Kamba Wa Unga Wa Dengu
Kamba Wa Unga Wa Dengu
Vipimo
Kamba wakubwa - 1 pakiti
Unga wa dengu - 1 Kikombe cha chai
Pilipili ya unga - Kiasi unavyopenda
Yai - 1
Chumvi - Kiasi
Bizari ya giligilani ya unga - ¼ Kijiko cha chai
Maji - Kiasi ya kuchanganyia
Mafuta ya kukaangia
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Chambua maganda ya kamba na bakisha mikia tu.
- Kwenye bakuli, changanya unga, chumvi, pilipili, bizari, yai na maji kisia ili mchanganyiko usiwe mzito sana.
- Weka mafuta katika karai yapate moto.
- Chovya kamba kwenye mchanganyiko wa dengu kwa kukamata mkia na uzikaange mpaka zigeuke rangi.
- Weka katika karatasi au chujio zichuje mafuta na zitakuwa tayari kuliwa na chatini upendayo.
