Al-Lajnah Ad-Daaimah: Akipiga Chafya Katika Swalaah Aseme AlhamduliLLaah?
Akipiga Chafya Katika Swalaah Aseme AlhamduliLLaah?
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Nikipiga chafya wakati nipo kwenye Swalaah Je, inafaa kusema Alhamdulillah au laa?
JIBU:
Yeyote ataepiga chafya ilihali yuko katika Swalaah, anatakiwa amshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na aseme: “AlhamduliLLaah”; ikiwa ni Swalaah ya fardhi ama ya Sunnah, na ndivyo walivyosema Jumhuwr ya Swahaba na Taabi’iyn, na akasema hivyo pia Imaam Maalik, Imaam Shafi’iy, na Imaam Ahmad, wakiwa na khilafu kati yao kuwa je, aseme kwa siri ama adhihirishe? Lililo sahihi kwenye kauli mbili za ‘Ulamaa, na madh-hab ya Imaam Ahmad, kwamba atadhihirisha sauti, lakini iwe kiasi cha kuisikilizisha nafsi yake tu ili asiwashawishi wanaoswali. Hilo linajumuisha ujumla wa Hadiyth aliyoipokea Abuu Hurayrah (Radhwiya Allahu Anhu) amehadithia:
عن ابي هريرة رضي الله عنه عَنْ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {إِذَا عَطَسَ أَحَدُكُمْ فَلْيَقُلْ: اَلْحَمْدُ لِلَّهِ - أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Akipiga chafya mmoja wenu aseme:
اَلْحَمْدُ لِلَّهِ
Alhamdulillaah [Al-Bukhaariy]
[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah Lil-Buhuwth Al-'Ilmiyyah Wal-Iftaa [Fatwa (26/114 -1-)]