03-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Huruma Na Upole Wake: Mpole Hata Kwa Adui Zake Walipotoa Maamkizi Ya Maangamizi Kwa Waislaam

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Huruma Na Upole Wake:

 

03-Mpole Hata Kwa Adui Zake

Walipotoa Maamkizi Ya Maangamizi Kwa Waislaam

 

Alhidaaya.com

 

 

Makafiri walipowaamkia Waislamu kwa maamkizi ya kuwakusudia maangamizi, ‘Aaishah (ضي الله عنها) aliwarudishia maamkizi ya maangamizi na laana juu yao, lakini Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakupendelea kuwarudishia waziwazi bali alitumia hikma kutokana na upole wake:

 

حَدَّثَنَا أَبُو الْيَمَانِ، أَخْبَرَنَا شُعَيْبٌ، عَنِ الزُّهْرِيِّ، قَالَ أَخْبَرَنِي عُرْوَةُ، أَنَّ عَائِشَةَ رضى الله عنها قَالَتْ دَخَلَ رَهْطٌ مِنَ الْيَهُودِ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالُوا السَّامُ عَلَيْكَ‏.‏ فَفَهِمْتُهَا فَقُلْتُ عَلَيْكُمُ السَّامُ وَاللَّعْنَةُ‏.‏ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ مَهْلاً يَا عَائِشَةُ، فَإِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الرِّفْقَ فِي الأَمْرِ كُلِّهِ ‏"‏‏.‏ فَقُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ أَوَلَمْ تَسْمَعْ مَا قَالُوا قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ فَقَدْ قُلْتُ وَعَلَيْكُمْ ‏"‏‏.‏

Amesimulia ‘Urwah kuwa ‘Aaishah (ضي الله عنها) amesema: Liliingia kundi la Mayahudi kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) wakasema:

السَّامُ عَلَيْكَ

Assaamu ‘alayka (mauti yawe juu yake)”.

 

Nikafahamu wanakusudia nini, nami nikawajibu:

عَلَيْكُمُ السَّامُ وَاللَّعْنَةُ

Alaykumus-saamu wa al-la‘nah (juu yenu kifo na laana)”.

 

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaniambia: “Taratibu ee ‘Aaishah! Hakika Allaah Anapenda upole katika kila jambo”. Nikasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Kwani hukuwasikia walivyosema?” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hakika tayari nishawaambia

وَعَلَيْكُمْ

Wa ‘Alaykum (iwe juu yenu)’”. [Al-Bukhaariy]

 

Share