072-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuharamishwa Kibri na Kujiona
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب تحريم الكبر والإعجاب
072-Mlango Wa Kuharamishwa Kibri na Kujiona
قَالَ الله تَعَالَى:
تِلْكَ الدَّارُ الْآخِرَةُ نَجْعَلُهَا لِلَّذِينَ لَا يُرِيدُونَ عُلُوًّا فِي الْأَرْضِ وَلَا فَسَادًا ۚ وَالْعَاقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ ﴿٨٣﴾
Hiyo ni nyumba ya Aakhirah, Tunaijaalia kwa wale wasiotaka kujitukuza katika ardhi na wala ufisadi. Na hatima njema ni kwa wenye taqwa. [Al-Qaswasw: 83]
وَلَا تَمْشِ فِي الْأَرْضِ مَرَحًا ۖ ﴿٣٧﴾
Na wala usitembee katika ardhi kwa majivuno. [Al-Israa: 37]
وَلَا تُصَعِّرْ خَدَّكَ لِلنَّاسِ وَلَا تَمْشِ فِي الْأَرْضِ مَرَحًا ۖ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخْتَالٍ فَخُورٍ ﴿١٨﴾
Na wala usiwageuzie watu uso wako kwa kiburi, na wala usitembee katika ardhi kwa maringo, hakika Allaah Hampendi kila mwenye kujivuna mwenye kujifakharisha. [Luqmaan: 18]
إِنَّ قَارُونَ كَانَ مِن قَوْمِ مُوسَىٰ فَبَغَىٰ عَلَيْهِمْ ۖ وَآتَيْنَاهُ مِنَ الْكُنُوزِ مَا إِنَّ مَفَاتِحَهُ لَتَنُوءُ بِالْعُصْبَةِ أُولِي الْقُوَّةِ إِذْ قَالَ لَهُ قَوْمُهُ لَا تَفْرَحْ ۖ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْفَرِحِينَ ﴿٧٦﴾
Hakika Qaaruwn alikuwa miongoni mwa kaumu ya Muwsaa, lakini aliwafanyia uonevu kwa kutakabari. Na Tulimpa katika hazina ambazo funguo zake zinalemea kundi la watu wenye nguvu (kuzibeba). Walipomwambia watu wake: Usifurahi kwa kujigamba. Hakika Allaah Hapendi wanaofurahi kwa kujigamba. [Al-Qaswasw: 76]
إِلَى قَوْله تَعَالَى:
فَخَسَفْنَا بِهِ وَبِدَارِهِ الْأَرْضَ ﴿٨١﴾
Basi Tukamdidimiza yeye na nyumba yake ardhini [Al-Qaswasw: 81]
Hadiyth – 1
وعن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه ، عن النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لاَ يَدْخُلُ الجَنَّةَ مَنْ كَانَ في قَلْبِهِ مِثْقَالُ ذَرَّة مِنْ كِبْرٍ ! )) فَقَالَ رَجُلٌ : إنَّ الرَّجُلَ يُحِبُّ أنْ يَكُونَ ثَوْبُهُ حَسَناً ، ونَعْلُهُ حَسَنَةً ؟ قَالَ : (( إنَّ اللهَ جَمِيلٌ يُحِبُّ الجَمَالَ ، الكِبْرُ : بَطَرُ الحَقِّ وَغَمْطُ النَّاسِ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa 'Abdillah bin Mas'uuwd (Radhwiya Alaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaah 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hataingia Peponi yeyote ambae katika moyo wake kuna chembe ya kiburi." Akasema mtu mmoja: "Hakika mtu anapenda kuwa na nguo nzuri na viatu vizuri?" Akasema: "Hakika Allaah ni mzuri na anapenda vizuri. Kiburi ni kukataa haki kwa kujiona na kuyarudisha kwa mwenyewe na kuwaona watu wengine kuwa duni." [Muslim]
Hadiyth – 2
وعن سلمة بن الأكوع رضي الله عنه : أنّ رَجُلاً أكَلَ عِنْدَ رسول الله صلى الله عليه وسلم بشمالِهِ ، فَقَالَ : (( كُلْ بيَمِينِكَ )) قَالَ : لاَ أسْتَطِيعُ ! قَالَ : (( لا اسْتَطَعْتَ )) مَا مَنَعَهُ إِلاَّ الكِبْرُ . قَالَ : فما رفَعها إِلَى فِيهِ . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Salamah bin Al-Akwa' (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: "Kuwa mtu mmoja alikula mbele ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa mkono wa kushoto. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Akasema: 'Kula kwa wa kulia.' Akasema: 'Siwezi.' Akasema: 'Hutaweza.' Hakuna kilichomzuia kufuata agizo la Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) isipokuwa kibri, hivyo hakuweza tena kuunyanyua mdomoni mwake." [Muslim]
Hadiyth – 3
وعن حارثة بن وهْبٍ رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( ألا أُخْبِرُكُمْ بأهْلِ النَّار : كلُّ عُتُلٍ جَوّاظٍ مُسْتَكْبرٍ )) متفقٌ عَلَيْهِ ، وتقدم شرحه في بابِ ضعفةِ المسلمين .
