073-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Tabia Njema
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب حسن الخلق
073-Mlango Wa Tabia Njema
قَالَ الله تَعَالَى:
وَإِنَّكَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِيمٍ﴿٤﴾
Na hakika wewe uko juu ya kiwango adhimu cha tabia njema. [Al-Qalam: 4]
وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ ۗ ﴿١٣٤﴾
Na wanazuia ghadhabu, na wenye kusamehe watu. [Aal-'Imraan: 134]
Hadiyth – 1
وعن أنس رضي الله عنه ، قال : كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم أحْسَنَ النَّاس خُلُقاً . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa ni mwenye tabia nzuri kuliko watu wote." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : مَا مَسِسْتُ دِيبَاجاً وَلاَ حَرِيراً ألْيَنَ مِنْ كَفِّ رسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، وَلاَ شَمَمْتُ رَائِحَةً قَطُّ أطْيَبَ مِنْ رَائِحَةِ رسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، وَلَقَدْ خدمتُ رسول اللهِ صلى الله عليه وسلم عَشْرَ سنين ، فما قَالَ لي قَطُّ : أُفٍّ، وَلاَ قَالَ لِشَيءٍ فَعَلْتُهُ : لِمَ فَعَلْتَه ؟ وَلاَ لشَيءٍ لَمْ أفعله : ألاَ فَعَلْتَ كَذا ؟ متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Sijashika dibaji wala hariri laini zaidi kuliko kiganja cha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), wala sijasikia harufu nzuri kuliko harufu ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), hakika nilimtumikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) miaka kumi, hakuniambia kabisa: 'Ah.' Na wala hakuniambia kwa kitu nilichofanya kwa nini umefanya?, Wala kwa kitu ambacho sikufanya, lau ungefanya hivi?" [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن الصعب بن جَثَّامَةَ رضي الله عنه ، قَالَ : أهديتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم حِمَاراً وَحْشِيّاً ، فَرَدَّهُ عَلَيَّ ، فَلَمَّا رأى مَا في وجهي ، قَالَ : (( إنّا لَمْ نَرُدَّهُ عَلَيْكَ إِلاَّ لأنّا حُرُمٌ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Swa'b bin Jathaamah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Nilimpatia hadiya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ya punda, naye akanirudishia. Alipoona alama ya sikitiko katika uso wangu, alisema: "Sijarudisha zawadi yako ila ni kwa sababu ya kuwa tumeshahirimia." [AL-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 4
وعن النَّوَاس بنِ سمعان رضي الله عنه ، قَالَ : سألتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم عن البِرِّ وَالإثم ، فَقَالَ : (( البِرُّ : حُسنُ الخُلقِ ، والإثمُ : مَا حاك في صدرِك ، وكَرِهْتَ أن يَطَّلِعَ عَلَيْهِ النَّاسُ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa An-Nawwaas bin sam'aan (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu wema na dhambi akasema: "Wema ni tabia nzuri, na dhambi ni iliokera nafsini mwako na ukachukia watu kuiona." [Muslim]
Hadiyth – 5
عن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما ، قَالَ : لَمْ يكن رسولُ الله صلى الله عليه وسلم فَاحِشاً وَلاَ مُتَفَحِّشاً ، وكان يَقُولُ : (( إنَّ مِنْ خِيَارِكُمْ أحْسَنَكُمْ أخْلاَقاً )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa 'Abdillah bin 'Amru bin Al-'aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: "Hakuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni mwenye kuzungumza maneno machafu wala kuyasikiliza." Na alikuwa akisema: "Hakika aliye bora miongoni mwenu ni yule mwenye tabia nzuri." [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na Ahmad].
Hadiyth – 6
وعن أَبي الدرداءِ رضي الله عنه : أن النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَا مِنْ شَيْءٍ أثْقَلُ في مِيزَانِ العبدِ المُؤْمِنِ يَوْمَ القِيَامَةِ مِنْ حُسْنِ الخُلُقِ ، وَإنَّ الله يُبْغِضُ الفَاحِشَ البَذِيَّ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Dardaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna kitu chochote kilicho kizito zaidi katika mizani ya Muumini Siku ya Qiyaamah kuliko tabia nzuri. Na hakika Allaah anamchukia mwenye kutoa maneno machafu na ya kishenzi." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh].
