنِ مَالِكٍ ، فاتَّزَرْتُ بِنِصْفِهَا ، وَاتَّزَرَ سَعْدٌ بِنِصْفِهَا ، فَمَا أصْبَحَ اليَوْمَ مِنَّا أحَدٌ إِلاَّ أَصْبَحَ أمِيراً عَلَى مِصرٍ مِنَ الأَمْصَارِ ، وَإنِّي أعُوذُ بِاللهِ أنْ أكُونَ فِي نَفْسِي عَظِيماً ، وَعِنْدَ اللهِ صَغِيراً .
رواه مسلم .
Na imepokewa kutoka kwa Khaalid bin 'Umayr Al-'Adawiy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Alituhutubia 'Utbah bin Ghazwaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) naye alikuwa ni Amiri wa Basrah. Alimuhimidi Allaah na kumtukuza, kisha akasema: "Ama baada ya hayo! Kwa hakika dunia inatangaza kumalizika kwake na imegeuza uso wake na inakimbia kwa haraka sana. Dunia imebakia ndogo sana kama mfano wa matone yanayobaki baada ya mtu kunywa maji kutoka kwenye chombo. Wapenzi wa dunia wanakunywa matone hayo. Na hakika nyinyi mtakuwa ni wenye kuhamishwa kutoka katika nyumba yenye kudumu milele. Hivyo, yakinisha kuwa utakwenda huko na vile vitu vizuri kabisa ulivyonavyo. Tumeelezwa ya kwamba jiwe litakuwa ni lenye kurushwa kwenye mdomo wa Jahanamu ambalo litachukua miaka sabiini kufika chini. Naapa kwa Allaah kuwa sehemu hiyo itajazwa (na watu waovu). Je, mnastaajabu? Na hakika tuliambiwa ya kwamba masafa baina ya mbao mbili za mlango wa Peponi ni mwendo wa miaka arobaini. Mbali ya hiyo itafika siku ambapo halaiki ya watu itajaa kwenye mlango huo. Nakumbuka nilipokuwa mmoja wa watu saba waliokuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakati ambao hatukuwa na chochote cha kula ila majani ya miti mpaka midomo yetu ikapata majeraha ya kupasuka pasuka. Hata hivyo nilipata kitambara ambacho nilikikata vipande viwili, kimoja nikatumia mimi na nusu ya pili nikampatia Sa'ad bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu). Ama leo kila moja miongoni mwetu ni Amiri wa mji miongoni mwa miji. Na kwa hakika mimi, najilinda kwa Allaah kwa hilo, kuwa katika nafsi yangu kujiona mtukufu na mbele ya Allaah nikawa mdogo sana." [Muslim]
Hadiyth – 9
وعن أَبي موسى الأشعري رضي الله عنه، قَالَ : أخْرَجَتْ لَنَا عَائِشَةُ رضي الله عنها كِسَاءً وَإزاراً غَلِيظاً ، قالَتْ : قُبِضَ رسول الله صلى الله عليه وسلم في هَذَيْنِ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abuu Muwsaa Al-Asha'ariy kwamba amesema: "Alituonyesha 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kitambara na kikoi kigumu, akasema: 'Ameaga dunia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa na nguo hizi mbili pekee." [Al-Bukhaariy na Muuslim]
Hadiyth – 10
وعن سعد بن أَبي وقاص رضي الله عنه، قَالَ : إنِّي لأَوَّلُ الْعَرَبِ رَمَى بِسَهْمٍ في سَبِيلِ الله ، وَلَقَدْ كُنَّا نَغْزُو مَعَ رسول الله صلى الله عليه وسلم مَا لَنَا طَعَامٌ إِلاَّ وَرَقُ الْحُبْلَةِ ، وَهذَا السَّمُرُ ، حَتَّى إنْ كَانَ أحَدُنَا لَيَضَعُ كَمَا تَضَعُ الشَّاةُ مَا لَهُ خَلْطٌ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Sa'ad bin Abuu Waqqaas (Radhwiya Allaah 'anhu) kwamba amesema: "Mimi nilikuwa Muarabu wa kwanza kurusha mshale katika njia ya Allaah. Tulikuwa tukipigana (katika Jihad) pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hatuna kabisa chakula isipokuwa majani ya miti ya jangwani (kama acacia). Hivyo kukifanya choo chetu kuwa kigumu kama kinyesi cha mbuzi." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 11
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( اللَّهُمَّ اجْعَلْ رِزْقَ آلِ مُحَمّدٍ قُوتاً )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ee Allaah! Ijaalie riziki ya familia ya Muhammad iwe ni yenye kutosha." [Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhiy]
Hadiyth – 12
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : وَاللهِ الَّذِي لاَ إِلهَ إِلاَّ هُوَ ، إنْ كُنْتُ لأَعْتَمِدُ بِكَبِدِي عَلَى الأَرْضِ مِنَ الجُوعِ ، وَإنْ كُنْتُ لأَشُدُّ الحَجَرَ عَلَى بَطنِي مِنَ الْجُوعِ . وَلَقَدْ قَعَدْتُ يَوماً عَلَى طَرِيقِهِمُ الَّذِي يَخْرُجُونَ مِنْهُ ، فَمَرَّ بِي النبي صلى الله عليه وسلم ، فَتَبَسَّمَ حِيْنَ رَآنِي ، وَعَرَفَ مَا فِي وَجْهِي وَمَا فِي نَفْسِي ، ثُمَّ قَالَ : (( أَبَا هِرٍّ )) قُلْتُ : لَبَّيْكَ يَا رسول الله ، قَالَ : (( الْحَقْ )) وَمَضَى فَاتَّبَعْتُهُ ، فَدَخَلَ فَاسْتَأذَنَ ، فَأَذِنَ لِي فَدَخَلْتُ ، فَوَجَدَ لَبَنَاً في قَدَحٍ ، فَقَالَ : (( مِنْ أَيْنَ هَذَا اللَّبَنُ ؟ )) قَالُوا : أهْدَاهُ لَكَ فُلانٌ – أَو فُلانَةٌ – قَالَ : (( أَبَا هِرٍّ )) قلتُ : لَبَّيْكَ يَا رسول اللهِ ، قَالَ : (( الْحَقْ إِلَى أهْلِ الصُّفَّةِ فَادْعُهُمْ لِي )) قَالَ : وَأهْلُ الصُّفَّة أضْيَافُ الإِسْلاَمِ ، لاَ يَأوُونَ علَى أهْلٍ وَلاَ مَالٍ وَلاَ عَلَى أحَدٍ ، وَكَانَ إِذَا أتَتْهُ صَدَقَةٌ بَعَثَ بِهَا إلَيْهِمْ ، وَلَمْ يَتَنَاوَلْ مِنْهَا شَيْئاً ، وَإِذَا أتَتْهُ هَدِيَّةٌ أرْسَلَ إلَيْهِمْ ، وَأصَابَ مِنْهَا ، وأشْرَكَهُمْ فِيهَا . فَسَاءنِي ذَلِكَ ، فَقُلْتُ : وَمَا هَذَا اللَّبَنُ في أهْلِ الصُّفَّةِ ! كُنْتُ أحَقُّ أنْ أُصِيبَ مِنْ هَذَا اللَّبَنِ شَرْبَةً أتَقَوَّى بِهَا ، فَإذَا جَاءُوا وَأمَرَنِي فَكُنْتُ أنَا أُعْطِيهِمْ ؛ وَمَا عَسَى أنْ يَبْلُغَنِي مِنْ هَذَا اللَّبَنِ . وَلَمْ يَكُنْ مِنْ طَاعَةِ اللهِ وَطَاعَةِ رسول الله صلى الله عليه وسلم بُدٌّ ، فَأَتَيْتُهُمْ فَدَعَوْتُهُمْ ، فَأقْبَلُوا وَاسْتَأذَنُوا ، فَأَذِنَ لَهُمْ وَأخَذُوا مَجَالِسَهُمْ مِنَ الْبَيْتِ ، قَالَ : (( يَا أَبَا هِرٍّ )) قُلْتُ: لَبَّيْكَ يَا رسول الله ، قَالَ : (( خُذْ فَأعْطِهِمْ )) قَالَ : فَأخَذْتُ القَدَحَ ، فَجَعَلْتُ أُعْطِيهِ الرَّجُل فَيَشْرَبُ حَتَّى يَرْوَى ، ثُمَّ يَرُدُّ عَلَيَّ الْقَدَحَ ، فَأُعْطِيهِ الرَّجُلَ فَيَشْرَبُ حَتَّى يَرْوَى ، ثُمَّ يَرُدُّ عَلَيَّ الْقَدَحَ ، فَأُعْطِيهِ الرَّجُلَ فَيَشْرَبُ حَتَّى يَرْوَى ، ثُمَّ يَرُدُّ عَلَيَّ الْقَدَحَ حَتَّى انْتَهَيْتُ إِلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، وَقَدْ رَوِيَ الْقَوْمُ كُلُّهُمْ ، فَأخَذَ الْقَدَحَ فَوضَعَهُ عَلَى يَدِهِ ، فَنَظَرَ إليَّ فَتَبَسَّمَ ، فَقَالَ : (( أَبَا هِرٍّ )) قُلْتُ : لَبَّيْكَ يَا رسول الله ، قَالَ : (( بَقيتُ أنَا وَأنْتَ )) قُلْتُ : صَدَقْتَ يَا رسول الله ، قَالَ : (( اقْعُدْ فَاشْرَبْ )) فَقَعَدْتُ فَشَرِبْتُ ، فَقَالَ (( اشْرَبْ )) فَشَرِبْتُ ، فَمَا زَالَ يَقُولُ : (( اشْرَبْ )) حَتَّى قُلْتُ: لا ، وَالَّذِي بَعَثَكَ بِالحَقِّ لاَ أجِدُ لَهُ مَسْلكاً ! قَالَ: (( فَأرِنِي )) فَأعْطَيْتُهُ الْقَدَحَ ، فَحَمِدَ الله تَعَالَى ، وَسَمَّى وَشَرِبَ الفَضْلَةَ . رواه البخاري .
Na imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah amesema: ""Naapa kwa ambaye hapana Mola isipokuwa Yeye, nilikuwa naegemeza tumbo langu ardhini kwa njaa, nikifunga jiwe tumboni mwangu kwa njaa. Siku moja nilikaa juu ya njia yao wanayotokea. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipita akatabasamu aliponiona, akajua kilicho usoni mwangu na yaliyo nafsini mwangu. Alisema: "Abuu Hirr." Nikasema: "Ee Rasuli wa Allaah." Akasema: "Nifuate." Aliondoka nikamfuata. Akabisha hodi akakaribishwa, akaniruhusu kuingia. Akakuta maziwa ndani ya jagi akasema: "Kutoka wapi haya maziwa?" Wakasema: "Fulani amekuzawadia." Akasema: "Abuu Hirr." Nikasema: "Labbayka, ee Rasuli wa Allaah." Akasema: "Nenda kaite watu wa Swuffah." Akasema: "Watu wa Swuffah ni wageni wa Waislamu, hawana isipokuwa jamaa, mali, wala yoyote," Alikuwa akipata swadaqah anawapelekea, hakutumia chochote humo. "Na anapopata zawadi anawapelekea naye anakula humo, na kuwashirikisha humo, Likaniumiza hilo, nikauliza: "Maziwa gani haya kwa watu wa Suwffah?" Nilikuwa na haki zaidi kupata haya maziwa ili yanipe nguvu. Watakapofiks ataniamuru kuwaandalia, pengine yasinifikie maziwa haya, hakukuwa na budi isipokuwa kutii amri ya Allaah na Rasuli Wake." Nilikwenda kuwaita, wakabisha hodi, wakaruhusiwa, wakakaa sehemu yao. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Abuu Hirr." Nikasema: "Labbayka, ee Rasuli wa Allaah." Akasema: "Chukua haya maziwa uwape." Akasema: "Nikachukua kikombe nikaanza kumpa wa kwanza, alikunywa hadi akatosheka. Kisha akanirudishia kikombe, nikampa mwengine hunywa mpaka anatosheka. Kisha hunirudishia kikombe kikamfikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wote wamemaliza kunywa. Nabiy akachukua kikombe mkononi mwake akanitazama akatabasamu, akasema: "Abuu Hirr." Nikasema: "Labbayka, ee rasuli wa Allaah." Akasema: "Tumebaki mimi na wewe." Nikasema: "Ndio, ee Rasuli wa Allaah." Akasema: "Kaa unywe." Nikakaa nakunywa." Akasema: "Kunywa." Nami nikanywa. Hakuacha kusema "Kunywa." Mpaka ikafika wakati nikasema: "Laa, naapa aliyekutuma kwa haki sina nafasi yake." Akasema: "Nipe." Nikampa kikombe, akamuhimidi Allaah, akasema: "Bismillaah, akanywa maziwa yaliyobakia." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 13
وعن محمد بن سيرين ، عن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : لَقَدْ رَأيْتُنِي وَإنِّي لأَخِرُّ فِيمَا بَيْنَ مِنْبَرِ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم إِلَى حُجْرَةِ عائِشَةَ رضي الله عنها مَغْشِيّاً عَلَيَّ ، فَيَجِيءُ الجَائِي ، فَيَضَعُ رِجْلَهُ عَلَى عُنُقِي ، وَيَرَى أنِّي مَجْنُونٌ وَمَا بِي مِنْ جُنُونٍ ، مَا بِي إِلاَّ الْجُوعُ . رواه البخاري.
