062-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupendelea Wengine na Kusaidiana

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب الإيثار والمواساة

062-Mlango Wa Kupendelea Wengine na Kusaidiana

 

Alhidaaya.com

 

قَالَ الله تَعَالَى:

وَيُؤْثِرُونَ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ ۚ ﴿٩﴾

Na wanawapendelea kuliko nafsi zao japokuwa wao wenyewe wanahitaji. [Al-Hashr: 9]

 

وَيُطْعِمُونَ الطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِ مِسْكِينًا وَيَتِيمًا وَأَسِيرًا﴿٨﴾

Na wanalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini na mayatima na mateka. [Al-Insaan: 8]

 

 

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : إنِّي مَجْهُودٌ، فَأرسَلَ إِلَى بَعْضِ نِسَائِهِ ، فَقالت : وَالَّذي بَعَثَكَ بِالحَقِّ مَا عِنْدِي إِلاَّ مَاءٌ، ثُمَّ أرْسَلَ إِلَى أُخْرَى ، فَقَالَتْ مِثلَ ذَلِكَ ، حَتَّى قُلْنَ كُلُّهُنَّ مِثلَ ذَلِكَ : لا وَالَّذِي بَعَثَكَ بالحَقِّ مَا عِنْدِي إِلاَّ مَاءٌ . فَقَالَ النبي صلى الله عليه وسلم : ((  مَنْ يُضيفُ هَذَا اللَّيْلَةَ ؟ )) فَقَالَ رَجُلٌ مِنَ الأنْصَارِ : أنَا يَا رسولَ الله ، فَانْطَلَقَ بِهِ إِلَى رَحْلِهِ ، فَقَالَ لامْرَأَتِهِ : أكرِمِي ضَيْفَ رسول الله صلى الله عليه وسلم .

وفي روايةٍ قَالَ لامْرَأَتِهِ : هَلْ عِنْدَكِ شَيْءٌ ؟ فقَالَتْ : لاَ ، إِلاَّ قُوتَ صِبيَانِي . قَالَ: فَعَلِّليهم بِشَيْءٍ وَإذَا أرَادُوا العَشَاءَ فَنَوِّمِيهمْ ، وَإِذَا دَخَلَ ضَيْفُنَا فَأطْفِئي السِّرَاجَ ، وَأريهِ أنَّا نَأكُلُ . فَقَعَدُوا وَأكَلَ الضَّيْفُ وَبَاتَا طَاوِيَيْنِ ، فَلَمَّا أصْبَحَ غَدَا عَلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم، فَقَالَ : ((  لَقَدْ عَجبَ الله مِنْ صَنِيعِكُمَا بِضَيْفِكُمَا اللَّيْلَةَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: "Alikuja mtu kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na akamwambia: "Mimi nina njaa." Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akatuma kwa mmoja wa wakeze, Alimjibu: "Naapa kwa aliyekutuma kwa haki sina chochote isipokuwa maji." Kisha akamtuma kwa mwingine, akasema mfano wake: "Naapa kwa aliyekutuma kwa haki sina isipokuwa maji." Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akauliza: "Nani atamkirimu huyu usiku wa leo?", Akasema mtu katika Answaari: "Mimi Ee Rasuli wa Allaah." Akaenda naye nyumbani kwake, akamwambia mkewe: "Mkirimu mgeni wa Rasuli wa Allaah(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)." 

Na katika riwaayah: alimwambia: "Je, una chochote?" Akasema: "La, isipokuwa chakula cha watoto." Akasema: Washughulishe na vitu, wakitaka chakula walalishe. Na anapoingia mgeni wetu zima koroboi, na muonyeshe kuwa tunakula. Wakakaa, na mgeni akala, Wao wakalala na njaa. Kulipo pambazuka alikwenda kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na akamwambia: "Hakika Allaah ameshangazwa kwa kitendo chenu cha usiku kwa mgeni wenu." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم  : ((  طَعَامُ الاثْنَيْنِ كَافِي الثَّلاَثَةِ ، وَطَعَامُ الثَّلاَثَةِ كَافِي الأربَعَةِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

وفي رواية لمسلمٍ عن جابر رضي الله عنه ، عن النبي صلى الله عليه وسلم  ، قَالَ : ((  طَعَامُ الوَاحِدِ يَكْفِي الاثْنَيْنِ ، وَطَعَامُ الاثْنَيْنِ يَكْفِي الأَرْبَعَةَ ، وَطَعَامُ الأَرْبَعَة يَكْفِي الثَّمَانِية ))

Na imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Chakula cha wawili kinatosha watatu, na chakula cha watatu kinatosha wanne." [Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhiy]

Na katika riwaayah ya Muslim kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Chakula cha mmoja kinatosha wawili, na chakula cha wawili kinatosha wanne, na chaula cha wanne kinatosha wanane."

