02-Vipi Uweze Kuhifadhi Qur-aan? (كَيْفَ تَحْفَظُ الْقُرآن): Fadhila Za Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan

 Vipi Uweze Kuhifadhi Qur-aan?

 

كَيْفَ تَحْفَظُ الْقُرآن؟

 

Alhidaaya.com

 

 

02-Fadhila Za Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan

 

 

02- Fadhila Za Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan

 

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Amewafanyia Ihsaan kubwa Waumini kwa kuwaletea Maneno Yake Mwenyewe kupitia kwa Rasuli Wake kama Anavyosema:

 

لَقَدْ مَنَّ اللَّـهُ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ إِذْ بَعَثَ فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْ أَنفُسِهِمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿١٦٤﴾

Kwa yakini Allaah Amewafanyia fadhila Waumini pale Alipomtuma kwao, Rasuli miongoni mwao, anawasomea Aayaat Zake na anawatakasa na anawafunza Kitabu na Hikmah (Sunnah); japokuwa walikuwa kabla katika upotofu bayana. [Aal-‘Imraan: 164]

 

 

Na ihsaan na fadhila hiyo inatokana na du’aa ya baba wa Manabii ambaye ni Nabiy Ibraahiym (عليه السلام), ambaye aliomba baada ya kujenga Al-Ka’bah:

 

رَبَّنَا وَابْعَثْ فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِكَ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُزَكِّيهِمْ ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٢٩﴾

Rabb wetu, wapelekee Rasuli miongoni mwao atakayewasomea Aayaat Zako na atakayewafunza Kitabu na Hikmah na atakayewatakasa. Hakika Wewe ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Al-Baqarah: (2:  129)]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

كَمَا أَرْسَلْنَا فِيكُمْ رَسُولًا مِّنكُمْ يَتْلُو عَلَيْكُمْ آيَاتِنَا وَيُزَكِّيكُمْ وَيُعَلِّمُكُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُعَلِّمُكُم مَّا لَمْ تَكُونُوا تَعْلَمُونَ ﴿١٥١﴾

Kama Tulivyomtuma kwenu Rasuli anayetokana na nyinyi, anawasomea Aayaat Zetu na anakutakaseni na anakufunzeni Kitabu na Hikmah (Sunnah), na anakufundisheni mambo ambayo hamkuwa mkiyajua. [Al-Baqarah (2: 151)]

 

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

هُوَ الَّذِي بَعَثَ فِي الْأُمِّيِّينَ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ﴿٢﴾

 

Yeye Ndiye Aliyepeleka Rasuli kwa wasiojua kusoma wala kuandika miongoni mwao anawasomea Aayaat Zake na Anawatakasa, na Anawafunza Kitabu na Hikmah na japo walikuwa hapo kabla katika upotofu bayana. [Al-Jumu’ah (62: 2)]

 

 

Na Allaah (سبحانه وتعالى) Akaendelea kumuamrisha Rasuli Wake aisome Qur-aan katika Aayah zifuatazo: 

 

إِنَّمَا أُمِرْتُ أَنْ أَعْبُدَ رَبَّ هَـٰذِهِ الْبَلْدَةِ الَّذِي حَرَّمَهَا وَلَهُ كُلُّ شَيْءٍ ۖ وَأُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْمُسْلِمِينَ ﴿٩١﴾ وَأَنْ أَتْلُوَ الْقُرْآنَ ۖ

Hakika nimeamrishwa nimwabudu Rabb wa mji huu Ambaye Ameufanya mtukufu, na ni Vyake Pekee vitu vyote. Na nimeamrishwa kwamba niwe miongoni mwa Waislamu. Na kwamba nisome Qur-aan [An-Naml: (27:  91-92)]

 

Na pia:

 

اتْلُ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِنَ الْكِتَابِ وَأَقِمِ الصَّلَاةَ ۖ

Soma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uliyoletewa Wahy katika Kitabu na simamisha Swalaah. [Al-‘Ankabuwt (29:  45)]

 

 

Nabiy akawasomea Sahaba zake nao wakaendeleza kuisoma na kuifundisha hadi kuwafikia Waumini wa zama zote.  

