057-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukinai, Utohara na Kukusuru Katika Maisha na Kutoa na Uovu Wa Kuomba Bila Ya Dharura

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب القناعة والعَفاف والاقتصاد في المعيشة والإنفاق وذم السؤال من غير ضرورة

57-Mlango Wa Kukinai, Utohara na Kukusuru Katika Maisha na Kutoa na Uovu Wa Kuomba Bila Ya Dharura

 

Alhidaaya.com

 

 

 

قَالَ الله تَعَالَى:

وَمَا مِن دَابَّةٍ فِي الْأَرْضِ إِلَّا عَلَى اللَّـهِ رِزْقُهَا ﴿٦﴾

Na hakuna kiumbe chochote kitembeacho katika ardhi isipokuwa riziki yake iko kwa Allaah;  [Huwd: 6]

 

لِلْفُقَرَاءِ الَّذِينَ أُحْصِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ لَا يَسْتَطِيعُونَ ضَرْبًا فِي الْأَرْضِ يَحْسَبُهُمُ الْجَاهِلُ أَغْنِيَاءَ مِنَ التَّعَفُّفِ تَعْرِفُهُم بِسِيمَاهُمْ لَا يَسْأَلُونَ النَّاسَ إِلْحَافًا ۗ  ﴿٢٧٣﴾

(Swadaqah ni) Kwa ajili ya mafakiri waliozuilika katika njia ya Allaah hawawezi kwenda huku na kule katika ardhi (kutafuta rizki); asiyewajua huwadhania kuwa ni matajiri kutokana na staha ya kujizua kwao, unawatambua kwa alama zao, hawaombi watu kwa ung’ang’anizi. [Al-Baqarah: 273]

 

وَالَّذِينَ إِذَا أَنفَقُوا لَمْ يُسْرِفُوا وَلَمْ يَقْتُرُوا وَكَانَ بَيْنَ ذَٰلِكَ قَوَامًا ﴿٦٧﴾

Na wale ambao wanapotoa huwa hawafanyi israfu na wala hawafanyi uchoyo na wanakuwa wastani baina ya hayo. [Al-Furqaan: 67]

 

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ ﴿٥٦﴾ مَا أُرِيدُ مِنْهُم مِّن رِّزْقٍ وَمَا أُرِيدُ أَن يُطْعِمُونِ ﴿٥٧﴾

Na Sikuumba majini na wana Aadam isipokuwa waniabudu. Sitaki kutoka kwao riziki yoyote, na wala Sitaki wanilishe. [Adh-Dhaariyaat: 56-57]

 

 

 

Hadiyth – 1

عن أَبي هريرة رضي الله عنه  ، عن النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  لَيْسَ الغِنَى عَن كَثرَةِ العَرَض ، وَلكِنَّ الغِنَى غِنَى النَّفْسِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) toka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Utajiri si wingi wa mali, lakini utajiri ni kutosheka katika nafsi." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( قَدْ أفْلَحَ مَنْ أسْلَمَ ، وَرُزِقَ كَفَافاً ، وقَنَّعَهُ الله بِمَا آتَاهُ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Amruw bin Al-'Aaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika amefanikiwa aliyesilimu na ikawa riziki yake ni yenye kumtosha na akakinaika kwa anachopewa na Allaah." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 3

