015-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kuudhi
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب النهي عن الإيذاء
015-Mlango Wa Kukatazwa Kuudhi
قال الله تَعَالَى :
وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ بِغَيْرِ مَا اكْتَسَبُوا فَقَدِ احْتَمَلُوا بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا ﴿٥٨﴾
Na wale wanaowaudhi Waumini wa kiume na Waumini wa kike bila ya kuwa wamechuma kosa, basi kwa yakini wamejibebea usingiziaji mkuu wa dhulma na dhambi bayana. [Al-Ahzaab: 58]
Hadiyth – 1
وعن عبدِ الله بن عمرو بن العاصِ رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( المُسْلِمُ مَنْ سَلِمَ المُسْلِمُونَ مِنْ لِسَانِهِ وَيَدِهِ ، والمُهَاجِرُ مَنْ هَجَرَ مَا نَهَى اللهُ عَنْهُ )) . متفق عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwake 'Abdillaah bin 'Amruw bin Al-'Asa (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Muislamu mzuri (na wa sawa) ni yule ambaye Waislamu wengine wanasalimika na shari za ulimi wake na mkono wake na Muhaajir ni yule anayeyahama yale aliyomkataza Allaah." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن عبدِ الله بن عمرو بن العاصِ رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ أحَبَّ أنْ يُزَحْزَحَ عَنِ النَّارِ ، ويُدْخَلَ الجَنَّةَ ، فَلْتَأْتِهِ مَنِيَّتُهُ وَهُوَ يُؤْمِنُ بِاللهِ وَاليَومِ الآخِرِ ، وَلْيَأْتِ إِلَى النَّاسِ الَّذِي يُحِبُّ أنْ يُؤْتَى إِلَيْهِ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Amruw bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anayependwa kulindwa na kuepushwa na Moto na kuingizwa Peponi, anatakiwa akutane na kifo akiwa anamuamini Allaah na Siku ya Mwisho, na aamiliane na watu kwa njia ambayo yeye anapenda watu waamiliane naye." [Muslim]. Hii ni sehemu ya Hadiyth ndefu ambayo tumetangulia kuitaja katika mlango "Wajibu wa Kuwatii Viongozi."