082-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuhimizwa Viongozi, Maqdhi na Wengineo Kuchagua Washauri na Mawaziri Wazuri na Wema na Kuonywa Kuwa na Marafiki Wabaya na Kuwakubali

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب حث السلطان والقاضي وغيرهما من ولاة الأمور عَلَى اتخاذ وزير صالح وتحذيرهم من قرناء السوء والقبول منهم

082-Mlango Wa Kuhimizwa Viongozi, Maqdhi na Wengineo Kuchagua Washauri na Mawaziri Wazuri na Wema na Kuonywa Kuwa na Marafiki Wabaya na Kuwakubali

 

Alhidaaya.com

 

قَالَ الله تَعَالَى:

الْأَخِلَّاءُ يَوْمَئِذٍ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ إِلَّا الْمُتَّقِينَ﴿٦٧﴾

Marafiki wapenzi Siku hiyo watakuwa maadui wao kwa wao isipokuwa wenye taqwa. [Az-Zukhruf: 67]

 

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي سعيدٍ وأبي هريرة رضي الله عنهما : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  مَا بَعَثَ اللهُ مِنْ نَبِيٍّ ، وَلاَ اسْتَخْلَفَ مِنْ خَليفَةٍ إِلاَّ كَانَتْ لَهُ بِطَانَتَانِ : بِطَانَةٌ تَأمُرُهُ بالمَعْرُوفِ وتَحُضُّهُ عَلَيْهِ ، وَبِطَانَةٌ تَأمُرُهُ بالشَّرِّ وَتَحُضُّهُ عَلَيْهِ ، وَالمَعْصُومُ مَنْ عَصَمَ اللهُ ))رواه البخاري .

Kutoka kwa Abu Sa'iyd na Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaah hakumtuma Nabiy yeyote wala hakumchagua Khalifa isipokuwa walikuwa na washauri wawili, mmoja alikuwa akimuamrisha mema na akimhimiza kwayo na mwengine akimuamrisha shari na kumhimiza kwayo. Na mtu asiyekuwa na hatia ni yule anayehifadhiwa na Allaah kutofanya madhambi." [Al-Bukhaariy].

 

 

Hadiyth – 2

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : ((  إِذَا أرَادَ اللهُ بِالأَمِيرِ خَيْراً ، جَعَلَ لَهُ وَزِيرَ صدقٍ ، إنْ نَسِيَ ذَكَّرَهُ ، وَإنْ ذَكَرَ أعَانَهُ ، وَإِذَا أرَادَ بِهِ غَيْرَ ذَلِكَ جَعَلَ لَهُ وَزِيرَ سُوءٍ ، إنْ نَسِيَ لَمْ يُذَكِّرْهُ ، وَإنْ ذَكَرَ لَمْ يُعِنْهُ )) رواه أَبُو داود بإسنادٍ جيدٍ عَلَى شرط مسلم .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaah anapoktakia kheri kiongozi, anamjalia yeye waziri mkweli (mzuri) ambaye anamkumbusha anaposahau na anapokumbuka basi humsaidia. Na anapomtakia kinyume na hilo (yaani shari), anamjaalia waziri mbaya ambaye hamkumbushi anaposahau na anapokumbuka basi hamsaidii." [Abuu-Daawuud, na Isnaad yake ni Jayd (nzuri) kwa sharti ya Muslim].

 

 

 

Share