 

Kuisikiliza au kuisoma Qur-aan   kunampelekea msikilizaji au msomaji kuhisi kuwa anasemeshwa na Muumba wake.  Hili ndilo linaloipa Qur-aan daraja na nafasi isiyokadirika kwa Muumini, kwani Muumini khasa ni yule anayeamini kuwa Qur-aan ni Maneno ya Allaah yaliyoteremshwa kwa Nabiy Muhammad kupitia kwa Jibril (عليه السلام) na kwamba kusomwa kwake ni ‘ibaadah.

 

 

Fadhila za kusoma, kuhifadhi na kuisikiliza Qur-aan ni nyingi kama zilivyotajwa katika Qur-aan na Sunnah. Vitabu na makala nyingi zimeandikwa kuhusiana na hilo; zifuatazo ni baadhi ya fadhila zake:

 

 

i-Kuisoma Qur-aan Ni Biashara Isiyofilisika, Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

إِنَّ الَّذِينَ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّـهِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَنفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً يَرْجُونَ تِجَارَةً لَّن تَبُورَ ﴿٢٩﴾ لِيُوَفِّيَهُمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِ ۚ إِنَّهُ غَفُورٌ شَكُورٌ ﴿٣٠﴾

Hakika wale wanaosoma Kitabu cha Allaah na wakasimamisha Swalaah, na wakatoa kutokana na yale Tuliyowaruzuku kwa siri na dhahiri wanataraji tijara isiyoteketea. Ili (Allaah) Awalipe ujira wao timilifu, na Awazidishie kutokana na fadhila Zake, hakika Yeye ni Mwingi wa kughufuria, Mwingi wa kupokea shukurani. [Faatwir (35: 29-30)]

 

 

ii-Mwenye Kujifundisha Kisha Akaifundisha Naye Ni Mbora Miongoni Mwa Waumini:

 

 

Bila shaka jambo lenye ubora, au uzuri wa kitu, huthibiti kwa sababu hii au ile au kwa kufungamana na mwenye hicho kitu; na ubora au uzuri wa Qur-aan ni kwa kuwa ni Maneno ya Aliyembora kabisa; na kuna ubora gani ulimwengu huu kuliko mtu kujifunza au  kufundisha Maneno ya Allaah; jambo alilolianza  mwalimu aliyebora kuliko wote hapa duniani ambaye ni Nabiy . Hivyo hakuna kazi wala amali iliyobora kuliko ile kazi au amali aliyoifanya Nabiy ambayo ni kusoma na kuisomesha Qur-aan kama ilivyothibiti katika Hadiyth:

 

 

 عَنْ عُثْمَانَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((خَيْرُكُمْ مَنْ تَعَلَّمَ الْقُرْآنَ وَعَلَّمَهُ)) 

Imepokelewa kutoka kwa 'Uthmaan bin 'Affaan (رضي الله عنه)  kwamba Nabiy amesema: ((Mbora wenu ni yule mwenye kujifunza Qur-aan kisha akaifundisha)) [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhy, An-Nasaaiy, Abu Daawuwd, Ahmad ]

 

 

 

iii-Kuisoma Qur-aan Ni Kuchuma Thawabu Kwa Kila Herufi Moja:

 

 

Kuisoma au kuisomesha Qur-aan ni ‘ibaadah kama ilivyotangulia; na ni ‘ibaadah yenye malipo makubwa kama itafungamana na sharti mojawapo katika masharti ya ‘ibaadah katika Uislamu; nayo ni    ikhlaasw (Niya safi kwa ajili ya Allaah). Hivyo mwenye kuisoma Qur-aan kwa ikhlaasw huwa ana matarajio ya malipo kama haya yaliyothibiti katika Hadiyth ya ibn Mas’uwd (رضي الله عنه) kwamba Nabiy amesema:

 

((مَنْ قَرَأَ حَرْفًا مِنْ كِتَابِ اللَّهِ فَلَهُ بِهِ حَسَنَةٌ وَالْحَسَنَةُ بِعَشْرِ أَمْثَالِهَا لَا أَقُولُ الم حَرْفٌ وَلَكِنْ أَلِفٌ حَرْفٌ وَلَامٌ حَرْفٌ وَمِيمٌ حَرْفٌ))

((Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Allaah atapata hasanah [jema] moja, na kila hasanah moja ni sawa na thawabu kumi, wala sisemi 'Alif-Laam-Miym' ni herufi moja, bali Alif ni herufi moja na Laam ni herufi moja na Miym ni herufi moja)) [At-Tirimidhiy]

 

