032-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Karaha ya Kurudisha Hiba (Zawadi) Ambayo Bado Hajaikabidhi kwa Mwenye Kupewa, na Hiba Aliyompa Mtoto Wake na Akaipokea au Hata Kama Hakuipokea, Karaha ya Kununua Kitu Alichokitoa Swadaqah kutoka kwa Aliyempa Swadaqah
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب كراهة عود الإنسان في هبة لَمْ يُسلِّمها
إِلَى الموهوب لَهُ وفي هبة وهبها لولده وسلمها أَوْ لَمْ يسلمها
وكراهة شرائه شَيْئاً تصدّق بِهِ من الَّذِي تصدق عَلَيْهِ
أَوْ أخرجه عن زكاة أَوْ كفارة ونحوها
وَلاَ بأس بشرائه من شخص آخر قَدْ انتقل إِلَيْهِ
032-Mlango Wa Karaha ya Kurudisha Hiba (Zawadi) Ambayo Bado Hajaikabidhi kwa Mwenye Kupewa, na Hiba Aliyompa Mtoto Wake na Akaipokea au Hata Kama Hakuipokea, Karaha ya Kununua Kitu Alichokitoa Swadaqah kutoka kwa Aliyempa Swadaqah au Zakaa au Kafara na Mfano Wake, Wala Hakuna Ubaya Kuinunua Kutoka kwa Mtu Mwingine Ambae Imehamia Kwake
Hadiyth – 1
وعن ابن عباس رضي الله عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( الَّذِي يَعُودُ في هِبَتِهِ كَالكَلْبِ يَرْجِعُ في قَيْئِهِ )) . متفق عَلَيْهِ .
وفي رواية : (( مَثَلُ الَّذِي يَرْجِعُ في صَدَقَتِهِ ، كَمَثَلِ الكَلْبِ يَقِيءُ ، ثُمَّ يَعُودُ في قَيْئِهِ فَيَأكُلُهُ )) .
وفي روايةٍ : (( العائِدُ في هِبَتِهِ كالعائِدِ في قَيْئِهِ )) .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuirudia zawadi yake ni kama mbwa aliyekula matapishi yake." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy]
Na katika riwaayah nyengine: "Mfano wa mwenye kurudia swadaqah yake ni kama mfano wa mbwa anaye tapika, kisha akayarudia matapishi yake na kuyala."
Na katika riwaayah: "Mwenye kuirudia zawadi ni kama mwenye kuyarudia matapishi yake."
Hadiyth – 2
وعن عمر بن الخطاب رضي الله عنه قَالَ : حَمَلْتُ عَلَى فَرَسٍ في سَبيلِ اللهِ فَأَضَاعَهُ الَّذِي كَانَ عِندَهُ ، فَأَرَدْتُ أن أشْتَرِيَهُ ، وَظَنَنْتُ أنَّهُ يَبِيعُهُ بِرُخْصٍ ، فَسَأَلْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : (( لاَ تَشْتَرِهِ وَلاَ تَعُدْ فِي صَدَقَتِكَ وإنْ أعْطَاكَهُ بِدِرْهَمٍ ؛ فَإنَّ العَائِدَ في صَدَقَتِهِ كَالعَائِدِ في قَيْئِهِ )) . متفق عَلَيْهِ .
Amesema 'Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nilimtoa farasi wangu swadaqah kwa ajili ya Jihadi katika njia ya Allaah, lakini yule niliyempatia alikuwa hamtizami vyema, hivyo nikafikiria kumnunua kutoka kwake na nikadhania kuwa angemuuza kwa bei nafuu. Nikamuuliza Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu jambo hilo, naye akaniambia: "Usimnunue na wala usiirudie swadaqah yako hata kama atakupa kwa dirhamu moja, kwani bila shaka anyeirudia swadaqah yake ni sawa na aliyeyarudia matapishi yake." [Al-Bukhaariy na Muslim]