010-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Kilichochinjwa Kwa Ajili Ya Asiye Allaah
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Vyakula Vilivyoharamishwa Na Kitabu Cha Allaah
Kilichochinjwa Kwa Ajili Ya Asiye Allaah
5- Kilichochinjwa Kwa Ajili Ya Asiye Allaah
Ni kama sanamu, au kiumbe, au kaburi, au maiti kama vile Sayyid Badawiy (Misri) au vinginevyo katika “matwaaghuwtw” (kila kiabudiachwo badala ya Allaah kama watu waliojivika uungu, mashaytwaan na kadhalika).
Na hii ni kwa Neno Lake Ta’aalaa:
"وَمَا ذُبِحَ عَلَى النُّصُبِ"
“Na waliochinjwa kwa ajili ya ‘ibaadah ya waabudiwa”. [Al-Maaidah: 03].