081-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kuomba Uongozi na Kuchagua
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب النهي عن سؤال الإمارة واختيار ترك الولايات إذا لَمْ يتعين عليه أَوْ تَدْعُ حاجة إِلَيْهِ
081-Mlango Wa Kukatazwa Kuomba Uongozi na Kuchagua
قَالَ الله تَعَالَى:
تِلْكَ الدَّارُ الْآخِرَةُ نَجْعَلُهَا لِلَّذِينَ لَا يُرِيدُونَ عُلُوًّا فِي الْأَرْضِ وَلَا فَسَادًا ۚ وَالْعَاقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ ﴿٨٣﴾
Hiyo ni nyumba ya Aakhirah, Tunaijaalia kwa wale wasiotaka kujitukuza katika ardhi na wala ufisadi. Na hatima njema ni kwa wenye taqwa. [Al-Qaswasw: 83]
Hadiyth – 1
وعن أَبي سعيدٍ عبدِ الرحمانِ بن سَمُرَة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ لي رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( يَا عَبْدَ الرَّحمان بن سَمُرَةَ ، لاَ تَسْأَلِ الإمَارَةَ ؛ فَإنّكَ إن أُعْطِيتَهَا عَنْ غَيْرِ مَسْألَةٍ أُعِنْتَ عَلَيْهَا ، وَإنْ أُعْطِيتَهَا عَنْ مَسْألَةٍ وُكِلْتَ إِلَيْهَا ، وَإِذَا حَلَفْتَ عَلَى يَمِينٍ ، فَرَأيْتَ غَيْرَهَا خَيْراً مِنْهَا ، فَأتِ الَّذِي هُوَ خَيْرٌ وَكَفِّرْ عَنْ يَمِينكَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd 'Abdir-Rahmaan bin Samurah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Aliniambia mimi Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ee 'Abdir-Rahmaan bin Samurah! Usiombe uongozi, hakika kama utapewa bila kuuomba utasaidiwa juu yake, na ukipewa kwa kuuomba utatelekezwa nao, na ukiapa juu ya yamini na ukaona vinginevyo ni bora basi lete ambalo ni kheri na toa kafara la yamini yako." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, At-Tirmidhiy, An-Nasai na Ahmad].
Hadiyth – 2
وعن أَبي ذرٍّ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( يَا أَبَا ذَرٍّ ، إنِّي أرَاكَ ضَعِيفاً ، وَإنِّي أُحِبُّ لَكَ مَا أُحِبُّ لِنَفْسِي . لاَ تَأمَّرَنَّ عَلَى اثْنَيْنِ ، وَلاَ تَوَلَّيَنَّ مَالَ يَتِيمٍ )) رواه مسلم .
Toka kwa Abu Dharr amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia: "Ee Aba Dharr! Hakika mimi nakuona udhaifu, Hakika mimi nakupendelea nipendelealo nafsi yangu. Usitake uongozi hata kuongoza watu wawili wala usisimamie mali ya yatima." [Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أَبي ذرٍّ رضي الله عنه ، قَالَ : قُلْتُ : يَا رسول الله ، ألا تَسْتَعْمِلُني ؟ فَضَرَبَ بِيَدِهِ عَلَى مَنْكِبي ، ثُمَّ قَالَ : (( يَا أَبَا ذَرٍّ ، إنَّكَ ضَعِيفٌ ، وإنّها أمانةٌ ، وَإنَّهَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ خِزْيٌ وَنَدَامَةٌ ، إِلاَّ مَنْ أخَذَهَا بِحَقِّهَا ، وَأدَّى الَّذِي عَلَيْهِ فِيهَا )) رواه مسلم .
Toka kwa Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): Kwa nini hunipi uongozi? Akanipiga Kofi kwa mkono wake mabega yangu, kisha akasema: "Ee Abu Dharr! Hakika wewe ni dhaifu, na hiyo ni amana, nao Siku ya Qiyaamah ni hizaya na majuto, ila mwenye kuuchukua kwa haki yake, na akatekeleza yanayo pasa ndani yake." [Muslim]
Hadiyth – 4
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إنَّكُمْ سَتَحْرِصُونَ عَلَى الإمَارَةِ ، وَسَتَكونُ نَدَامَةً يَوْمَ القِيَامَةِ )) رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu)kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika nyinyi mutakuwa munapupia uongozi na utakuwa juu yenu Siku ya Qiyaamah ni majuto." [Al-Bukhaariy]