وعن حكيم بن حزام رضي الله عنه  ، قَالَ : سألتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم فَأعْطَانِي ، ثُمَّ سَألْتُهُ فَأَعْطَانِي ، ثُمَّ سَألْتُهُ فَأعْطَانِي ، ثُمَّ قَالَ : ((  يَا حَكِيم ، إنَّ هَذَا المَالَ خَضِرٌ حُلْوٌ ، فَمَنْ أخَذَهُ بِسَخَاوَةِ نَفسٍ بُورِكَ لَهُ فِيهِ ، وَمَنْ أخَذَهُ بإشرافِ نَفسٍ لَمْ يُبَارَكْ لَهُ فِيهِ ، وَكَانَ كَالَّذِي يَأكُلُ وَلاَ يَشْبَعُ ، وَاليَدُ الْعُلْيَا خَيْرٌ مِنَ اليَدِ السُّفْلَى )) قَالَ حكيم : فقلتُ : يَا رسول الله ، وَالَّذِي بَعَثَكَ بِالحَقِّ لاَ أرْزَأُ أحَداً بَعْدَكَ شَيْئاً حَتَّى أُفَارِقَ الدُّنْيَا ، فَكَانَ أَبُو بَكْرٍ رضي الله عنه يَدْعُو حَكيماً لِيُعْطِيَه العَطَاء ، فَيَأبَى أنْ يَقْبَلَ مِنْهُ شَيْئاً ، ثُمَّ إنَّ عُمَرَ رضي الله عنه  دَعَاهُ لِيُعْطِيَه فَأَبَى أنْ يَقْبَلَهُ . فقالَ : يَا مَعْشَرَ المُسْلِمِينَ ، أُشْهِدُكُمْ عَلَى حَكيمٍ أنّي أعْرِضُ عَلَيْهِ حَقَّهُ الَّذِي قَسَمَهُ اللهُ لَهُ في هَذَا الفَيء فَيَأبَى أنْ يَأخُذَهُ . فَلَمْ يَرْزَأْ حَكيمٌ أحَداً مِنَ النَّاسِ بَعْدَ النبي صلى الله عليه وسلم حَتَّى تُوُفِّي . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Hakiym bin Hizaam (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Nilimuomba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) naye akanipatia, kisha nikamwuomba mara nyengine, naye akanipa. Kisha nikamuomba tena naye akanipatia. Hapo akaniambia: "Ee Hakiym! Hakika hii mali ni kijani na ni tamu. Mwenye kuichukua kwa nafsi ya upaji atabarikiwa, na mwenye kuichukua kutaka nayo utukufu hatabarikiwa. Naye anakuwa mfano wa mlaji asiyeshiba. Na mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini." Akasema Hakiym (Radhwiya Allaahu 'anhu) nikasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Naapa kwa aliyekutuma kwa haki, sitamuomba yeyote mpaka nitakapoaga dunia." Abuu Bakr (Radhwiya Allaahu 'anhu) alikuwa akimuiita Hakiym ampe, anakataa kupokea. Kisha "Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) alimuiita ampe akakataa kupokea. 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) alisema: "Enyi kongamano la Waislamu! Shuhudieni kuwa juu ya Hakiym kuwa nilimpa haki yake aliyomgawia Allaah katika ngawira amekataa kuichukua." Hivyo Hakiym hakumuomba yoyote baada ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mpaka amekufa." [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na An-Nasaai]

 

 

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي بردة ، عن أَبي موسى الأشعري رضي الله عنه ، قَالَ : خَرَجْنَا مَعَ رسول الله صلى الله عليه وسلم في غَزاةٍ وَنَحْنُ سِتَّةُ نَفَرٍ بَيْنَنَا بَعِيرٌ نَعْتَقِبُهُ ، فَنقِبَت أقدَامُنَا وَنَقِبَت قَدَمِي ، وسَقَطت أظْفَاري ، فَكُنَّا نَلُفُّ عَلَى أرْجُلِنا الخِرَقَ ، فَسُمِّيَت غَزْوَةَ ذَاتِ الرِّقَاعِ لِمَا كُنَّا نَعْصِبُ عَلَى أرْجُلِنَا مِنَ الخِرَقِ ، قَالَ أَبُو بُردَة : فَحَدَّثَ أَبُو مُوسَى بِهَذَا الحَدِيثِ ، ثُمَّ كَرِه ذَلِكَ ، وقال : مَا كُنْتُ أصْنَعُ بِأنْ أذْكُرَهُ ! قَالَ : كأنَّهُ كَرِهَ أنْ يَكُونَ شَيْئاً مِنْ عَمَلِهِ أفْشَاهُ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Abuu Burdah kwa Abuu Muwsaa Al-'Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa: Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuelekea vitani, tulikuwa watu sita tukipanda ngamia mmoja kwa zamu. Nyayo zetu zilipasuka, miguu yangu ikapasuka kucha zangu za miguu zikatoka. Ili kufunika majeraha, tulifunga miguu yetu matambara, kwa hiyo vikaitwa Dhaatur Riqaai, kwa sababu ya kufunga matambara miguuni mwetu. Akasema Abuu Burdah: "Abuu Muwsaa alihadithia kisa hiki kisha akachukia hilo, akasema: Sikufanya hilo ilinikumbukwe." Akasema: "Kana kwamba amechukia kufichua matendo yake (ya Jihaad) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 5

