020-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kuwadharau Waislamu

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب تحريم احتقار المسلمين

020-Mlango Wa Kukatazwa Kuwadharau Waislamu

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَسْخَرْ قَوْمٌ مِّن قَوْمٍ عَسَىٰ أَن يَكُونُوا خَيْرًا مِّنْهُمْ وَلَا نِسَاءٌ مِّن نِّسَاءٍ عَسَىٰ أَن يَكُنَّ خَيْرًا مِّنْهُنَّ ۖ وَلَا تَلْمِزُوا أَنفُسَكُمْ وَلَا تَنَابَزُوا بِالْأَلْقَابِ ۖ بِئْسَ الِاسْمُ الْفُسُوقُ بَعْدَ الْإِيمَانِ ۚ وَمَن لَّمْ يَتُبْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ﴿١١﴾

Enyi walioamini! Wanaume wasiwafanyie dhihaka na kuwadharau wanaume wengineo asaa wakawa bora kuliko wao, wala wanawake kwa wanawake wengineo, asaa wakawa bora kuliko wao. Na wala msifedheheshane kwa kutukanana, na wala msiitane majina (mabaya) ya utani. Ubaya ulioje kuita jina la ufasiki baada ya Iymaan! Na yeyote asiyetubu, basi hao ndio madhalimu. [Al-Hujuraat: 11]

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( بِحَسْبِ امْرِئٍ مِنَ الشَّرِّ أنْ يَحْقِرَ أَخَاهُ المُسْلِمَ )) . رواه مسلم ، وَقَدْ سبق قريباً بطوله .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Inatosha kwa mtu kuwa ni miongoni mwa watu wanaofanya shari kwa kumdharau ndugu yake Muislamu." [Muslim], na imetajwa karibuni kwa urefu.

 

Hadiyth – 2

وعن ابن مسعودٍ رضي الله عنه ، عن النبيّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لا يَدْخُلُ الجَنَّةَ مَنْ كَانَ فِي قَلْبِهِ مِثْقَالُ ذَرَّةٍ مِنْ كِبْرٍ ! )) فَقَالَ رَجُلٌ : إنَّ الرَّجُلَ يُحِبُّ أَنْ يَكُونَ ثَوْبُهُ حَسَناً ، وَنَعْلُهُ حَسَنةً ، فَقَالَ : (( إنَّ اللهَ جَمِيلٌ يُحِبُّ الجَمَالَ ، الكِبْرُ : بَطَرُ الحَقِّ ، وَغَمْطُ النَّاسِ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwake 'Abdillaah bin Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hataingia Peponi yeyote mwenye katika moyo wake chembe ya kiburi." Akasema mtu mmoja: "Hakika mtu anapenda kuwa na nguo nzuri na viatu vizuri?" Akasema: "Hakika Allaah ni Mzuri na anapenda vizuri. Kiburi ni kukataa haki na kudharau watu." [Muslim].

 

Hadiyth – 3

وعن جُندب بن عبدِ الله رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( قَالَ رَجُلٌ : وَاللهِ لا يَغْفِرُ اللهُ لِفُلانٍ ، فَقَالَ اللهُ عزوجل : مَنْ ذا الَّذِي يَتَأَلَّى عَلَيَّ أنْ لا أغْفِرَ لِفُلانٍ ! فَإنِّي قَدْ غَفَرْتُ لَهُ ، وَاحْبَطْتُ عَمَلَكَ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwake Jundub bin 'Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtu mmoja alisema: Wa-Allaahi (Naapa kwa Allaah)! Allaah Hatamsamehe fulani." Allaah 'Azza wa Jalla akasema: "Ni mtu gani huyu anayeapa kwa jina Langu kuwa sitamsamehe fulani. Hakika Mimi nimemsamehe na Nimebatilisha amali yako." [Muslim]

 

Share