Imepokewa kutoka kwake Muhammad bin Siiyriyn kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Nilijiona naanguka baina ya mimbari ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na chumba cha 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) na kupoteza fahamu, anapita mtu anaweka mguu wake shingoni mwangu, akidhani mimi ni mwenda wazimu. Ns mimi si mwenda wazimu isipokuwa njaa." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 14
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : تُوُفِّي رسول الله صلى الله عليه وسلم وَدِرْعُهُ مَرْهُونَةٌ عِنْدَ يَهُودِي في ثَلاثِينَ صَاعاً مِنْ شَعِير . متفق عَلَيْهِ .
Na imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba amesema: "Alifariki Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na dir'a (nguo ya chuma inayotumiwa katika vita) yake ameiweka rahani kwa Myahudi kwa Swaa' (takriban kilo mbili na nusu) thelathini za shayiri." [Al-Bukhaariy, Muslim na An-Nasaai]
Hadiyth – 15
وعن أنسٍ رضي الله عنه، قَالَ : رَهَنَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم دِرْعَهُ بِشَعِيرٍ ، وَمَشَيْتُ إِلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم بخُبْزِ شَعِيرٍ وَإهَالَة سَنِخَةٍ ، وَلَقَدْ سَمِعْتُهُ يَقُولُ : (( مَا أصْبَحَ لآلِ مُحَمّدٍ صَاعٌ وَلاَ أمْسَى )) وَإنَّهُمْ لَتِسْعَةُ أبيَات . رواه البخاري .
Imepokewa kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: "Aliweka rehani Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) dir'a yake kwa shayiri, nikamchukulia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mkate wa shayiri na samli, Nimemsikia anasema: "Haijapambazuka Familia ya Muhammad ikiwa na pishi ya chakula wala kuchwewe." Na hizo ni nyumba tisa." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 16
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : لَقَدْ رَأَيْتُ سَبْعِينَ مِنْ أَهْلِ الصُّفَّةِ ، مَا مِنْهُمْ رَجُلٌ عَلَيْهِ ردَاءٌ ، إمَّا إزَارٌ وَإمَّا كِسَاءٌ ، قَدْ رَبَطُوا في أعْنَاقِهِم مِنْهَا مَا يَبْلُغُ نِصْفَ السَّاقَيْن ، وَمِنْهَا مَا يَبْلُغُ الكَعْبَيْنِ فَيَجْمَعُهُ بِيَدِهِ كَرَاهِيَةَ أنْ تُرَى عَوْرَتُهُ . رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Nimeona Swahaaba sabiini miongoni mwa watu wa Swuffah, hakuna mtu miongoni mwao mwenye kikoi, shuka, wamezifunga katika shingo zao. Kuna zinazofika nusu ya miguu, nyingine kwenye fundo mbili, hivyo huzishika mkononi mwake kuchukia uchi wao kuonekana." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 17
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كَانَ فِرَاشُ رسول الله صلى الله عليه وسلم مِنْ أُدْمٍ حَشْوُهُ لِيفٌ . رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwake 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba amesema: "Godoro la Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) lilikuwa limetengenezwa kwa ngozi iliyotiwa magamba ya mtende." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 18
وعن ابن عمر رضي الله عنهما، قَالَ : كُنَّا جُلُوساً مَعَ رسول الله صلى الله عليه وسلم، إِذْ جَاءَ رَجُلٌ مِنَ الأنْصَارِ ، فَسَلَّمَ عَلَيْهِ ، ثُمَّ أدْبَرَ الأَنْصَاريُّ ، فَقَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( يَا أخَا الأنْصَارِ ، كَيْفَ أخِي سَعْدُ بْنُ عُبَادَةَ ؟ )) فَقَالَ : صَالِحٌ ، فَقَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ يَعُودُهُ مِنْكُمْ ؟ )) فَقَامَ وَقُمْنَا مَعَهُ ، وَنَحْنُ بضْعَةَ عَشَرَ ، مَا عَلَيْنَا نِعَالٌ ، وَلاَ خِفَافٌ ، وَلاَ قَلاَنِسُ ، وَلاَ قُمُصٌ ، نَمْشِي في تِلك السِّبَاخِ ، حَتَّى جِئْنَاهُ ، فَاسْتَأْخَرَ قَوْمُهُ مِنْ حَوْله حَتَّى دَنَا رسول الله صلى الله عليه وسلم وَأصْحَابُهُ الَّذِينَ مَعَهُ . رواه مسلم .
imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba amesema: "Tulikuwa tumekaa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuja mtu kutoka kwa Answaar na kumsalima Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Kisha yule Answaar akawa anaondoka, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akauliza: "Ee ndugu yangu wa Ki-Answaar, ndugu yangu Sa'ad bin 'Ubaadah yu hali gani?' Akasema: "Hali yake ni nzuri." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Nani atakayemzuru miongoni mwenu?" Alisimama na tukasimama pamoja naye. Na sisi tulikuwa kumi, na hakuna miongoni mwetu aliyekuwa na viatu au soksi za ngozi, wala kofia au shati. Tulikuwa tunatembea katika hali hiyo mpaka tukafika katika nyumba ya Sa'ad. Watu wake wa nyumbani (familia yake) walitupatia nafasi mpaka Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaaba zake waliokuwa pamoja naye wakapata nafasi ya kuja karibu yake." [Muslim]
Hadiyth – 19
وعن عِمْرَان بنِ الحُصَيْنِ رضي الله عنهما ، عن النبي صلى الله عليه وسلم ، أنّه قَالَ : (( خَيْرُكُمْ قَرْنِي ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ )) قَالَ عِمْرَانُ : فَمَا أدْري قَالَ النبي صلى الله عليه وسلم مَرَّتَيْنِ أَو ثَلاَثاً (( ثُمَّ يَكُونُ بَعْدَهُمْ قَوْمٌ يَشْهَدُونَ وَلاَ يُسْتَشْهَدُونَ ، وَيَخُونُونَ وَلاَ يُؤْتَمَنُونَ ، وَيَنْذِرُونَ وَلاَ يُوفُونَ ، وَيَظْهَرُ فِيهمُ السَّمَنُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwake 'Imraan bin Al-Huswaiyn (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mbora wenu ni (watu wa) karne yangu, kisha wanaowafuata, kisha wanaowafuata, kisha wanaowafuata, Akasema 'Imraan: "Sijui Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameisema mara mbili au mara tatu. Kisha watakuja baada yao watu watashuhudia wala hawatakiwi kushuhudia, wanakhini wala hawaaminiwi, utadhihiri miongoni mwao umeme (walionenepa)." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 20
وعن أَبي أُمَامَة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( يَا ابْنَ آدَمَ ، إنَّكَ أنْ تَبْذُلَ الفَضْلَ خَيرٌ لَكَ ، وَأنْ تُمسِكَهُ شَرٌ لَكَ ، ولاَ تُلاَمُ عَلَى كَفَافٍ ، وَابْدأ بِمَنْ تَعُولُ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Abuu Umamah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ee mwanadamu! Hakika lau utatoa fadhila (hela) za ziada itakuwa bora kwako, na kuzuilia (kutotumia) ni shari kwako. Hutalaumiwa kuwa na hela kwa kadiri ya mahitaji yako. Na anza kuitumia kwa wale wenye haki kwako." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 21
وعن عُبيْدِ الله بنِ محْصن الأَنصَارِيِّ الخطميِّ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ أصْبَحَ مِنْكُمْ آمِناً في سربِهِ ، مُعَافَىً في جَسَدِهِ ، عِنْدَهُ قُوتُ يَوْمِهِ ، فَكَأنَّمَا حِيزَتْ لَهُ الدُّنْيَا بِحَذَافِيرِهَا )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa 'Ubaydullaah bin Muhswan Al-Answaariy Al-Khutwamiy kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Yeyote atakaye pambazukiwa (atakaye inuka asubuhi) akiwa yu salama wa nafsi yake (au familia yake), akiwa na siha mzuri ya mwili wake, anacho chakula cha siku yake hiyo. Mwenye hayo ni kama ambaye amepatiwa dunia na vilivyomo ndani yake." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 22
وعن عبد الله بن عَمْرو بنِ العاص رضي الله عنهما : أن رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( قَدْ أفْلَحَ مَنْ أسْلَمَ ، وَكَانَ رِزْقُهُ كَفَافاً ، وَقَنَّعَهُ اللهُ بِمَا آتَاهُ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Amru bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika amefanikiwa aliyesilimu na ikiwa riziki yake ni yenye kumtosha na akakinaika kwa anachopewa na Allaah." [Muslim]
Hadiyth – 23
وعن أَبي محمدٍ فضَالَة بن عبيدٍ الأنصاريِّ رضي الله عنه: أنه سمع رسول الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( طُوبَى لِمَنْ هُدِيَ لِلإسْلاَمِ ، وَكَانَ عَيْشُهُ كَفَافاً وَقَنِعَ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Abuu Muhammad Fadhwalah bin 'Ubayd Al-Answaariy (Radhwiya Allaah 'anhu) kuwa amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Habari njema kwa anayeongoka na kusilimu na akapata rizki ya kumtosha mahitaji yake na akakinai kwa hilo." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 24
وعن ابن عباس رضي الله عنهما ، قَالَ : كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم يَبيتُ اللَّيَالِيَ الْمُتَتَابِعَةَ طَاوِياً ، وَأهْلُهُ لاَ يَجِدُونَ عَشَاءً ، وَكَانَ أكْثَرُ خُبْزِهِمْ خُبزَ الشَّعيرِ . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Na imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba amesema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akilala akiwa na shida ya njaa kwa masiku marefu yenye kufuatana na familia yake haina chochote cha kula usiku. Na mara nyingi mkate waliokuwa wakitumia ni mkate wa shayiri." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 25
وعن فُضَالَةَ بن عبيدٍ رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا صَلَّى بِالنَّاسِ ، يَخِرُّ رِجَالٌ مِنْ قَامَتِهِمْ في الصَّلاةِ مِنَ الخَصَاصَةِ – وَهُمْ أصْحَابُ الصُّفَّةِ – حَتَّى يَقُولَ الأعْرَابُ : هؤُلاء مَجَانِينٌ . فَإذَا صلَّى رسول الله صلى الله عليه وسلم انْصَرَفَ إلَيْهِمْ ، فَقَالَ : (( لَوْ تَعْلَمُونَ مَا لَكُمْ عِنْدَ اللهِ تَعَالَى ، لأَحْبَبْتُمْ أنْ تَزْدَادُوا فَاقَةً وَحَاجَةً )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwake Fadhwalah bin 'Ubayd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswalisha watu wakianguka chini baadhi ya watu wa Swuffah kwa sababu ya njaa kali mpaka wakawa wanasema Mabedui: "Hawa ni wenda wazimu." Alipokamilisha Swalah Rasuli wa Allaah alikuwa akiwaendea na kuwaambia: "Lau mngejua yaliyoko (katika thawabu) kwa Allaah Ta'aalaa, mngependa hali ya njaa kali ikaongezeka." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 26
وعن أَبي كريمة المقدام بن معد يكرِبَ رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( مَا مَلأَ آدَمِيٌّ وِعَاء شَرّاً مِنْ بَطْنٍ ، بِحَسْبِ ابنِ آدَمَ أُكُلاَتٌ يُقِمْنَ صُلْبَهُ ، فإنْ كانَ لا مَحالةَ فثُلُثٌ لِطَعَامِهِ ، وَثُلُثٌ لِشَرابِهِ ، وَثُلُثٌ لِنَفَسه )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Kariymah Al-Miqdaam bin Ma'di Yakrib (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hajajaza mwanadamu chombo kiovu zaidi kuliko tumbo lake. Inamtosha mwanadamu tonge la kuufanya mgongo usimame wima. Ikiwa hapana budi ila kula hicho chakula basi thuluthi ya tumbo iwe kwa chakula na thuluthi kwa kinywaji na thuluthi kwa nafsi yake (pumzi)." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan].
