009-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuhimiza Kuthibitisha kwa Anayosema

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب الحثّ عَلَى التثبت فيما يقوله ويحكيه

009-Mlango Wa Kuhimiza Kuthibitisha kwa Anayosema

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

وَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۚ  ﴿٣٦﴾

Na wala usifuate usiyo na elimu nayo. [Al-Israa: 36]

مَّا يَلْفِظُ مِن قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ﴿١٨﴾

Hatamki kauli yeyote isipokuwa anaye mchungaji aliyejitayarisha (kurekodi). [Qaaf: 18]

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( كَفَى بالمَرْءِ كَذِباً أنْ يُحَدِّثَ بِكُلِّ مَا سَمِعَ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Inatosha kwa mtu kuwa muongo kwa kuhadithia (bila kuchunguza) kila analolisikia." [Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن سَمُرَةَ رضي اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ حَدَّثَ عَنِّي بِحَديثٍ يَرَى أَنَّهُ كَذِبٌ فَهُوَ أَحَدُ الكَاذِبينَ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwake Samurah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kunizuilia mimi Hadiyth ambayo anajua wazi kuwa ni uongo, basi yeye ni miongoni mwa waongo." [Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن أسماء رَضِيَ اللهُ عنها : أنَّ امْرأةً قالت : يَا رسولَ الله ، إنَّ لِي ضَرَّةً فهل عَلَيَّ جُنَاحٌ إنْ تَشَبَّعْتُ مِنْ زَوْجِي غَيْرَ الَّذِي يُعْطِيني ؟ فَقَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( المُتَشَبِّعُ بِما لَمْ يُعْطَ كَلاَبِسِ ثَوْبَيْ زُورٍ )) . متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwake Asmaa (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba wakati mmoja alikuja mwanamke na kuuliza: "Ee Rasuli wa Allaah! Hakika mimi nina mke mwenza. Je, ninaruhusiwa kumwambia mke mwenza kuwa mume wangu amenipatia kitu ambacho hakunipatia?" Akasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Mwenye kudai kuwa amepatiwa kitu na kumbe hajapatiwa ni kama anayevaa mavazi mawili ya uongo." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share