Hadiyth – 7
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : سُئِلَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم عَنْ أكثرِ مَا يُدْخِلُ النَّاسَ الْجَنَّةَ ؟ قَالَ : (( تَقْوَى اللهِ وَحُسنُ الخُلُقِ )) ، وَسُئِلَ عَنْ أكْثَرِ مَا يُدْخِلُ النَّاسَ النَّارَ، فَقَالَ : (( الفَمُ وَالفَرْجُ )) رواه الترمذي، وقال : (( حديث حسن صحيح )).
Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Aliulizwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa mambo ambayo yatawaingiza watu wengi Peponi?" Akasema: "Uchaji wa Allaah na tabia nzuri." Na akaulizwa kuhusu mambo ambayo yatawaingiza wengi Motoni. Akasema: "Ulimi na sehemu za siri." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh].
Hadiyth – 8
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قال: قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( أكْمَلُ المُؤمنينَ إيمَاناً أحسَنُهُمْ خُلُقاً، وَخِيَارُكُمْ خِيَارُكُمْ لِنِسَائِهِمْ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Muumini mkamilifu wa Iymaani ni mzuri wao wa tabia, na wabora wenu ni wabora wenu kwa wake zao." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 9
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : سَمِعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( إنَّ المُؤْمِنَ لَيُدْرِكُ بحُسْنِ خُلُقِه دَرَجَةَ الصَّائِمِ القَائِمِ )) رواه أَبُو داود .
Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakika Muumini anafikia kwa tabia nzuri daraja ya mfungaji mwenye kusimama usiku." [Abu Daawuud]
Hadiyth – 10
وعن أَبي أُمَامَة الباهِليِّ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( أنَا زَعِيمٌ ببَيتٍ في ربَض الجَنَّةِ لِمَنْ تَرَكَ المِرَاءَ ، وَإنْ كَانَ مُحِقّاً ، وَبِبَيْتٍ في وَسَطِ الجَنَّةِ لِمَنْ تَرَكَ الكَذِبَ ، وَإنْ كَانَ مَازِحاً ، وَبِبَيْتٍ في أعلَى الجَنَّةِ لِمَنْ حَسُنَ خُلُقُهُ )) . حديث صحيح ، رواه أَبُو داود بإسناد صحيح .
Imepokewa kutoka kwa Abu Umamah Al-Baahiliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mimi ni mdhamini wa nyumba ya chini Peponi kwa mwenye kuacha kujionesha japo ana haki. Na nyumba ya katikati ya Peponi, kwa mwenye kuacha uongo, japokuwa kwa kufanya mzaha. Na kwa nyumba iliyo sehemu ya juu kabisa Peponi kwa mwenye tabia nzuri." [Hadiyth Swahiyh, Abu Daawuud kwa Isnaad Swahiyh]
Hadiyth – 11
وعن جابر رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إنَّ مِنْ أحَبِّكُمْ إليَّ ، وَأقْرَبِكُمْ مِنِّي مَجْلِساً يَوْمَ القِيَامَةِ ، أحَاسِنَكُم أخْلاَقاً ، وَإنَّ أبْغَضَكُمْ إلَيَّ وَأبْعَدَكُمْ مِنِّي يَوْمَ القِيَامَةِ ، الثَّرْثَارُونَ وَالمُتَشَدِّقُونَ وَالمُتَفَيْهقُونَ )) قالوا : يَا رسول الله ، قَدْ عَلِمْنَا (( الثَّرْثَارُونَ وَالمُتَشَدِّقُونَ )) ، فمَا المُتَفَيْهقُونَ ؟ قَالَ : (( المُتَكَبِّرُونَ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika wapendwa wenu zaidi kwangu, na wakaribu wenu zaidi wa kukaa nami Siku Ya Qiyaamah, ni wazuri wenu zaidi wa tabia. Na wabughudhiwa wenu zaidi wenu zaidi kwangu Siku ya Qiyaamah ni wale ma-tharthar (wenye kuzungumza sana) na mutashaddiquun (wanaorefusha mazungumzo yao na wanazungumza kwa kujaza midomo yao kwa majisifu) na mutafayhiquun." Wakasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Hakika tunawajua ma-tharthar na mutashaddiquun lakini hawa mutafayhiquun ni kina nani?" Akasema: "Wenya kiburi." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]