 

iv-Mwenye Kufungamana Na Qur-aan Huwa Ni Miongoni Mwa Watu Wake Allaah (سبحانه وتعالى) Walio Karibu Naye Na Awapendao:

 

 

Qur-aan kama tuaminivo ni Maneno ya Allaah, hivyo mwenye kushikamana nayo huwa ni miongoni mwa watu Wake Allaah Anaowapenda. Imethibiti hili katika Hadiyth ifuatayo: 

 

 عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((إِنَّ لِلَّهِ أَهْلِينَ مِنْ النَّاسِ)) قَالُوا يَا رَسُولَ اللَّهِ مَنْ هُمْ قَالَ:  ((هُمْ أَهْلُ الْقُرْآنِ أَهْلُ اللَّهِ وَخَاصَّتُهُ))

 

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik  (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah amesema:  ((Allaah Ana watu wake (makhsusi) kati ya wanaadamu)) Wakauliza: Ee Rasuli wa Allaah,  hao ni akina nani? Akasema: ((Hao ni watu wa Qur-aan na ni watu wa Allaah wateule Wake (Awepandao))) [Ahmad, Ibn Maajah] 

 

 

 

v-Mwenye Kuisoma Kwa Mashaka  Hupata Thawabu Mara Mbili Yake:

 

 

Nabiy hakutaka Waislamu wakate tamaa au waache mara moja kuisoma au kujifunza Qur-aan; huenda kutokana na sababu ya kutokuwa na lafdhi ya lugha ya Kiarabu kwa wasiokuwa na asili ya Kiarabu au kwa sababu ya uzito wa ulimi na akili hivyo basi ikawa ni shida kwa mtu huyo kuisoma kwa kudodosa dodosa.  Basi Nabiy aliwatia nguvu Waislamu kwa kuwahakikishia kuwa malipo msomaji anayesumbuka kujifunza na kuisoma Qur-aan ni mara mbili: 

 

 عَنْ عَائِشَةَ قَالَتْ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((الْمَاهِرُ بِالْقُرْآنِ مَعَ السَّفَرَةِ الْكِرَامِ الْبَرَرَةِ وَالَّذِي يَقْرَأُ الْقُرْآنَ وَيَتَتَعْتَعُ فِيهِ وَهُوَ عَلَيْهِ شَاقٌّ لَهُ أَجْرَانِ))  

Imepokelewa kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها) kwamba Rasuli wa Allaah amesema: ((Yule aliyekuwa hodari wa kusoma Qur-aan atakuwa pamoja na Malaika Waandishi wa Allaah, watukufu, wema. Na yule ambaye anaisoma Qur-aan kwa mashaka na huku anajitahidi kwa kudodosa atapata ujira mara mbili)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

vi-Harufu Nzuri Na Ladha Nzuri Kwa Anayeisoma Qur-aan:

 

 

Nabiy ametofautisha mfano wa Muumini anayesoma na asiyesoma Qur-aan katika Hadiyth ifuatayo: iliyopokelewa toka kwa

 

Kutoka kwa Abu Muwsaa Al-Ash'ariy (رضي الله عنه): kwamba Nabiy amesema:

 

 ((مَثَلُ الْمُؤْمِنِ الَّذِي يَقْرَأُ الْقُرْآنَ كَمَثَلِ الْأُتْرُجَّةِ رِيحُهَا طَيِّبٌ وَطَعْمُهَا طَيِّبٌ وَمَثَلُ الْمُؤْمِنِ الَّذِي  لَا يَقْرَأُ الْقُرْآنَ كَمَثَلِ التَّمْرَةِ لَا رِيحَ لَهَا وَطَعْمُهَا حُلْوٌ))  

 ((Mfano wa Muumini ambaye anayesoma Qur-aan ni kama tunda la Utrujjah;  harufu yake nzuri na ladha yake nzuri. Na mfano wa Muumini asiyesoma Qur-aan mfano wake kama tende zisizokuwa na harufu lakini zina ladha tamu))

 

 

Utrujjah: Tunda linalofanana na ndimu lenye rangi ya orenji inayokaribia rangi ya dhahabu, linajulikana kama tufaha la ki-Ajemi. Lina harufu nzuri kabisa.

