016-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kubughudhiana na Kukatana na Kupeana Nyongo
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب النهي عن التباغض والتقاطع والتدابر
016-Mlango Wa Kukatazwa Kubughudhiana na Kukatana na Kupeana Nyongo
قال الله تَعَالَى :
إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ ﴿١٠﴾
Hakika Waumini ni ndugu [Al-Hujuraat: 10]
أَذِلَّةٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ ﴿٥٤﴾
Wanyenyekevu kwa Waumini, washupavu juu ya makafiri [Al-Maaidah: 45]
مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّـهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ ۖ ﴿٢٩﴾
Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni Rasuli wa Allaah. Na wale walio pamoja naye ni wakali zaidi dhidi ya makafiri wanahurumiana baina yao. [Al-Fat-h: 29]
Hadiyth – 1
وعن أنس رضي اللهُ عنه : أنَّ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( لاَ تَبَاغَضُوا ، وَلاَ تَحَاسَدُوا ، وَلاَ تَدَابَرُوا ، وَلاَ تَقَاطَعُوا ، وَكُونُوا عِبَادَ اللهِ إخْوَاناً ، وَلاَ يَحِلُّ لِمُسْلِمٍ أنْ يَهْجُرَ أخَاهُ فَوْقَ ثَلاَثٍ )). متفق عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Msichukiane wala msihusudiane, wala msipeane nyongo, wala msikate uhusiano, lakini kuweni enyi waja wa Allaah ndugu. Na haifai kwa Muislamu kuhama nduguye zaidi ya siku tatu." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( تُفْتَحُ أبْوابُ الجَنَّةِ يَوْمَ الإثْنَيْنِ ويَوْمَ الخَمْيِسِ ، فَيُغْفَرُ لِكُلِّ عَبْدٍ لا يُشْرِكُ بِاللهِ شَيْئاً ، إِلاَّ رَجُلاً كَانَتْ بينهُ وَبَيْنَ أخِيهِ شَحْناءُ فَيُقَالُ : أنْظِرُوا هَذَيْنِ حَتَّى يَصْطَلِحَا ! أَنْظِرُوا هَذَينِ حَتَّى يَصْطَلِحَا ! )) . رواه مسلم .
وفي روايةٍ لَهُ : (( تُعْرَضُ الأعْمالُ في كُلِّ يَوْمِ خَمِيسٍ وإثْنَيْن )) وذَكَرَ نَحْوَهُ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Milango ya Pepo hufunguliwa siku ya Jumatatu na Alkhamisi, hivyo kusamehewa kila mja asiyemshirikisha Allaah na kitu chochote isipokuwa mtu ambaye ana uadui (utesi) baina yake na nduguye. Atasema: 'Waacheni hawa wawili mpaka wafanye mapatano baina yao!' [Muslim].
Na katika riwaayah yake nyengine: "Huonyeshwa amali kila siku ya Jumatatu na Alkhamisi", na akataja mfano wa hiyo riwaayah ya mwanzo.