069-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupendekeza Kujitenga Wakati wa Uharibifu na Ufisadi au Hofu ya Fitnah Katika Dini au Kujiingiza Katika Haramu na Shaka

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب استحباب العزلة عند فساد الناس والزمان

069-Mlango Wa Kupendekeza Kujitenga Wakati wa Uharibifu na Ufisadi au Hofu ya Fitnah Katika Dini au Kujiingiza Katika Haramu na Shaka

 

 

Alhidaaya.com

 

قَالَ الله تَعَالَى:

فَفِرُّوا إِلَى اللَّـهِ ۖ إِنِّي لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ مُّبِينٌ ﴿٥٠﴾

Basi kimbilieni kwa Allaah, hakika mimi kwenu ni mwonyaji bayana kutoka Kwake. [Adh-Dhaariyaat: 50]

 

 

Hadiyth – 1

وعن سعد بن أَبي وقاص رضي الله عنه  ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : ((  إنَّ الله يُحِبُّ الْعَبْدَ التَّقِيَّ الغَنِيّ الْخَفِيَّ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Sa'd bin Abu Waqqaas (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakika Allaah anampenda mja mchamngu mwenye utajiri wa nafsi na asiyejionesha." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رَجُلٌ : أيُّ النَّاسِ أفْضَلُ يَا رسولَ الله ؟ قَالَ : ((  مُؤْمِنٌ مُجَاهِدٌ بِنَفْسِهِ وَمَالِهِ في سَبيلِ اللهِ )) قَالَ : ثُمَّ مَنْ ؟  قَالَ : ((  ثُمَّ رَجُلٌ مُعْتَزِلٌ فِي شِعْبٍ مِنَ الشِّعَابِ يَعْبُدُ رَبَّهُ )) . وفي رواية : ((  يَتَّقِي اللهَ ، وَيَدَعُ النَّاسَ مِنْ شَرِّهِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Mtu alisema: "Ee Rasuli wa Allaah! Mtu gani bora zaidi?" Akasema: "Muumini anayepigana kwa nafsi yake na mali yake katika njia ya Allaah." Akasema: "Kisha ni nani?" Akasema: "Kisha mtu aliyejitenga katika bonde miongoni mwa mabonde akimuabudu Rabb wake." Katika riwaayah: "Anamcha Allaah na kuacha watu na shari yake (kutowaudhi)." [Al-Bukhaariy na Muslim] 

 

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم  : ((  يُوشِكُ أنْ يَكُونَ خَيْرَ مَالِ المُسْلِمِ غَنَمٌ يَتَّبعُ بِهَا شَعَفَ الجِبَالِ ، وَمَواقعَ الْقَطْر يَفِرُّ بِدينِهِ مِنَ الفِتَنِ )) رواه البخاري .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Wakati upo karibu ambapo mali bora ya Muislamu itakuwa ni mbuzi wengi ambao atakwenda nao juu ya jabali au sehemu ya mvua ili kuilinda Dini yake kutokana na fitna." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  مَا بَعَثَ اللهُ نَبِيّاً إِلاَّ رَعَى الْغَنَمَ )) فَقَالَ أصْحَابُهُ : وأنْتَ ؟ قَالَ : ((  نَعَمْ ، كُنْتُ أرْعَاهَا عَلَى قَرَارِيطَ لأَهْلِ مَكَّةَ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaah hakutuma Nabiy, ila Nabiy huyu alichunga mbuzi." Swahaabah wakauliza: "Hata wewe?" Akasema: "Ndio nilikuwa nikichunga kwa watu wa Makkah na nikilipwa Qaraarit (kipimo maalum cha dhahabu chenye wizani wa 1/24 ya dinari)." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم ، أنَّه قَالَ : ((  مِنْ خَيْرِ مَعَاشِ النَّاسِ لهم رَجُلٌ مُمْسِكٌ عِنَانَ فَرَسِهِ في سَبيلِ الله، يَطيرُ عَلَى مَتْنِهِ كُلَّمَا سَمِعَ هَيْعَةً أَوْ فَزعَةً ، طَارَ عَلَيْهِ يَبْتَغِي القَتْلَ ، أَوْ المَوْتَ مَظَانَّه ، أَوْ رَجُلٌ فِي غُنَيمَةٍ في رَأسِ شَعَفَةٍ مِنْ هذِهِ الشَّعَفِ ، أَوْ بَطنِ وَادٍ مِنْ هذِهِ الأَوْدِيَةِ ، يُقِيمُ الصَّلاَةَ ، وَيُؤتِي الزَّكَاةَ ، وَيَعْبُدُ رَبَّهُ حَتَّى يأتِيَهُ اليَقِينُ ، لَيْسَ مِنَ النَّاسِ إِلاَّ فِي خَيْرٍ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Maisha yaliyo bora miongoni mwa watu ni mtu kushika hatamu za farasi katika njia ya Allaah. Anampanda kwenye mgongo wake na kuruka nae (kwenda haraka) pindi tu anaposikia sauti ya vita (kuwa vipo tayari) au mfano wake wa fazaa. Anakimbilia sehemu hiyo akiwa tayari kupigana au kwa yule mtu anayejitenga na mbuzi wake  wachanga juu ya mlima miongoni mwa hii milima au akawa anaishi kati ya moja ya mabonde. Na hapo anasimamisha Swalaah na kutoa Zakaah na kutekeleza 'Ibadah ya Rabb wake mpaka yatakapomfikia yeye umauti na wala haingilii maisha ya watu ila kwa kutaka kheri." [Muslim]

 

 

 

Share