005-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kuchukua Hadiyth, Maneno ya Watu na Kuyapeleka kwa Viongozi Ikiwa Hapana Haja Yoyote Kama Hofu ya Ufisadi na Mfano Wake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب النهي عن نقل الحديث وكلام الناس

إِلَى ولاة الأمور إِذَا لَمْ تَدْعُ إِلَيْهِ حاجة كخوف مفسدة ونحوه

005-Mlango Wa Kukatazwa Kuchukua Hadiyth, Maneno ya Watu na Kuyapeleka kwa Viongozi Ikiwa Hapana Haja Yoyote Kama Hofu ya Ufisadi na Mfano Wake

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ ۚ  ﴿٢﴾

Na shirikianeni katika wema na taqwa, na wala msishirikiane katika dhambi na uadui. [Al-Maaidah: 2]

 

وعن ابن مسعودٍ رضي اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( لا يُبَلِّغُنِي أَحَدٌ مِنْ أصْحَابِي عَنْ أَحَدٍ شَيْئاً ، فإنِّي أُحِبُّ أنْ أخْرُجَ إِلَيْكُمْ وأنَا سَليمُ الصَّدْرِ )) . رواه أَبُو داود والترمذي .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: " Asinifikishie Swahaaba wangu yeyote jambo baya lolote kuhusu mtu mwengine, kwani mimi napenda kukutana nanyi kifua changu kikiwa safi kabisa (bila ya kuwa na kinyongo na yeyote)." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]

 

 

Share