034-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ukubwa wa uharamu wa Riba
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب تغليظ تحريم الربا
034-Mlango Wa Ukubwa wa uharamu wa Riba
قال الله تَعَالَى :
الَّذِينَ يَأْكُلُونَ الرِّبَا لَا يَقُومُونَ إِلَّا كَمَا يَقُومُ الَّذِي يَتَخَبَّطُهُ الشَّيْطَانُ مِنَ الْمَسِّ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا إِنَّمَا الْبَيْعُ مِثْلُ الرِّبَا ۗ وَأَحَلَّ اللَّـهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا ۚ فَمَن جَاءَهُ مَوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّهِ فَانتَهَىٰ فَلَهُ مَا سَلَفَ وَأَمْرُهُ إِلَى اللَّـهِ ۖ وَمَنْ عَادَ فَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٧٥﴾
Wale wanaokula riba hawatosimama (Siku ya Qiyaamah) ila kama anavyosimama yule aliyezugwa na shaytwaan kwa kuguswa na kupatwa. Hivyo kwa sababu wao wamesema: Hakika biashara ni kama riba. Na Allaah Amehalalisha biashara na Ameharamisha riba. Na atakayefikiwa na mawaidha kutoka kwa Rabb wake akakoma, basi ni yake yale yaliyopita, na hukumu yake iko kwa Allaah. Na atakayerudia basi hao ni watu wa motoni, wao humo ni wenye kudumu.
يَمْحَقُ اللَّـهُ الرِّبَا وَيُرْبِي الصَّدَقَاتِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ ﴿٢٧٦﴾
Allaah Huifuta baraka (mali ya) riba na Huzibariki swadaqah. Na Allaah Hampendi kila aliye mwingi wa kukufuru apapiae madhambi.
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ لَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ﴿٢٧٧﴾
Hakika wale walioamini na wakatenda mema na wakasimamisha Swalaah na wakatoa Zakaah, (hao) watapata ujira wao kutoka kwa Rabb wao, na wala hakuna khofu juu yao na wala wao hawatohuzunika.
Enyi walioamini! Mcheni Allaah na acheni yaliyobakia katika riba ikiwa nyinyi ni Waumini. [Al-Baqarah: 275-278]
وعن ابن مسعود رضي الله عنه قَالَ: لَعَنَ رسول الله صلى الله عليه وسلم آكِلَ الرِّبَا وَمُوكِلَهُ . رواهُ مسلم ، زاد الترمذي وغيره : وَشَاهِدَيْهِ وَكَاتِبَهُ .
Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Amemlani mwenye kula riba na mwenye kumuwakilisha. [Muslim]. Na akaongeza At-Tirmidhiy na wengineo na mashahidi wake na muadhishi wake.