 

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه ، قَالَ : بَيْنَمَا نَحْنُ فِي سَفَرٍ مَعَ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم إذْ جَاءَ رَجُلٌ عَلَى رَاحِلَةٍ لَهُ ، فَجَعَلَ يَصرِفُ بَصَرَهُ يَميناً وَشِمَالاً ، فَقَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  مَنْ كَانَ مَعَهُ فَضْلُ ظَهْرٍ فَليَعُدْ بِهِ عَلَى مَنْ لا ظَهرَ لَهُ ، وَمَنْ كَانَ لَهُ فَضْلٌ مِنْ زَادٍ ، فَلْيَعُدْ بِهِ عَلَى مَنْ لا زَادَ لَهُ )) فَذَكَرَ مِنْ أصْنَافِ المالِ مَا ذكر حَتَّى رَأيْنَا أنَّهُ لاَ حَقَّ لأحَدٍ مِنَّا في فَضْلٍ . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Sa'iyd Al-Khudhriy(Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Tulipokuwa katika safari pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mara akaja mtu akiwa amepanda kipandio chake na huku anatizama kuliani na kushotoni kwake. Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): 'Yeyote ambaye ana kipando cha ziada (mnyama wa kupanda) basi ampatie (kama swadaqah) asiyekuwa nao; na yoyote mwenye ziada ya chakula basi atoe swadaqah kwa asiyekuwa nacho.' Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaendelea kutaja aina tofauti ya mali mpaka tukadhania kuwa hapana haki ya mmoja wetu kuwa na ziada ya chochote." [Muslim] 

 

 

Hadiyth – 4

وعن سهل بن سعدٍ رضي الله عنه : أنَّ أمْرَأةً جَاءَتْ إِلَى رسول الله صلى الله عليه وسلم بِبُرْدَةٍ مَنْسُوجَةٍ ، فَقَالَتْ : نَسَجْتُها بِيَدَيَّ لأَكْسُوكَهَا ، فَأَخَذَهَا النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم مُحْتَاجاً إِلَيْهَا ، فَخَرَجَ إِلَيْنَا وَإنَّهَا إزَارُهُ ، فَقَالَ فُلانٌ : اكْسُنِيهَا مَا أحْسَنَهَا ! فَقَالَ : ((  نَعَمْ )) فَجَلَسَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم في المَجْلِسُ ، ثُمَّ رَجَعَ فَطَواهَا ، ثُمَّ أرْسَلَ بِهَا إِلَيْهِ : فَقَالَ لَهُ الْقَومُ : مَا أحْسَنْتَ ! لَبِسَهَا النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم مُحتَاجَاً إِلَيْهَا ، ثُمَّ سَألْتَهُ وَعَلِمْتَ أنَّهُ لا يَرُدُّ سَائِلاً ، فَقَالَ : إنّي وَاللهِ مَا سَألْتُهُ لألْبِسَهَا ، إنَّمَا سَألْتُهُ لِتَكُونَ كَفنِي . قَالَ سَهْلٌ : فَكَانَتْ كَفَنَهُ . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Sahl bin Sa'd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa mwanamke alimjia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na shuka iliyofumwa akasema: "Nimeifuma kwa mikono yangu ili nikuvalishe." Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaichukua kwani alikuwa anaihitaji, aliivaa kama izari yake (kikoi). Mtu akasema: "Nipe mimi kwani ni kizuri sana." Akasema: "Ndio." Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akakaa katika kikao, aliingia ndani, akakikunja na kumpelekea. Watu wakamwambia: "Hukufanya vizuri kwani Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikivaa kwa kuwa anakihitaji nawe ukamuomba akupati huku ukijua kuwa yeye hamrudishi mtupu mwenye kumuomba." Akasema: "Wa-Allaahi mimi sikumuomba ili nikivae, bali nimemuomba ili iwe sanda yangu." Akasema Sahl: "Hiyo ndiyo iliyokuwa sanda yake." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي موسى رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  إنَّ الأشْعَرِيِّينَ إِذَا أرْمَلُوا في الغَزْوِ ، أَوْ قَلَّ طَعَامُ عِيَالِهِمْ بالمَديِنَةِ ، جَمَعُوا مَا كَانَ عِنْدَهُمْ في ثَوْبٍ وَاحِدٍ ، ثُمَّ اقْتَسَمُوهُ بَيْنَهُمْ في إنَاءٍ وَاحدٍ بالسَّوِيَّةِ فَهُمْ مِنِّي وَأنَا مِنْهُمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Muwsaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Al'Ash'ariyy wanapoenda vitani au chakula cha ukoo kikipungua Madiynah, wana jumuisha walivyonavyo katika nguo moja, kisha wanagawana baina yao sawasawa katika chombo kimoja. Hivyo wao ni pamoja na mimi, nami ni pamoja na wao." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

 

Share