004-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuharamishwa Umbeya, Nako ni Kueneza Maneno Baina ya Watu kwa Njia ya Kuleta Ufisadi
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب تحريم النميمة
وهي نقل الكلام بَيْنَ الناس عَلَى جهة الإفساد
004-Mlango Wa Kuharamishwa Umbeya, Nako ni Kueneza Maneno Baina ya Watu kwa Njia ya Kuleta Ufisadi
قال الله تَعَالَى :
هَمَّازٍ مَّشَّاءٍ بِنَمِيمٍ﴿١١﴾
Mwingi wa kukashifu, mpitaji huku na kule kwa kufitinisha. [Al-Qalam: 11]
مَّا يَلْفِظُ مِن قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ﴿١٨﴾
Hatamki kauli yeyote isipokuwa anaye mchungaji aliyejitayarisha (kurekodi). [Qaaf: 18]
Hadiyth – 1
وعن حُذَيْفَةَ رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( لا يَدْخُلُ الجَنَّةَ نَمَّامٌ )).متفق عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Hudhayfah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hataingia Peponi mmbeya (mwenezaji uvumi / msingiziaji) [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]
Hadiyth – 2
وعن ابن عباسٍ رضي الله عنهما : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم مرَّ بِقَبْرَيْنِ فَقَالَ : (( إنَّهُمَا يُعَذَّبَانِ ، وَمَا يُعَذَّبَانِ في كَبيرٍ ! بَلَى إنَّهُ كَبِيرٌ : أمَّا أَحَدُهُمَا ، فَكَانَ يَمْشِي بِالنَّمِيمَةِ ، وأمَّا الآخَرُ فَكَانَ لاَ يَسْتَتِرُ مِنْ بَوْلِهِ )) . متفق عَلَيْهِ . وهذا لفظ إحدى روايات البخاري .
Amesimulia Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliyapitia makaburi mawili na akasema: “Hakika hawa wawili wanaadhibiwa, na wala hawaadhibiwi kwa sababu ya jambo kubwa (la kuwashinda kulitekeleza au kujiepusha nalo).” Kisha hapo hapo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ”Hapana! Bali ni kubwa (dhambi kubwa na adhabu zake)! Ama mmoja wao, huyu alikuwa akipita kufitinisha watu, na ama mwingine, huyu alikuwa hajikingi na mkojo wake [anapokojoa].” [Al-Bukhaariy na Muslim]" [Al-Bukhaariy na Muslim, na hili tamshi ni moja ya riwaayah za Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 3
وعن ابن مسعود رضي الله عنه : أن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( أَلاَ أُنَبِّئُكُمْ مَا العَضْهُ ؟ هي النَّمَيمَةُ ؛ القَالَةُ بَيْنَ النَّاسِ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Je, niwajulishe nyinyi 'Adhhu ni nini? Huo ni uongo na kuzungusha maneno baina ya watu." [Muslim]