وعن عمرو بن تَغْلِبَ – بفتح التاء المثناة فوق وإسكان الغين المعجمة وكسر اللام - رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم أُتِي بِمالٍ أَوْ سَبْيٍ فَقَسَّمَهُ ، فَأعْطَى رِجَالاً ، وَتَرَكَ رِجَالاً ، فَبَلغَهُ أنَّ الَّذِينَ تَرَكَ عَتَبُوا ، فَحَمِدَ اللهَ ، ثُمَّ أثْنَى عَلَيْهِ ، ثُمَّ قَالَ :     ((  أمَّا بعْدُ ، فَواللهِ إنِّي لأُعْطِي الرَّجُلَ وَأدَعُ الرَّجُلَ ، وَالَّذِي أدَعُ أحَبُّ إلَيَّ مِنَ الَّذِي أُعْطِي ، وَلَكِنِّي إنَّمَا أُعْطِي أقْوَاماً لِمَا أرَى في قُلُوبِهِمْ مِنَ الجَزَعِ وَالهَلَعِ ، وَأكِلُ أقْوَاماً إِلَى مَا جَعَلَ اللهُ في قُلُوبِهم مِنَ الغِنَى وَالخَيْرِ ، مِنْهُمْ عَمْرُو بنُ    تَغْلِبَ )) قَالَ عَمْرُو بنُ تَغْلِبَ : فَوَاللهِ مَا أُحِبُّ أنَّ لِي بِكَلِمَةِ رسول الله صلى الله عليه وسلم حُمْرَ النَّعَم . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa 'Amruw bin Taghlib (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba aliletewa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mali au ngawira akaigawa. Aliwapa baadhi ya watu na kuwaacha wengine. Ikamfikia kwamba ambao amewaacha wamelalamika, Basi Akamhimidi Allaah, Akamsifu, kisha akasema: "Amma Ba'ad, Wa-Allaahi! Mimi nampa mtu na namuacha mwingine, ninayemnyima nampenda zaidi kuliko ninayempa. Ninawapa watu niwaonao mioyoni mwao babaiko na papara, na wengine nawaegemeza kwenye majaliwa ya Allaah mioyoni mwao, ukwasi na kheri, miongoni mwao ni 'Amruw bin Taghlib." Akasema 'Amruw bin Taghlib (Radhwiya Allaahu 'anhu) : "Naapa kwa Allaah! Sipendi mbadala wa maneno ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hata kwa ngamia wekundu, (ambao walikuwa wakithaminiwa sana na Waarabu)." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 6

وعن حكيم بن حزام رضي الله عنه : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  اليَدُ العُلْيَا خَيْرٌ مِنَ اليَدِ السُّفْلَى ، وَابْدَأْ بِمَنْ تَعُولُ ، وَخَيْرُ الصَّدَقَةِ مَا كَانَ عَنْ ظَهْرِ غِنىً ، وَمَنْ يَسْتَعْفِفْ يُعِفُّهُ الله ، وَمَنْ يَسْتَغْنِ يُغنهِ الله )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwake Hakiym bin Hizaam: Kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini, anza kwa wanaokutegemea. Na bora ya swadaqah ni ilio nje ya kujitosha, Mwenye kujichunga Allaah atamwezesha. Na Mwenye kujitosha Allaah atamtosha." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 7

وعن أَبي عبد الرحمان معاوية بن أبي سفيان رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لاَ تُلْحِفُوا في الْمَسْأَلَةِ ، فَوَاللهِ لاَ يَسْأَلُنِي أَحَدٌ مِنْكُمْ شَيْئاً ، فَتُخْرِجَ لَهُ مَسْأَلَتُهُ مِنِّي شَيْئاً وَأنَا لَهُ كَارهٌ ، فَيُبَارَكَ لَهُ فِيمَا أعْطَيْتُهُ )) رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwa Abuu Sufyaan |Swakhr bin Harb (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Msing'ang'anie katika kuuliza. Wa-Allaahi! Haniombi miongoni mwenu chochote, na nikampatia hicho alichoomba nami nachukia habarikiwi katika nilichompa." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 8

