Imaam Ibn Baaz: Kutumia Jina La Ibn Siynaa Haijuzu Kutokana Na ‘Aqiydah Yake Isiyo Sahihi
Kutumia Jina La Ibn Siynaa Haijuzu Kutokana Na ‘Aqiydah Yake Isiyo Sahihi
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema
“Haitakikani kwa Waislaamu kuiita sehemu yeyote ile kwa majina ya Ibn Siynaa–Alfaraabiy (Qabbahahu Allaah).
Amesema Ibn Taymiyah (Rahimahu Allaah): Ibn Siynaa alikuwa na ‘Aqiydah (itikadi) ya Ushia akiwatukana Swahaba (Radhwiya Allaahu Anhum), na kuwapunguzia heshima yao.
[Imaam Ibn Baaz: Alfawaaidul-Jaaliyah]