022-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kukashifu (Kutusi) Nasaba

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب تحريم الطعن في الأنساب الثابتة في ظاهر الشرع

022-Mlango Wa Kukatazwa Kukashifu (Kutusi) Nasaba

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ بِغَيْرِ مَا اكْتَسَبُوا فَقَدِ احْتَمَلُوا بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا ﴿٥٨﴾

Na wale wanaowaudhi Waumini wa kiume na Waumini wa kike bila ya kuwa wamechuma kosa, basi kwa yakini wamejibebea usingiziaji mkuu wa dhulma na dhambi bayana. [Al-Ahzaab: 58]

 

 

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( اثْنَتَان في النَّاسِ هُمَا بهم كُفْرٌ : الطَّعْنُ فِي النَّسَبِ ، وَالنِّيَاحَةُ عَلَى المَيِّتِ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mambo mawili wanayoyafanya watu ni katika matendo ya ukafiri: Kukashifu na kutusi ukoo wa mtu na kuomboleza maiti." [Muslim]

 

 

 

 

Share