Kuku Wa Sosi Tamu (Trinidad)
Kuku Wa Sosi Tamu (Trinidad)
Vipimo
Kuku - 6 LB
Kitunguu saumu/thomu na tangawizi iliyosagwa - 2 vijiko vya supu
Mtindi (Yoghurt) - 2 vijiko vya supu
Chumvi - kiasi
Pilipili nyekundu ya unga - 1 kijiko cha chai
Sosi
Mafuta - 2 vijiko vya supu
Thomu iliyosagwa - 1 kijiko cha chai
Sosi ya tomato (tomato sauce) - ¼ kikombe
Sosi ya HP - 2 Vijiko vya supu
Cellery - 1 mche
Parsley na kotmiri - ¼ kikombe
Nyanya - 3
Chumvi - kiasi
Pilipili manga - 1 Kijiko cha supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Mkate kuku vipande vikubwa vikubwa, msafishe kwa siki atoke harufu
- Mrowanishe na thomu, tangawizi , chumvi, mtindi na pilipili kwa muda wa saa au zaidi.
- Mtie katika tryea ya kupikia katika oveni.
- Mchome kwa moto juu (grill) au ukipenda moto wa chini (bake) , akishawiva pakua katika bakuli la kupakulia.
- Tengeneza sosi kwa kufanya ifuatavyo:
- Saga kwanza Nyanya, cellery, parsely na kotmiri.
- Kaaanga thomu katika mafuta kisha tia sosi zote pamoja na mchanganyiko uliosaga wa cellery.
- Mwagia sosi katika kuku akiwa tayari kuliwa.
Kidokezo : Nzuri kula na wali kama pilau kavu au upendavyo.