 

 

vii-Qur-aan Ni Shafaa’ah (Kiombezi) Siku Ya Qiyaamah:

 

 

Mwenye kupenda kutafuta marafiki na maswahiba wa kweli na wakumfaa basi afanye usahiba na Qur-aan kwa sababu haitamtupa kamwe    swahiba wake wakati wa shida na fazaa za Siku Ya Qiyaamah: 

 

 

عن أبي أُمَامَةَ الْبَاهِلِيُّ قَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((اقْرَءُوا الْقُرْآنَ فَإِنَّهُ يَأْتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ شَفِيعًا لِأَصْحَابِهِ))

 

Imepokelewa kutoka kwa Abu Umaamah Al-Baahiliyy (رضي الله عنه) ambaye amesema: “Nimemskia Rasuli wa Allaah akisema: ((Someni Qur-aan kwani itakuja siku ya Qiyaamah ikimuombea aliyekuwa swahiba wake [mwenye kuisoma])) [Muslim]

 

 

 

viii-Qur-aan Humnyanyua Na Kumpandisha Daraja Mwenye Kushikamana Nayo:

 

 

 

قَالَ عُمَرُ أَمَا إِنَّ نَبِيَّكُمْ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَدْ قَالَ: ((إِنَّ اللَّهَ يَرْفَعُ بِهَذَا الْكِتَابِ أَقْوَامًا وَيَضَعُ بِهِ آخَرِينَ)) 

'Umar (رضي الله عنه) amesema: “Nabiy wenu amesema: ((Allaah Atawanyanyua baadhi ya watu kwa kitabu hiki [Qur-aan] na Atawadhalilisha wengine kwa kitabu hiki)) [Muslim Ibn Maajah, Ahmad]

 

 

ix-Qur-aan Humpandisha Mtu Daraja Ya Jannah:

 

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:  ((يُقَالُ لِصَاحِبِ الْقُرْآنِ اقْرَأْ وَارْتَقِ وَرَتِّلْ كَمَا كُنْتَ تُرَتِّلُ فِي الدُّنْيَا فَإِنَّ مَنْزِلَتَكَ عِنْدَ آخِرِ آيَةٍ تَقْرَأُ بِهَا))

 

Imepokelewa kutoka kwa 'Abdullaah bin 'Umar   (رضي الله عنهما) kwamba Nabiy amesema: ((Huambiwa swahiba wa Qur-aan [aliyeshikamana na Qur-aan]: “Soma na panda [juu katika daraja za Pepo]  na uisome kwa 'Tartiyl' [ipasavyo kwa tajwiyd] kama ulivyokuwa ukiisoma ulipokuwa duniani, kwani makazi yako ni pale utakapofika katika Aayah ya mwisho utakayoisoma))  [At-Tirmidhiy, Abu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad]

 

 

 

x-Huteremka Malaika Kwa Utulivu Na Rahmah Kwa Wanaosoma Qur-aan:

 

 

 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَا اجْتَمَعَ قَوْمٌ فِي بَيْتٍ مِنْ بُيُوتِ اللَّهِ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّهِ وَيَتَدَارَسُونَهُ بَيْنَهُمْ إِلَّا نَزَلَتْ عَلَيْهِمْ السَّكِينَةُ وَغَشِيَتْهُمُ الرَّحْمَةُ وَحَفَّتْهُمُ الْمَلَائِكَةُ وَذَكَرَهُمُ اللَّهُ فِيمَنْ عِنْدَهُ)) 

Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه)  kwamba Rasuli wa Allaah amesema ((Hawakusanyiki pamoja watu katika miongoni mwa nyumba za Allaah wakisoma kitabu cha Allaah, na wanafundishana baina yao, ila huwateremkia utulivu na hufunikwa na Rahmah na Malaika huwazunguka na Allaah Anawataja mbele ya [Malaika] aliokuwa nao)) [Muslim Abu Daawuwd, Ibn Maajah , Ahmad]

 

 

Pia,

 

