019-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kuwa na Dhana Mbaya kwa Waislamu Bila ya Dharura
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب النهي عن سوء الظنّ بالمسلمين من غير ضرورة
019-Mlango Wa Kukatazwa Kuwa na Dhana Mbaya kwa Waislamu Bila ya Dharura
قال الله تَعَالَى :
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اجْتَنِبُوا كَثِيرًا مِّنَ الظَّنِّ إِنَّ بَعْضَ الظَّنِّ إِثْمٌ ۖ ﴿١٢﴾
Enyi walioamini! Jiepusheni sana na dhana, kwani hakika baadhi ya dhana ni dhambi. [Al-Hujuraat: 12]
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( إيَّاكُمْ والظَّنَّ ، فإنَّ الظَّنَّ أكْذَبُ الحَدِيثِ )) . متفق عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Tahadharini na dhana, kwani dhana ni uwongo mkubwa katika mazungumzo." [Al-Bukhaariy na Muslim].