013-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Kila Ndege Mwenye Kucha

 

 

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا

 

 Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi

 

Alhidaaya.com

 

Vyakula Vilivyoharamishwa Na Hadiyth Za Rasuli 

 

Kila Ndege Mwenye Kucha (Ndege Wawindaji Wenye Kujeruhi Na Kuua)

 

 

 

3-  Kila Ndege Mwenye Kucha (Ndege Wawindaji Wenye Kujeruhi Na Kuua)

 

 

Ni kama kozi, kipanga, mwewe, na mfano wao.  Ni kwa Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas iliyotangulia:

 

"أَنَّ النَّبِيَ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَهَى عَنْ كُلِّ ذِيْ مِخْلَبٍ مِنَ الطَّيْرِ"

 

“Kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kila ndege mwenye makucha”.   [Hadiyth Swahiyh.  Imetajwa nyuma kidogo].

 

Muradi wa makucha hapa ni yale anayowindia, kwa kuwa ni maarufu kwa Waarabu kwamba hawamuiti “Mwenye Makucha” kwao isipokuwa yule mwenye kuwinda kwa kutumia makucha yake tu.  Ama jogoo, njiwa na ndege wengineo wasiowinda kwa kutumia makucha, hao hawaitwi “Wenye Makucha” katika Lugha ya Kiarabu, kwa kuwa makucha yao ni ya kujishikilia uzani wa mwili na kuchakuria, na si kwa kuwindia au kuulia.

 

Jumhuwr ya ‘Ulamaa - kinyume na Maalik!! – wamesema ni haramu kila ndege mwenye makucha (ya kuwindia, kujeruhia na kuulia).

 

 

 

Share