Hadiyth – 27
وعن أَبي أُمَامَة إياسِ بن ثعلبةَ الأَنْصَارِيِّ الحارثي رضي الله عنه ، قَالَ : ذَكَرَ أصْحَابُ رسول الله r يَوماً عِنْدَهُ الدُّنْيَا ، فَقَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( ألاَ تَسْمَعُونَ ؟ ألاَ تَسْمَعُونَ ؟ إنَّ البَذَاذَةَ مِنَ الإِيمَانِ ، إنَّ البَذَاذَةَ مِنَ الإِيمَانِ )) يَعْنِي : التَّقَحُّلَ . رواهُ أَبو داود
Imepokewa kutoka kwa Abu Umaamah Iyaas bin Tha'labah Al-Answaariy Al-Haarithiy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Siku moja Sahaabah wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walimtajia kuhusu dunia mbele yake. Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Je,hamjasikia? Je, hamjasikia? Hakika kuupa nyongo ulimwengu ni katika Imaani. Hakika kuupa nyongo ulimwengu ni katika Imaani (kwa kuacha fakhari katika mavazi na mengineo)." [Abu Daawuud]
Hadiyth – 28
وعن أَبي عبد الله جابر بن عبد الله رضي الله عنهما ، قَالَ : بَعَثَنَا رسول الله صلى الله عليه وسلم ، وَأمَّرَ عَلَيْنَا أَبَا عُبَيْدَةَ رضي الله عنه ، نَتَلَقَّى عِيراً لِقُرَيْشٍ ، وَزَوَّدَنَا جِرَاباً مِنْ تَمْرٍ لَمْ يَجِدْ لَنَا غَيْرَهُ ، فَكَانَ أَبو عُبيدَةَ يُعْطِينَا تَمْرَةً تَمْرَةً ، فَقيلَ : كَيْفَ كُنْتُمْ تَصْنَعُونَ بِهَا ؟ قَالَ : نَمَصُّهَا كَمَا يَمَصُّ الصَّبي ، ثُمَّ نَشْرَبُ عَلَيْهَا مِنَ الْمَاءِ ، فَتَكْفِينَا يَوْمَنَا إِلَى اللَّيْلِ ، وَكُنَّا نَضْرِبُ بِعِصيِّنَا الخَبَطَ ، ثُمَّ نَبُلُّهُ بِالماءِ فَنَأكُلُهُ . قَالَ : وَانْطَلَقْنَا عَلَى سَاحِلِ الْبَحْرِ ، فَرُفِعَ لَنَا عَلَى سَاحِلِ الْبَحْرِ كَهَيْئَةِ الكَثِيبِ الضَّخْمِ ، فَأَتَيْنَاهُ فَإذَا هِيَ دَابَّةٌ تُدْعَى الْعَنْبَرَ ، فَقَالَ أَبو عُبَيْدَةَ : مَيْتَةٌ ، ثُمَّ قَالَ : لا ، بَلْ نَحْنُ رُسُلُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ، وفي سبيل الله وَقَدِ اضْطُرِرْتُمْ فَكُلُوا ، فَأقَمْنَا عَلَيْهِ شَهْراً ، وَنَحْنُ ثَلاَثُمِئَةٍ حَتَّى سَمِنَّا ، وَلَقَدْ رَأيْتُنَا نَغْتَرِفُ مِن وَقْبِ عَيْنِهِ بِالقِلاَلِ الدُّهْنَ وَنَقْطَعُ مِنْهُ الفِدَرَ كالثَّوْرِ أَوْ كَقَدْرِ الثَّوْرِ ، وَلَقَدْ أَخَذَ مِنَّا أَبو عُبَيْدَةَ ثَلاثَةَ عَشَرَ رَجُلاً فَأقْعَدَهُمْ في وَقْبِ عَيْنِهِ وَأخَذَ ضِلْعاً مِنْ أضْلاَعِهِ فَأقَامَهَا ثُمَّ رَحَلَ أعْظَمَ بَعِيرٍ مَعَنَا فَمَرَّ مِنْ تَحْتهَا وَتَزَوَّدْنَا مِنْ لَحْمِهِ وَشَائِقَ ، فَلَمَّا قَدِمْنَا المَدِينَةَ أَتَيْنَا رسول الله صلى الله عليه وسلم فَذَكَرْنَا ذَلِكَ لَهُ ، فَقَالَ : (( هُوَ رِزْقٌ أخْرَجَهُ اللهُ لَكُمْ ، فَهَلْ مَعَكُمْ مِنْ لَحْمِهِ شَيْءٌ فَتُطْعِمُونَا ؟ )) فَأرْسَلْنَا إِلَى رسول الله صلى الله عليه وسلم مِنْهُ فَأكَلَهُ . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu 'Abdillaah Jaabir bin Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: "Alitutuma Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), amiri alikuwa Abu 'Ubaydah (Radhwiya Allaahu 'anhu), ili kuteka msafara wa Makureshi. Akatupa mfuko wa tende bila kitu kingine. Abu 'Ubaydah akawa akimpa kila mmoja watu tende moja moja tu. Akaulizwa: 'Mlikuwa mnaifanya nini?, Akasema: 'Tulikuwa tunainyonya kama anavyonyonya mtoto mchanga, kisha tukinywamaji. Ilikuwa ikitutosha mchana hadi usiku. Tulikuwa tukikata majani kwa fimbo, tukizitia kati maji na kuzila.' Akasema: 'Tulikwenda tukafika ufukweni ikanyanyuliwa kwetu katika huo ufuo wa bahari mfano wa kichuguu kikubwa. Tukakijia kumbe ni mnyama anayeitwa nyangumi.' Abu 'Ubaydah akasema: 'Huyu ni maiti.' Kisha akasema: 'Bali sisi ni wajumbe wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na tuko katika njia ya Allaah, na hii ni dharura kwa hivyo kuleni.' Tukamla mwezi mzima, nasi ni mia tatu hadi tukanenepa. Tulikuwa tukimtoa mafuta jichoni na kujaza viriba vya ngozi, tunakata nyama kama ng'ombe dume au mfano wake. Abu 'Ubaydah alikalisha watu kumi na tatu kwenye shimo la jicho lake. Akatoa mfupa wa mbavu yake na kuusimamisha na kupitisha ngamia mrefu zaidi chini yake. Wakati tunarudi tulichukua mapande makubwa na kuyachemsha kwa ajili ya chakula chetu. Tulipofika Madiynah tulikwenda kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na tukamtajia hayo, Akasema: "Hiyo ni riziki Allaah amekutoleeni, je mna chochote katika nyama yake mtupe" Tulimpa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) sehemu yake akaila." [Muslim]
Hadiyth – 29