Imepokewa kutoka kwa Haarithah bin Wahb (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Je, niwaeleze nyinyi kuhusu watu wa Peponi? Kila dhaifu na mwenye kudhoofishwa. Lau ataapa kwa Allaah, Allaah atamtekelezea. Je, siwapashi habari juu ya watu wa Motoni? Ni kila mkavu, safihi na mwenye kiburi." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 4
وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه ، عن النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( احْتَجّتِ الجَنَّةُ وَالنَّارُ ، فَقَالَت النَّارُ : فيَّ الْجَبَّارُونَ والمُتَكَبِّرُونَ . وقالتِ الجَنَّةُ : فيَّ ضُعفاءُ الناس ومساكينُهُم ، فقضى اللهُ بَينهُما : إنكِ الجنّةُ رَحْمَتِي أرْحَمُ بِك مَنْ أشَاءُ ، وَإنَّكِ النَّارُ عَذَابِي أُعَذِّبُ بِكِ مَنْ أشَاءُ ، وَلِكِلَيْكُمَا عَلَيَّ مِلْؤُهَا )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Pepo na Moto zilibishana. Moto ukasema: 'Ndani yangu watakaa majabari na wenye kiburi.' Na Pepo ikasema: 'Ndani yangu watakaa madhaifu miongoni mwa watu na masikini wao.' Allaah akaamua baina yao: 'Hakika yako wewe, Pepo ni Rehema Yangu ninamrehemu kwako nimtakaye. Na hakika yako wewe, Moto ni adhabu Yangu, ninawaadhibu kwako nimtakaye, Na ni juu Yangu kuwajaza nyote wawili." [Muslim]
Hadiyth – 5
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لاَ يَنْظُرُ اللهُ يَوْمَ القِيَامَةِ إِلَى مَنْ جَرَّ إزَارَهُ بَطَراً )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaah hamwangalii siku ya Qiyaamah mwenye kuburuza kikoi chake kwa kiburi." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 6
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( ثَلاَثَةٌ لاَ يُكَلِّمُهُمُ اللهُ يَوْمَ القِيَامَة ، وَلاَ يُزَكِّيهِمْ ، وَلاَ يَنْظُرُ إلَيْهِمْ ، وَلَهُمْ عَذَابٌ ألِيمٌ : شَيْخٌ زَانٍ ، وَمَلِكٌ كَذَّابٌ ، وَعَائِلٌ مُسْتَكْبِرٌ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Watu watatu Allaah hatazungumza nao Siku ya Qiyaamah wala hatawatakasa wala hatawaangalia: Mzee mzinifu, na mfalme mwongo na fakiri mwenye kiburi." [Muslim]
Hadiyth – 7
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( قَالَ الله (عزّ وجلّ) : العِزُّ إزَاري ، والكبرياءُ رِدائي ، فَمَنْ يُنَازِعُنِي في وَاحِدٍ منهما فَقَد عَذَّبْتُهُ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Amesema Allaah ('Azza wa Jalla): Utukufu ni kikoi Changu, na kiburi ni shuka Yangu, na atakayeshindana Nami katika moja wapo ya viwili hivi Nitamuadhibu." [Muslim]
Hadiyth – 8
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( بَيْنَمَا رَجُلٌ يَمشِي في حُلَّةٍ تُعْجِبُهُ نَفْسُهُ ، مُرَجِّلٌ رَأسَهُ ، يَخْتَالُ فِي مَشْيَتهِ ، إِذْ خَسَفَ اللهُ بِهِ ، فَهُوَ يَتَجَلْجَلُ في الأَرضِ إِلَى يَوْمِ القِيَامَةِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtu akiwa anatembea katika pambo akijiona nafsini mwake. Nywele zake zimechanwa, anajivuna katika kutembe kwake. Allaah akamdidimiza ardhini, Yeye anadidimia ardhini hadi Siku ya Qiyaamah.' [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 9
وعن سَلَمةَ بنِ الأكْوَعِ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لاَ يَزَالُ الرَّجُلُ يَذْهَبُ بِنَفْسِهِ حَتَّى يُكْتَبَ في الجبَّارِين ، فَيُصيبَهُ مَا أصَابَهُمْ )) رواه الترمذي ، وقال: (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa Salamah bin Al-Akwa' (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anaendelea mtu kujitenga na watu na kuwa ni mwenye kiburi mpaka anaandikwa pamoja na wenye kiburi na hivyo kupatiwa adhabu sawa na wale wenye kiburi." [At-Tirmidhiy, na akasema hii ni Hadiyth Hasan]