031-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuharamishwa kwa Mtu Mwenye Uwezo Kukataa Kulipa Deni
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب تحريم مطل الغني بحقٍّ طلبه صاحبه
031-Mlango Wa Kuharamishwa kwa Mtu Mwenye Uwezo Kukataa Kulipa Deni
قال الله تَعَالَى :
إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَىٰ أَهْلِهَا ﴿٥٨﴾
Hakika Allaah Anakuamrisheni kurudisha amana kwa wenyewe. [An-Nisaa: 58]
فَإِنْ أَمِنَ بَعْضُكُم بَعْضًا فَلْيُؤَدِّ الَّذِي اؤْتُمِنَ أَمَانَتَهُ ﴿٢٨٣﴾
Na ikiwa mmoja wenu amewekewa amana na mwengine, basi airudishe yule ambaye ameaminiwa amana ya mwenzake [Al-Baqarah: 283]
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( مَطْلُ الغَنِيِّ ظُلْمٌ، وَإِذَا أُتْبعَ أَحَدُكُمْ عَلَى مَلِيءٍ فَلْيَتْبَع )) . متفق عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Haifai kwa tajiri kukwepa kulipa deni, ni dhulma. Na mmoja wenu atakaposhawishiwa kwa mwenye uwezo, basi na akubali." [Al-Bukhaariy na Muslim].