وعن أَبي عبدِ الرحمان عوف بن مالِك الأَشْجَعِيِّ رضي الله عنه ، قَالَ : كُنَّا عِنْدَ رسول الله صلى الله عليه وسلم تِسْعَةً أَوْ ثَمَانِيَةً أَوْ سَبْعَةً ، فَقَالَ : ((  ألاَ تُبَايِعُونَ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم )) وَكُنَّا حَديثِي عَهْدٍ ببَيْعَةٍ ، فَقُلْنَا : قَدْ بَايَعْنَاكَ يَا رسولَ اللهِ ، ثمَّ قالَ : (( ألا تُبَايِعُونَ رسولَ اللهِ )) فَبَسَطْنا أيْدينا ، وقلنا : قدْ بايعناكَ فَعَلامَ نُبَايِعُكَ ؟ قَالَ : ((  عَلَى أنْ تَعْبُدُوا اللهَ وَلاَ تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئاً ، وَالصَّلَوَاتِ الخَمْسِ وَتُطِيعُوا الله )) وأَسَرَّ كَلِمَةً خَفِيفَةً ((  وَلاَ تَسْألُوا النَّاسَ شَيْئاً )) فَلَقَدْ رَأيْتُ بَعْضَ أُولئِكَ النَّفَرِ يَسْقُطُ سَوطُ أحَدِهِمْ فَمَا يَسأَلُ أحَداً يُنَاوِلُهُ إيّاهُ . رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwake Abuu 'Abdir-Rahmaan 'Awf bin Maalik Al-Ashja'iy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema kuwa: Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah watu wa tisa au nane au saba, akasema: "Kwa nini hamum-bai' Rasuli wa Allaah? Tukanyoosha mikono yetu tukasema: Tumekubali (Bay'ah) ee Rasuli wa Allaah? Je, tukuba'i juu ya nini?" Akasema: "Juu ya kumuabudu Allaah wa msimshirikishe na chochote, na Swalaah tano, hafifu: (taratibu): "Wala msiwaombe watu chochote." Hakika nimeona baadhi ya watu hao hata akaiangukwa na kikoto (kiboko), haombi yoyote kumuokotea." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 9

وعن ابن عمر رضي الله عنهما: أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ: (( لاَ تَزَالُ الْمَسْأَلةُ بأَحَدِكُمْ حَتَّى يَلْقَى الله تَعَالَى وَلَيْسَ في وَجْهِهِ مُزْعَةُ لَحْمٍ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwake Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Itabaki kuomba kwa mmoja wenu hadi atakapokutana na Allaah Ta'aalaa na hana katika uso wake kipande cha nyama." [Al-Bukhaariy, Muslim na An-Nasaai]

 

 

Hadiyth – 10

وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ وَهُوَ عَلَى المِنْبَرِ ، وَذَكَرَ الصَّدَقَةَ وَالتَّعَفُّفَ عَنِ الْمَسْأَلَةِ : ((  اليَدُ العُلْيَا خَيْرٌ مِنَ اليَدِ السُّفْلَى ، وَاليَدُ العُلْيَا هِيَ المُنْفِقَةُ ، وَالسُّفْلَى هِيَ السَّائِلَةُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alizungumza kuhusu swadaqah na kutoomba akiwa juu ya minbar na akasema: "Mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini. Mkono wa juu ni wenye kutoa na wa chini ni wenye kuomba." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 11

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  مَنْ سَألَ النَّاسَ تَكَثُّراً فإنَّمَا يَسْألُ جَمْراً ؛ فَلْيَسْتَقِلَّ أَوْ لِيَسْتَكْثِرْ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuomba watu ili mali yake iongezeke, hakika yeye anaomba kaa la moto. Hivyo ni juu yake ima kupunguza au kuongeza." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 12

وعن سَمُرَةَ بنِ جُنْدبٍ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  إنَّ المَسْأَلَةَ كَدٌّ يَكُدُّ بِهَا الرَّجُلُ وَجْهَهُ ، إِلاَّ أنْ يَسْأَلَ الرَّجُلُ سُلْطاناً أَوْ في أمْرٍ لاَ بُدَّ مِنْهُ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwake Samurah bin Jundub (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika kuomba inamjeruhi mtu uso wake isipokuwa anapomuomba mtu sultani au kwa jambo ambalo hapana budi (ila kuomba)." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 13

وعن ابن مسعود رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  مَنْ أصَابَتْهُ فَاقَةٌ فَأنْزَلَهَا بالنَّاسِ لَمْ تُسَدَّ فَاقَتُهُ ، وَمَنْ أنْزَلَهَا باللهِ ، فَيُوشِكُ اللهُ لَهُ بِرِزْقٍ عَاجِلٍ أَوْ آجِلٍ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Yeyote mwenye kupatwa na shida (kama njaa na ufakiri), kisha akaipeleka kwa watu ili wamsaidie, shida yake hiyo haitaondoka (kutaka uasidizi) kwa Allaah basi ataondoshewa na Allaah kwa haraka na kupatiwa riziki kwa wakati wa karibu au baadae." [Abuu Daawud na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

 

Hadiyth – 14

وعن ثوبان رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  مَنْ تَكَفَّلَ لِي أنْ لاَ يَسْأَلَ النَّاسَ شَيْئاً ، وَأتَكَفَّلُ لَهُ بِالْجَنَّةِ ؟ )) فقلتُ : أنَا ، فَكَانَ لاَ يَسْأَلُ أحَداً شَيْئاً . رواه أَبُو داود بإسناد صحيح .

