25-Du’aa Toka Kwenye Qur-aan Tukufu Na Sharh Yake: Maghfirah Na Rahmah

Du’aa Toka Kwenye Qur-aan Tukufu

 

Na Sharh Yake

 

Alhidaaya.com

 

25-Maghfirah Na Rahmah

 

 

 

" رَّبِّ اغْفِرْ وَارْحَمْ وَأَنتَ خَيْرُ الرَّاحِمِينَ "

 

 

Rabb wangu! Ghufuria na Rehemu, Nawe Ni Mbora wa wenye kurehemu”. [Al-Muuminuwn: (118)].

 

Allaah Ta’aalaa Amemwamuru Nabiy Wake Muhammad (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuomba du’aa hii.  Amemwamuru aombe maghfirah na rahmah. Mambo haya mawili yamekariri kwenye du’aa nyingi zilizopo ndani ya Qur-aan kutokana na umuhimu wake.  Nabiy ameamuriwa ayaombe mawili hayo pamoja na kuwa amesamehewa madhambi yake yaliyopita na yajayo, basi je sisi itakuwaje?

 

Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na sisi tumeamuriwa kuomba du’aa hii kutokana na faida yake kubwa duniani na aakhirah.  Na ndio maana Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamfundisha Abu Bakr As-Swiddiyq (Radhwiya Allaah ‘anhu) mfano wa du’aa hii.  Abu Bakr alimwambia Rasuli: “Nifundishe du’aa ya kuomba katika Swalah yangu.  Rasuli akamwambia sema:

 

"اللَّهُمَّ إِنِّي ظَلَمْتُ نَفْسِي ظُلْمًا كَثِيرًا، وَلَا يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا أَنْتَ، فَاغْفِرْ لِي مَغْفِرَةً مِنْ عِنْدِكَ، وَارْحَمْنِي، إِنَّك أَنْتَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ"

 

“Ee Allaah! Hakika mimi nimeidhulumu nafsi yangu dhulma nyingi, na hakuna yeyote anayeghufuria madhambi isipokuwa Wewe tu.  Basi Nighufurie mimi maghfirah itokayo Kwako na Unirehemu.  Hakika Wewe Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwingi wa Kurehemu”.  [Al-Bukhaariy:  Kitaabul Aadhaan]

 

 

Faida kutokana na du’aa hii:

 

 

1-  Du’aa hii ni muhimu mno kwa kuwa Rasuli kaamriwa na Allaah Mtukufu kuiomba.

 

2-   Umuhimu wa kutawassal kwa Jina la Rabbu.

 

3-  Mwombaji aanze kuomba maghfirah kwanza kabla ya rahmah.  Maghfirah ni ufunguo wa rahmah.

 

 

 

Share