021-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa kufurahi kwa Baya Linalomkumba Muislamu
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب النهي عن إظهار الشماتة بِالمُسْلِم
021-Mlango Wa Kukatazwa kufurahi kwa Baya Linalomkumba Muislamu
قال الله تَعَالَى :
إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ ﴿١٠﴾
Hakika Waumini ni ndugu [Al-Hujuraat: 10]
إِنَّ الَّذِينَ يُحِبُّونَ أَن تَشِيعَ الْفَاحِشَةُ فِي الَّذِينَ آمَنُوا لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۚ ﴿١٩﴾
Hakika wale wanaopenda uenee uchafu wa kashfa kwa wale walioamini, watapata adhabu iumizayo duniani na Aakhirah. [An-Nuwr: 19]
وعَن وَائِلَةَ بن الأسقع رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لا تُظْهِرِ الشَّمَاتَةَ لأَخِيكَ فَيَرْحَمَهُ اللهُ وَيَبْتَلِيكَ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa Waathilah bin Al-Asqa' (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Usifurahi kwa msiba alioupata nduguyo hivyo Allaah Akamrehemu na akakutia wewe katika mtihani." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]