عن أُسَيْدَ بْنَ حُضَيْرٍ بَيْنَمَا هُوَ لَيْلَةً يَقْرَأُ  فِي ِرْبَدِهِ، إِذْ جَالَتْ فَرَسُهُ، فَقَرَأَ ثُمَّ جَالَتْ أُخْرَى،  فَقَرَأَ ثُمَّ جَالَتْ أَيْضًا. قَالَ أُسَيْدٌ:  "فَخَشِيتُ أَنْ تَطَأَ يَحْيَى فَقُمْتُ إِلَيْهَا فَإِذَا مِثْلُ الظُّلَّةِ فَوْقَ رَأْسِي فِيهَا أَمْثَالُ السُّرُجِ عَرَجَتْ فِي الْجَوِّ حَتَّى مَا أَرَاهَا". قَالَ: "فَغَدَوْتُ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ بَيْنَمَا أَنَا الْبَارِحَةَ مِنْ جَوْفِ اللَّيْلِ أَقْرَأُ فِي مِرْبَدِي إِذْ جَالَتْ فَرَسِي". فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((اقْرَأْ ابْنَ حُضَيْرٍ)) قَالَ: "فَقَرَأْتُ ثُمَّ جَالَتْ أَيْضًا". فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((اقْرَأْ ابْنَ حُضَيْرٍ)) قَالَ:  "فَقَرَأْتُ ثُمَّ جَالَتْ أَيْضًا". فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((اقْرَأْ ابْنَ حُضَيْرٍ)) قَالَ: "فَانْصَرَفْتُ وَكَانَ يَحْيَى قَرِيبًا مِنْهَا خَشِيتُ أَنْ تَطَأَهُ، فَرَأَيْتُ مِثْلَ الظُّلَّةِ فِيهَا أَمْثَالُ السُّرُجِ عَرَجَتْ فِي الْجَوِّ حَتَّى مَا أَرَاهَا". فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((تِلْكَ الْمَلَائِكَةُ كَانَتْ تَسْتَمِعُ لَكَ وَلَوْ قَرَأْتَ لَأَصْبَحَتْ يَرَاهَا النَّاسُ مَا تَسْتَتِرُ مِنْهُمْ))

 

Imepokelewa kutoka kwa Usayd bin Khudhwayr, kwamba alipokuwa akisoma akiwa katika mirbad[1] yake akashtuka farasi wake. Akasoma, kisha    akashtuka   tena, akasoma kisha akashtuka tena. Akasema Usayd: Nikaogopa asije kumkanyaga Yahya (mwanawe). Nikainuka kumwendea (farasi) nikaona kitu kama kivuli juu ya kichwa changu kama kina kandili kikipanda mbinguni hadi kikapotea. Nikamwendea Rasuli wa Allaah siku ya pili nikwamwambia: “Ee Rasuli wa Allaah! Jana usiku nilipokuwa katika mirbad yangu nikisoma Qur-aan, farasi wangu alishtuka!  Rasuli wa Allaah akasema: ((Soma Ibn Khudhwayr)). Akasema: Nilisoma lakini alishtuka tena. Rasuli wa Allaah akasema: ((Soma Ibn Khudhwayr)). Akasema: Nilisoma lakini alishtuka tena. Rasuli wa Allaah akasema ((Soma Ibn Khudhwayr)). Akasema niliondoka kwani Yahya alikuwa karibu naye, nikahofu asimkanyage. Nikaona kama kivuli kikiwa na taa kinapanda juu hadi kikapotea. Akasema Rasuli wa Allaah : ((Hao ni Malaika walikuwa wakikusikiliza, lau ungeliendelea kusoma hadi asubuhi watu wangelikiona kisingelipotea)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

xi-Kuhifadhi Na Kujifunza Maana Ya Qur-aan Ni Bora Kuliko Mapambo Ya Dunia:

 

عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ قَالَ خَرَجَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَنَحْنُ فِي الصُّفَّةِ فَقَالَ: ((أَيُّكُمْ يُحِبُّ أَنْ يَغْدُوَ كُلَّ يَوْمٍ إِلَى بُطْحَانَ أَوْ إِلَى الْعَقِيقِ فَيَأْتِيَ مِنْهُ بِنَاقَتَيْنِ كَوْمَاوَيْنِ فِي غَيْرِ إِثْمٍ وَلَا قَطْعِ رَحِمٍ؟)) فَقُلْنَا يَا رَسُولَ اللَّهِ نُحِبُّ ذَلِكَ قَالَ: ((أَفَلَا يَغْدُو أَحَدُكُمْ إِلَى الْمَسْجِدِ فَيَعْلَمُ أَوْ يَقْرَأُ آيَتَيْنِ مِنْ كِتَابِ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ خَيْرٌ لَهُ مِنْ نَاقَتَيْنِ وَثَلَاثٌ خَيْرٌ لَهُ مِنْ ثَلَاثٍ وَأَرْبَعٌ خَيْرٌ لَهُ مِنْ أَرْبَعٍ وَمِنْ أَعْدَادِهِنَّ مِنْ الْإِبِلِ))

