017-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Hasadi
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب تحريم الحسد
017-Mlango Wa Kukatazwa Hasadi
قال الله تَعَالَى :
أَمْ يَحْسُدُونَ النَّاسَ عَلَىٰ مَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ ۖ ﴿٥٤﴾
Au wanawahusudu watu (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم na Waumini) kwa yale Aliyowapa Allaah katika Fadhila Zake? [An-Nisaa: 54]
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه: أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( إيَّاكُمْ وَالحَسَدَ ؛ فَإنَّ الحَسَدَ يَأكُلُ الحَسَنَاتِ كَمَا تَأكُلُ النَّارُ الحَطَبَ )) أَوْ قَالَ : (( العُشْبَ )) . رواه أَبُو داود .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Tahadharini hasadi, kwani hasadi hula hasanati (amali njema) kama moto unavyokula kuni." au alisema: "Majani/malisho." [Abuu Daawuwd]