64-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الإِلهُ
Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi
(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)
الإِلهُ
الإِلهُ Al-Ilaah Ilaah - Mwabudiwa Wa Haki
|
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
أَمْ كُنتُمْ شُهَدَاءَ إِذْ حَضَرَ يَعْقُوبَ الْمَوْتُ إِذْ قَالَ لِبَنِيهِ مَا تَعْبُدُونَ مِن بَعْدِي قَالُوا نَعْبُدُ إِلَـٰهَكَ وَإِلَـٰهَ آبَائِكَ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ ﴿١٣٣﴾
Je, mlikuwa mashahidi wakati mauti yalipomfikia Ya’quwb alipowaambia wanawe: Mtaabudu nini baada yangu? Wakasema: Tutamwabudu Ilaaha wako (Allaah) na Ilaaha wa baba zako, Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq; Ilaah Mmoja, nasi ni Waislamu (tunajisalimisha) Kwake. [Al-Baqarah (2): 133]