وعن أسماء بنتِ يزيد رضي الله عنها ، قالت : كَانَ كُمُّ قَمِيصِ رسول الله صلى الله عليه وسلم إِلَى الرُّصْغِ . رواه أَبو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Na imepokewa kutoka kwa Asmaa' bint Yaziyd (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba amesema: "Mikono ya shati la Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ilikuwa ikifika mpaka kwenye kiungo cha viganja." [Abu Daawuud na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 30
وعن جابر رضي الله عنه ، قَالَ : إنَّا كُنَّا يَوْمَ الْخَنْدَقِ نَحْفِرُ ، فَعَرَضَتْ كُدْيَةٌ شَدِيدَةٌ ، فَجَاؤُوا إِلَى النبي صلى الله عليه وسلم ، فقالوا : هذِهِ كُدْيَةٌ عَرَضَتْ في الخَنْدَقِ . فَقَالَ : (( أنَا نَازِلٌ )) ثُمَّ قَامَ ، وَبَطْنُهُ مَعْصُوبٌ بِحَجَرٍ ، وَلَبِثْنَا ثَلاَثَة أيّامٍ لاَ نَذُوقُ ذَوَاقاً فَأخَذَ النبي صلى الله عليه وسلم المِعْوَلَ ، فَضَرَبَ فَعَادَ كَثيباً أهْيَلَ أَو أهْيَمَ ، فقلت : يَا رسول الله ، ائْذَنْ لي إِلَى البَيْتِ ، فقلتُ لامْرَأتِي : رَأيْتُ بالنَّبيِّ صلى الله عليه وسلم شَيئاً مَا في ذَلِكَ صَبْرٌ فَعِنْدَكِ شَيْءٌ ؟ فقالت : عِنْدي شَعِيرٌ وَعَنَاقٌ ، فَذَبَحْتُ العَنَاقَ وَطَحَنْتُ الشَّعِيرَ حَتَّى جَعَلْنَا اللَّحْمَ في البُرْمَةِ ، ثُمَّ جِئْتُ النبي صلى الله عليه وسلم ، وَالعَجِينُ قَدِ انْكَسَرَ ، وَالبُرْمَةُ بَيْنَ الأثَافِيِّ قَدْ كَادَتْ تَنْضِجُ ، فقلتُ : طُعَيْمٌ لي ، فَقُمْ أنْتَ يَا رسول اللهِ وَرَجُلٌ أَوْ رَجُلانِ ، قَالَ : (( كَمْ هُوَ )) ؟ فَذَكَرْتُ لَهُ ، فَقَالَ : (( كثيرٌ طَيِّبٌ قُل لَهَا لاَ تَنْزَع البُرْمَةَ ، وَلاَ الخبْزَ مِنَ التَّنُّورِحتى آتِي )) فَقَالَ : (( قُومُوا )) ، فقام المُهَاجِرُونَ وَالأنْصَارُ ، فَدَخَلْتُ عَلَيْهَا فقلتُ : وَيْحَكِ قَدْ جَاءَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم وَالمُهَاجِرُونَ وَالأنْصَارُ ومن مَعَهُمْ ! قالت : هَلْ سَألَكَ ؟ قُلْتُ : نَعَمْ ، قَالَ : (( ادْخُلُوا وَلاَ تَضَاغَطُوا )) فَجَعَلَ يَكْسرُ الخُبْزَ ، وَيَجْعَلُ عَلَيْهِ اللَّحْمَ ، وَيُخَمِّرُ البُرْمَةَ وَالتَّنُّور إِذَا أخَذَ مِنْهُ ، وَيُقَرِّبُ إِلَى أصْحَابِهِ ثُمَّ يَنْزعُ ، فَلَمْ يَزَلْ يِكْسِرُ وَيَغْرِفُ حَتَّى شَبِعُوا ، وَبَقِيَ مِنْهُ ، فَقَالَ : (( كُلِي هَذَا وَأهِدي ، فَإنَّ النَّاسَ أصَابَتْهُمْ مَجَاعَةٌ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
وفي رواية قَالَ جابر : لَمَّا حُفِرَ الخَنْدَقُ رَأيْتُ بالنبيِّ صلى الله عليه وسلم خَمَصاً ، فَانْكَفَأْتُ إِلَى امْرَأتِي ، فقلت : هَلْ عِنْدَكِ شَيْءٌ ؟ فَإنّي رَأيْتُ برسول الله صلى الله عليه وسلم خَمَصاً شَديداً ، فَأخْرَجَتْ إلَيَّ جِرَاباً فِيه صَاعٌ مِنْ شَعِيرٍ ، وَلَنَا بَهِيمَةٌ دَاجِنٌ فَذَبَحْتُهَا ، وَطَحَنتِ الشَّعِيرَ ، فَفَرَغَتْ إِلَى فَرَاغي ، وَقَطَعْتُهَا في بُرْمَتها ، ثُمَّ وَلَّيْتُ إِلَى رسول الله صلى الله عليه وسلم ، فقالت : لاَ تَفْضَحْنِي برسول الله صلى الله عليه وسلم وَمَنْ مَعَهُ ، فَجئتهُ فَسَارَرْتُهُ ، فَقُلْتُ : يَا رسول الله ، ذَبَحْنَا بهيمَة لَنَا ، وَطَحَنْتُ صَاعاً مِنْ شَعِيرٍ ، فَتَعَالَ أنْتَ وَنَفَرٌ مَعَكَ ، فَصَاحَ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : (( يَا أهلَ الخَنْدَقِ : إنَّ جَابِراً قَدْ صَنَعَ سُؤْراً فَحَيَّهَلا بِكُمْ )) فَقَالَ النبي صلى الله عليه وسلم : (( لاَ تُنْزِلُنَّ بُرْمَتَكُمْ وَلاَ تَخْبزنَّ عَجِينَكُمْ حَتَّى أجِيءَ )) فَجِئْتُ ، وَجَاءَ النبي صلى الله عليه وسلم يَقْدُمُ النَّاسَ ، حَتَّى جِئْتُ امْرَأتِي ، فقالَتْ : بِكَ وَبِكَ ! فقُلْتُ : قَدْ فَعَلْتُ الَّذِي قُلْتِ . فَأخْرَجَتْ عَجِيناً ، فَبسَقَ فِيهِ وَبَاركَ ، ثُمَّ عَمَدَ إِلَى بُرْمَتِنا فَبصَقَ وَبَارَكَ، ثُمَّ قَالَ: (( ادْعِي خَابزَةً فَلْتَخْبِزْ مَعَكِ ، وَاقْدَحِي مِنْ بُرْمَتِكُمْ ، وَلاَ تُنْزِلُوها )) وَهُم ألْفٌ ، فَأُقْسِمُ بِالله لأَكَلُوا حَتَّى تَرَكُوهُ وَانْحَرَفُوا ، وَإنَّ بُرْمَتَنَا لَتَغِطّ كَمَا هِيَ ، وَإنَّ عَجِينَنَا لَيُخْبَزُ كَمَا هُوَ .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Siku ya Khandaq tulikuwa tunachimba pakatokea jiwe gumu, wakaja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakasema: 'Jiwe limedhihiri katika Khandaq' akasema: "Mimi nitateremka." Kisha akasimama na tumbo lake limefungwa jiwe. Tulikaa siku tatu bila kuonja chakula. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akachukua mtaimbo akalipiga likawa kichuguu laini, au mchanga. Nikasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Niruhusu niende nyumbani." Nilimwambia mke wangu: "Nimemuona Nabiy (Swalla Allaau 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika hali ambayo siwezi kuvumilia. Una chochote?" Akasema: "Ipo shayiri na mwana mbuzi." Nilimchinja mbuzi na kutwanga shayiri hadi tukaiweka nyama katika chungu. Baada ya hapo nilikuja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mchunzi ukiwa unatokota na unga wa shayiri umekandwa na tayari kutiwa katika tanuri. Nilimwambia: "Nimeandaa chakula. Njoo wewe na mtu au watu wawili." Akasema: "Huo unatosha kiasi gani?" Nikamtajia. Akasema: "Wengi ni bora, mwambie mkeo asiepue chungu, motoni wala mikate katika tanuri hadi nije." Kisha akawambia Swahaba zake: "Twendeni." Wakasimama Muhaajiruun na Answaar. Nikaingia kwa mke wangu nikamwambia: "Umebarikiwa! Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), Muhaajiruun na Answaar wote wanakuja." Akasema: "Je, alikuuliza?" Nikasema: "Ndio." Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alifika hapo na kuwaambia Swahaba zake: "Ingieni wala msisongamane." Akawa anakata mikate, na juu yake anaweka nyama. Anatoa mchuzi kwenye chungu na mikate kutoka kwa tanuri, kisha akaifunika na kuwapa Swahaba zake. Kisha anarudia, hakuacha hilo mpaka wakashiba na kikabaki. Akasema: "Kula hiki chakula na ukigawe, kwani watu wamepata njaa." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Katika riwaayah: Jaabir amesema: "Khandaq lilipofukuliwa, nilimuona Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ana njaa. Hivyo nilikwenda kwa mke wangu na kumuuliza: "Una kitu chochote kwani nimemuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ana njaa kali?" Alitoa mkoba wenye pishi ya shayiri, nasi tuna mwana mbuzi. Nikamchinja, mke wangu akakanda shayiri na akaoka mkate. Nikaikata nyama na kuitia chunguni. Kisha nilikwenda kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), Akaniambia mke wangu: "Usinifedheheshe kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na walio pamoja naye." Nilikuja kwake na kumnong'oneza nikasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Tumechinja mnyama wetu, na tuna pishi ya shayiri, njoo wewe kikundi pamoja nawe." Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), akaita: "Enyi watu wa Khandaq! Hakika Jaabir ameandaa karamu kwa hivyo nyote njooni." Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Msiepue chungu wala msiitoe mikate yenu mpaka nije." Nilirudi nyumbani Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaja anaongoza watu. Nilimjia mke wangu. Akasema: "Kwako wewe." Nikasema: "Nimefanya ulivyoniamuru." Mke wangu alileta mkate, na Nabiy akautia mate yake na kuubariki, kisha akaenda kwenye chungu akatema ndani yake na kukibariki. Kisha akasema: "Muite muokaji aoke pamoja nawe, na toeni mchuzi kwenye chungu, wala msikiinue chungu (motoni)." Wao ni elfu. Naapa kwa Allaah! Walikula mpaka wakakiacha wakaondoka. Chungu chetu kimejaa kama kilivyokuwa, na ngano yetu iko kama mwanzo.
Hadiyth – 31
وعن أنسٍ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ أَبو طَلْحَةَ لأُمِّ سُلَيمٍ : قَدْ سَمِعْتُ صَوْتَ رسول الله صلى الله عليه وسلم ضَعيفاً أعْرِفُ فيه الجُوعَ ، فَهَلْ عِنْدَكِ مِنْ شَيْءٍ ؟ فَقَالَتْ : نَعَمْ ، فَأخْرَجَتْ أقْرَاصاً مِنْ شَعِيرٍ ، ثُمَّ أخَذَتْ خِمَاراً لَهَا ، فَلَفَّتِ الخُبْزَ بِبَعْضِهِ ، ثُمَّ دَسَّتْهُ تَحْتَ ثَوْبِي وَرَدَّتْنِي بِبَعْضِهِ ، ثُمَّ أرْسَلَتْني إِلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم ، فَذَهَبتُ بِهِ ، فَوَجَدْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، جَالِساً في المَسْجِدِ ، وَمَعَهُ النَّاسُ، فَقُمْتُ عَلَيْهمْ، فَقَالَ لي رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( أرْسَلَكَ أَبو طَلْحَةَ ؟ )) فقلت : نَعَمْ ، فَقَالَ : (( ألِطَعَامٍ ؟ )) فقلت : نَعَمْ ، فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( قُومُوا )) فَانْطَلَقُوا وَانْطَلَقْتُ بَيْنَ أيْدِيهِمْ حَتَّى جِئْتُ أَبَا طَلْحَةَ فَأخْبَرْتُهُ ، فَقَالَ أَبو طَلْحَةَ : يَا أُمَّ سُلَيْمٍ ، قَدْ جَاءَ رسول الله صلى الله عليه وسلم بالنَّاسِ وَلَيْسَ عِنْدَنَا مَا نُطْعِمُهُمْ ؟ فَقَالَتْ : الله وَرَسُولُهُ أعْلَمُ . فَانْطَلَقَ أَبو طَلْحَةَ حَتَّى لَقِيَ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، فَأقْبَلَ رسول الله صلى الله عليه وسلم مَعَهُ حَتَّى دَخَلاَ ، فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( هَلُمِّي مَا عِنْدَكِ يَا أُمَّ سُلَيْمٍ )) فَأتَتْ بِذلِكَ الخُبْزِ ، فَأمَرَ بِهِ رسول الله صلى الله عليه وسلم فَفُتَّ ، وَعَصَرَتْ عَلَيْهِ أمُّ سُلَيْمٍ عُكّةً فَآدَمَتْهُ، ثُمَّ قَالَ فِيهِ رسول الله صلى الله عليه وسلم مَا شَاءَ اللهُ أنْ يَقُولَ ، ثُمَّ قَالَ : (( ائْذَنْ لِعَشْرَةٍ )) فأذنَ لَهُمْ فَأكَلُوا حتى شَبِعُوا ثُمَّ خَرَجُوا ، ثُمَّ قَالَ : (( ائْذَنْ لِعَشْرَةٍ )) فأذِنَ لهم حَتَّى أكَلَ الْقَوْمُ كُلُّهُمْ وَشَبِعُوا وَالقَوْمُ سَبْعُونَ رَجُلاً أَو ثَمَانُونَ . متفقٌ عَلَيْهِ .
