Faluda (Pakistani)
Faluda (Pakistani)

VIPIMO: Kutengenezea glass 12
Tambi- 200 - 300 gms
Jelly ya Cherry - 2 pkts ndogo
Condensed milk - 1 tin
Fruit Cocktail au peaches (cubes)(ukipenda) - 1 tin
Vanilla Ice-cream - kiasi
Rose Syrup - kiasi
Habbat Rayhaan (Basil Seeds) - 1 tablespoon
au kwa jina la Kipakistani ni Tukhme-Rayhaan
(sio lazima ukipenda) – Rowanisha
NAMNA YA KUTAYARISHA
- Tengeneza Jelly kama inavyoeleza katika pakti. Inapokuwa tayari imeganda ikate kate vipande vya cubes.
- Chemsha tambi, chuja maji weka kando.
- Katika glass, gawa vitu vyote na kupanga kwa mpango huu:
- Tambi
- Weka jelly cubes
- Weka fruit cocktail au peaches
- Tia condensed milk
- Tia Habbat-Rayhaan kama ½ teaspoon
- Tia scoop za ice-cream mbili
- Mwisho tia rose Syrup kidogo juu ya ice-cream na tayari kuliwa.
