Sharbati Ya Embe Maziwa Na Mtindi
Sharbati Ya Embe Maziwa Na Mtindi
Vipimo
Maembe yaliyoiva - 2
Mtindi (yogurt) - 2 Vikombe vya chai
Maziwa mazito (Condensed Milk) - kikopo 1
Barafu - 12 vipande
Arki au rose essence - matone
Namna Ya Kutayarisha
- Menya maembe kisha ukate kate vipande.
- Weka vipimo vyote isipokuwa kwenye mashine ya kusagia (blender).
- Saga hadi ilainike.
- Mimina kwenye gilasi sharbati iko tayari
Bis-swihhah wal-hanaa (kunywa kwa siha na kuburudika)
