061-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Ubakhili na Uchoyo
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب النهي عن البخل والشح
061-Mlango Wa Kukatazwa Ubakhili na Uchoyo
قَالَ الله تَعَالَى:
وَأَمَّا مَن بَخِلَ وَاسْتَغْنَىٰ ﴿٨﴾ وَكَذَّبَ بِالْحُسْنَىٰ ﴿٩﴾ فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْعُسْرَىٰ ﴿١٠﴾ وَمَا يُغْنِي عَنْهُ مَالُهُ إِذَا تَرَدَّىٰ ﴿١١﴾
Ama yule afanyaye ubakhili na akajiona amejitosheleza. Na akakadhibisha Al-Husnaa (anayowajibika kuyasadiki). Na Tutamuwepesishia kwa yaliyo magumu. Na itamsaidia nini mali yake atakapoporomoka kuangamia (motoni). [Al-Layl: 8-11]
وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ﴿١٦﴾
Na yeyote anayeepushwa na ubakhili na tamaa ya uchu wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu. [At-Taghaabun: 16]
Hadiyth – 1
وعن جابر رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( اتَّقُوا الظُّلْمَ ؛ فَإِنَّ الظُّلْمَ ظُلُمَاتٌ يَوْمَ القِيَامَةِ . وَاتَّقُوا الشُّحَّ ؛ فَإنَّ الشُّحَّ أهْلَكَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ ، حَمَلَهُمْ عَلَى أنْ سَفَكُوا دِمَاءهُمْ وَاسْتَحَلُّوا مَحَارِمَهُمْ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ogopeni dhuluma, kwani dhuluma, ni giza kwa mwenye kuifanya Siku ya Qiyaamah. Na ogopeni (tahadharini) na ubakhili, kwani ubakhili ndio uliowaangamiza waliokuwa kabla yenu. Huu (ubakhili) uliwapelekea wao kumwaga damu na kuhalalisha vilivyo haramu." [Muslim]