033-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uharamu wa Kula Mali ya Yatima
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب تأكيد تحريم مال اليتيم
033-Mlango Wa Uharamu wa Kula Mali ya Yatima
قال الله تَعَالَى :
إِنَّ الَّذِينَ يَأْكُلُونَ أَمْوَالَ الْيَتَامَىٰ ظُلْمًا إِنَّمَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ نَارًا ۖ وَسَيَصْلَوْنَ سَعِيرًا ﴿١٠﴾
Hakika wale wanaokula mali ya mayatima kwa dhulma hapana shaka kwamba wanakula katika matumbo yao moto, na watauingia moto uliowashwa vikali mno. [An-Nisaa: 10]
وَلَا تَقْرَبُوا مَالَ الْيَتِيمِ إِلَّا بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ ﴿١٥٢﴾
Na wala msiikaribie mali ya yatima isipokuwa kwa njia njema ya manufaa [Al-An'aam: 152]
وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْيَتَامَىٰ ۖ قُلْ إِصْلَاحٌ لَّهُمْ خَيْرٌ ۖ وَإِن تُخَالِطُوهُمْ فَإِخْوَانُكُمْ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ الْمُفْسِدَ مِنَ الْمُصْلِحِ ۚ ﴿٢٢٠﴾
Na wanakuuliza kuhusu mayatima. Sema: Kuwatengenezea (ya kuwafaa) ni kheri zaidi. Na mkichanganya mambo yenu na yao basi hao ni ndugu zenu. Na Allaah Anamjua fisadi na mtengenezaji. [Al-Baqarah: 220]
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( اجْتَنِبُوا السَّبْعَ المُوبِقَاتِ ! )) قالُوا : يَا رَسُولَ اللهِ ، وَمَا هُنَّ ؟ قَالَ : (( الشِّرْكُ باللهِ ، والسِّحْرُ ، وَقَتْلُ النَّفْسِ الَّتي حَرَّمَ اللهُ إِلاَّ بالحَقِّ ، وأكلُ الرِّبَا ، وأكْلُ مَالِ اليَتِيمِ ، والتَّوَلِّي يَوْمَ الزَّحْفِ ، وقَذْفُ المُحْصَنَاتِ المُؤْمِنَاتِ الغَافِلاَتِ )) . متفق عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Jiepusheni na madhambi saba yanayoangamiza." Watu wakauliza: "Ee Rasuli wa Allaah ni yepi hayo?" Akasema: "Kumshirikisha Allaah, na uchawi, na kuua nafsi ambayo Allaah Ameiharamisha isipokuwa kwa haki, na kula riba, kula mali ya yatima, kukimbia siku ya vita na kuwatuhumu kwa zinaa wanawake waliohifadhiwa na Allaah, Waumini wasiyo na habari ya zinaa." [Al-Bukhaariy na Muslim]