Juisi Ya Embe Na Karakara/Pasheni (Passion Fruit)
Juisi Ya Embe Na Karakara/Pasheni
Vipimo
Passion fruit - 8
Embe - 6 za kiasi
Maji - kiasi
Sukari - kiasi upendavyo
Namna Ya Kutyarisha
- Kata passion fruit toa nyama weka mashine ya kusagia (blender) . Tia maji kiasi kisha saga na uchuje .
- Saga embe na maji kidogo kisha changanya na juisi ya passion.
- Tia sukari korogo ikiwa tayari.