Imepokewa kutoka kwake Thawbaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Yeyote atakaye nidhaminia kwamba hatamuuliza (kuomba) mtu yeyote kwa kitu chochote basi kwake nitamdhaminia Pepo. Nikasema: 'MImi.' Baada ya hapo hakumuomba (yaani Thawbaan) mtu yoyote kitu chochote." [Abuu Daawud kwa Isnaad iliyo Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 15

وعن أَبي بِشْرٍ قَبيصَةَ بنِ المُخَارِقِ رضي الله عنه ، قَالَ : تَحَمَّلْتُ حَمَالَةً فَأتَيْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم أسْأَلُهُ فِيهَا ، فَقَالَ : ((  أقِمْ حَتَّى تَأتِيَنَا الصَّدَقَةُ فَنَأمُرَ لَكَ بِهَا )) ثُمَّ قَالَ : ((  يَا قَبيصةُ ، إنَّ المَسْأَلَةَ لاَ تَحِلُّ إِلاَّ لأَحَدِ ثلاثَةٍ : رَجُلٌ تحمَّلَ حَمَالَةً ، فَحَلَّتْ لَهُ المَسْأَلَةُ حَتَّى يُصِيبَها ، ثُمَّ يُمْسِكُ ، وَرَجُلٌ أصَابَتْهُ جَائِحَةٌ اجْتَاحَتْ   مَالَهُ ، فَحَلَّتْ لَهُ الْمَسْأَلَةُ حَتَّى يُصِيبَ قواماً مِنْ عَيش - أَوْ قَالَ : سِدَاداً مِنْ عَيْشٍ - وَرَجُلٌ أصَابَتْهُ فَاقَةٌ ، حَتَّى يَقُولَ ثَلاَثَةٌ مِنْ ذَوِي الحِجَى مِنْ قَوْمِه : لَقَدْ أصَابَتْ فُلاناً فَاقَةٌ . فَحلَّتْ لَهُ الْمَسْأَلَةُ حَتَّى يصيب قواماً من عيش ، أَوْ قَالَ : سداداً من عيشِ ، فما سِوَاهُنَّ مِنَ المسألَةِ يَا قَبِيصَةُ سُحْتٌ ، يَأكُلُهَا صَاحِبُهَا سُحْتاً )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Bishr Qabiyswah bin Al-Mukhaariq amesema: Nilibeba dhamana ya fidia ya mauaji. Nilimwendea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kumuulizia hilo. Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ngojea mpaka itujie swadaqah tutakuamrishia chochote." Kisha akasema: "Ee Qabiyswah! Hakika kuomba si halali ila kwa moja ya matatu: Mtu anayedaiwa, ni halali kwake kuomba hadi alipate, kisha ajizuie; Na mtu amepata maafa mali yake ikaharibika ni halali kwake kuomba mpaka apate msimamo katika maisha- au alisema:' "Kukidhi maisha." Na mtu amepata ufukara, mpaka waseme watu watatu wenye akili katika watu wake: 'fulani amepata njaa.' Ni halali kwake kuomba mpaka apate msimamo wa maisha au alisema, "Kukidhi maisha." Wasiokuwa hawa kuomba ee Qabiyswah ni haramu, anaekula anakula haramu." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 16

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  لَيْسَ المسكينُ الَّذِي يَطُوفُ عَلَى النَّاسِ تَرُدُّهُ اللُّقْمَةُ وَاللُّقْمَتَانِ ، وَالتَّمْرَةُ وَالتَّمْرَتَانِ ، وَلكِنَّ المِسكينَ الَّذِي لاَ يَجِدُ غِنىً يُغْنِيهِ ، وَلاَ يُفْطَنُ لَهُ فَيُتَصَدَّقُ عَلَيْهِ ، وَلاَ يَقُومُ فَيَسْألَ النَّاسَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Masikini si yule anaeranda kwa watu anarudishwa kwa tonge moja au mbili, tende moja na tende mbili, Ila masikini ni asiyepata cha kumtosheleza wala hakuna anayemjua ili ampe swadaqah, wala hasimami kuomba watu." [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

 

 

 

Share