010-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuharamishwa Ushuhuda wa Uwongo
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب بيان غلظ تحريم شهادة الزُّور
010-Mlango Wa Kuharamishwa Ushuhuda wa Uwongo
قال الله تَعَالَى :
وَاجْتَنِبُوا قَوْلَ الزُّورِ ﴿٣٠﴾
Na jiepusheni na kauli za uongo. [Al-Hajj: 30]
وَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۚ ﴿٣٦﴾
Na wala usifuate usiyo na elimu nayo. [Al-Israa: 36]
مَّا يَلْفِظُ مِن قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ﴿١٨﴾
Hatamki kauli yeyote isipokuwa anaye mchungaji aliyejitayarisha (kurekodi). [Qaaf: 18]
إِنَّ رَبَّكَ لَبِالْمِرْصَادِ ﴿١٤﴾
Hakika Rabb wako bila shaka Yu tayari Anaziona nyenendo zao zote. [Al-Fajr: 14]
وَالَّذِينَ لَا يَشْهَدُونَ الزُّورَ ﴿٧٢﴾
Na wale ambao hawashuhudii uongo. [Al-Furqaan: 72]
وعن أَبي بَكْرَةَ رضي اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( ألاَ أُنَبِّئُكُمْ بِأكْبَرِ الكَبَائِرِ ؟ )) قُلْنَا : بَلَى يَا رسولَ اللهِ . قَالَ : (( الإشْراكُ باللهِ ، وعُقُوقُ الوَالِدَيْنِ )) وكَانَ مُتَّكِئاً فَجَلَسَ ، فَقَالَ : (( ألا وَقولُ الزُّورِ )) فما زال يُكَرِّرُهَا حَتَّى قلنا : لَيْتَهُ سَكَتَ . متفق عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Bakrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Je, niwajulishe nyinyi madhambi makubwa kuliko yote?" Tukasema: "Kwa nini tusitake, ee Rasuli wa Allaah." Akasema: "Kumshirikisha Allaah na kuwaasi wazazi wawili." Akakaa sawa baada ya kuwa ameegemea mto, akasema: "Jiepusheni na kauli ya urongo." Na kutoa ushahidi wa uongo aliendelea kuirudia kauli hiyo mpaka tukasema afadhali angelinyamaza." [Al-Bukhaariy na Muslim]