Imepokelewa toka kwa 'Uqbah bin 'Aamir(رضي الله عنه)   ambaye amesema: “Rasuli wa Allaah alitujia wakati tulikuwa katika Swuffah[2] akauliza: ((Kuna yeyote miongoni mwenu anayetaka kwenda soko la Butw-haan[3] au [soko] la Al-'Aqiyq[4] na akapata humo ngamia wawili wakubwa na waliyonona bila ya kutenda dhambi au kukata undugu?)) Tukajibu kwamba sote tunapenda kufanya na kupata hivyo. Kisha akasema: ((Basi aende mmoja wenu msikitini akajifunze au asome Aayah mbili katika kitabu cha Allaah عزوجل basi akifanya hivyo ni bora kuliko ngamia wawili. Na Aayah tatu ni bora kuliko ngamia watatu, na Aayah nne ni bora kuliko ngamia wanne, na mfano wa hivyo hivyo wa Aayah kwa ngamia)) [Muslim, Abu Daawuwd, Ahmad]

 

 

X2-Mwenye Kuhifadhi Qur-aan Huvalishwa Taji Siku Ya Qiyaamah:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((يَجِيءُ الْقُرْآنُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَيَقُولُ يَا رَبِّ حَلِّهِ،  فَيُلْبَسُ تَاجَ الْكَرَامَةِ ثُمَّ يَقُولُ: يَا رَبِّ زِدْهُ، فَيُلْبَسُ حُلَّةَ الْكَرَامَةِ ثُمَّ يَقُولُ: يَا رَبِّ ارْضَ عَنْهُ فَيَرْضَى عَنْهُ فَيُقَالُ لَهُ: اقْرَأْ وَارْقَ.  وَتُزَادُ بِكُلِّ آيَةٍ حَسَنَةً))  

Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه)  kwamba, Rasuli wa Allaah amesema: ((Qur-aan itakuja siku ya Qiyaamah na itasema: “Ee Rabb, Mpambe” [Mwenye kuhifadhi Qur-aan]. Kisha atavalishwa taji. Kisha [Qur-aan] itasema: “Ee Rabb, muongeze”. Kisha huyo mtu atavishwa nguo ya heshim. Kisha itasema: “Ee Rabb, Ridhika naye”. Allaah, Ataridhika naye. Kisha ataambiwa: “Soma na panda”. Atapokea thawabu zaidi ya mema kwa kila Aayah [atakayosoma])) [At-Tirmidhy na Al-Haakim]

 

 

 

X3-Mwenye Ujuzi Zaidi Wa Qur-aan Huwa Na Mwanga Kaburini:

 

 

عن جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَجْمَعُ بَيْنَ الرَّجُلَيْنِ مِنْ قَتْلَى أُحُدٍ فِي ثَوْبٍ وَاحِدٍ ثُمَّ يَقُولُ:  ((أَيُّهُمَا أَكْثَرُ أَخْذًا لِلْقُرْآنِ)) فَإِذَا أُشِيرَ إِلَى أَحَدِهِمَا قَدَّمَهُ فِي اللَّحْدِ  

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه) kwamba alikuwa Rasuli wa Allaah akiwakusanya watu wawili waliokufa katika vita vya       Uhud katika nguo moja kisha anauliza, ((Nani katika hao mwenye ujuzi zaidi wa Qur-aan?)) Anapojulishwa mmoja kati ya hao, humtanguliza mwanandani)) [Al-Bukhaariy, An Nasaaiy]

 

 

[1] Sehemu ya mifugo ya farasi

 

[2] Sehemu katika Msikiti wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) waliyokuwa wakikaa Swahaba ambao hali zao walikuwa ni masikini.  

 

[3] Bonde lilioko Kusini mwa mji wa Madiynah kuelekea upande wa Magharibi karibu na Jabali la Sal’. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitawadha katika bonde hili siku ya vita vya Khandaq

 

[4] Bonde maarufu kabisa katika mji wa Madiynah au eneo la Al-Hijaaz yote. Liko umbali wa maili kilometa mia Kusini na linaelekea upande wa Mashariki. Linajulikana kuwa ni ‘Bonde lenye Baraka’.

 

 

Share