وفي رواية : فَمَا زَالَ يَدْخُلُ عَشرَة ، وَيخرجُ عشرةٌ حَتَّى لَمْ يَبْقَ مِنْهُمْ أحَدٌ إِلاَّ دَخَلَ ، فَأكَلَ حَتَّى شَبعَ ، ثُمَّ هَيَّأهَا فَإذَا هِيَ مِثْلُهَا حِيْنَ أكَلُوا مِنْهَا .
وفي رواية : فَأَكَلُوا عَشرَةً عَشرةً ، حَتَّى فَعَلَ ذَلِكَ بِثَمَانِينَ رَجُلاً ، ثُمَّ أكَلَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم بَعْدَ ذَلِكَ وَأهْلُ البَيْتِ ، وَتَرَكُوا سُؤْراً .
وفي رواية : ثُمَّ أفْضَلُوا مَا بَلَغُوا جيرانَهُمْ .
وفي رواية عن أنس ، قَالَ : جِئتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يوماً ، فَوَجَدْتُهُ جَالِساً مَعَ أصْحَابِه ، وَقَدْ عَصَبَ بَطْنَهُ ، بِعِصَابَةٍ ، فقلتُ لِبَعْضِ أصْحَابِهِ : لِمَ عَصَبَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم بَطْنَهُ ؟ فقالوا : مِنَ الجوعِ ، فَذَهَبْتُ إِلَى أَبي طَلْحَةَ ، وَهُوَ زَوْجُ أُمِّ سُلَيْمٍ بِنْت مِلْحَانَ ، فقلتُ : يَا أبتَاهُ ، قَدْ رَأيْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم عَصَبَ بَطْنَهُ بِعِصَابَةٍ ، فَسَألْتُ بَعْضَ أصْحَابِهِ ، فقالوا : من الجُوعِ . فَدَخَلَ أَبو طَلْحَةَ عَلَى أُمِّي ، فَقَالَ : هَلْ مِنْ شَيءٍ ؟ قالت : نَعَمْ ، عِنْدِي كِسَرٌ مِنْ خُبْزٍ وَتَمَرَاتٌ ، فَإنْ جَاءنَا رسول الله صلى الله عليه وسلم وَحْدَهُ أشْبَعْنَاهُ ، وَإنْ جَاءَ آخَرُ مَعَهُ قَلَّ عَنْهُمْ ... وَذَكَرَ تَمَامَ الْحَدِيثِ .
Kutoka kwa Anas amesema: Abuu Twalhah alimwambia Ummu Sulaym (Radhwiya Allaahu 'anhaa): "Nimesikia sauti ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni dhaifu, najua ana njaa. Una chochote?" Akasema: "Ndio." Akatoa mikate ya shayiri, kisha akachukua khimaar yake na kufinika mkate kwa sehemu yake, na kuificha ndani ya nguo yangu, kisha akanituma kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nikaenda nao, nikamkuta Rasuli wa Allaah amekaa Msikitini pamoja na watu. Nilisimama mbele yao, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Umetumwa na Abuu Twalhah?" Nikasema: "Ndio." Akasema: "Je, ni chakula?" Nikasema: "Ndio." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Inukeni" Wakaondoka, nikatembea mbele yao, hadi nikamfikia Abuu Twalhah (Radhwiya Allaahu 'anhu) nilimwarifu yaliyojiri Msikitini. Abuu Twalhah akasema: "Ee Umm Sulaym! Hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekuja na watu nasi hatuna cha kuwalisha." Akasema: "Allaah na Rasuli Wake wanajua zaidi." Abuu Twalhah alitoka mpaka akakutana na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), naye alifuatana na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hadi wakaingia nyumbani. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Ee Umm Sulaym! Lete ulichonacho." Akaleta mikate, Rasuli wa Allaah akaamuru ikakatwa katwa. Umm Sulaym akaitia siagi kwenye chupa kutayarisha mchuzi. Kisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema alichomjaalia Allaah kusema, kisha akasema: "Waruhusuni watu kumi." Wakaruhusiwa wakala mpaka wakashiba, kisha wakatoka. Kisha akasema: "Waruhusuni watu kumi." Wakaruhusiwa wakala mpaka wakashiba, kisha wakatoka. Kisha akasema: "Waruhusuni watu kumi." Wakaruhusiwa wakala mpaka wakashiba, kisha wakatoka. Na idadi ya watu ilikuwa ni sabiini au themanini. [Al-Bukhaariy na Muslim].
Katika riwaayah: "Hawakuacha kuingia kumi, na kutoka kumi mpaka hakubakia wakamalizika wote yoyote isipokuwa aliingia, akala hadi akashiba. Kisha wakakikusanya kikawa mfano wa kilicholiwa walipoanza kula."
Katika riwaayah: "Wakala watu kumi kumi mpaka wakafika themanini. Kisha akala Nabiy (swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), baadae ahlul bayt, wakaacha mabaki.
Katika riwaayah: "Kisha kilichobakia kiligawiwa majirani."
Katika riwaayah ya Anas amesema: "Nilimjia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) siku moja, Nikamkuta amekaa na Swahaba zake, Amefunga tumbo lake kwa mkanda; Nikauliza baadhi ya Swahaba zake: "Kwa nini Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amefunga tumbo lake?" Wakasema: "Kutokana na njaa." Nikaenda kwa Abuu Twalhah, mume wa Umm Sulaym bint Milhaan nikamwambia: "Ee babangu! Nimemwona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amefunga tumbo lake kwa mkanda, Nikauliza baadhi ya Swahaba zake wakasema: "NI kutokana na njaa." Abuu Twalhah akaingia kwa mamangu, akasema: kumwambia: "Kuna chochote?" Akasema: "Ndio, nina vipande vya mkate na tende. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akitujia peke yake tutamshibisha, Akija mwingine pamoja nae kitakuwa kidogo." Akataja Hadiyth kamili.