037-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uharamu wa Kumwangalia Mwanamke wa Kando na Mvulana Mzuri Bila Haja ya Kisheria

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب تحريم النظر إِلَى المرأة الأجنبية والأمرد الحسن

لغير حاجة شرعية

037-Mlango Wa Uharamu wa Kumwangalia Mwanamke wa Kando na Mvulana Mzuri Bila Haja ya Kisheria

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

قُل لِّلْمُؤْمِنِينَ يَغُضُّوا مِنْ أَبْصَارِهِمْ ﴿٣٠﴾

Waambie Waumini wanaume wainamishe macho yao [An-Nuwr: 30]

إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَـٰئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْئُولًا ﴿٣٦﴾

Hakika masikio na macho na moyo; vyote hivyo vitaulizwa. [Al-Israa: 36]

يَعْلَمُ خَائِنَةَ الْأَعْيُنِ وَمَا تُخْفِي الصُّدُورُ﴿١٩﴾

(Allaah) Anajua khiyana za macho na yale yanayoficha vifua. [Ghaafir: 19]

إِنَّ رَبَّكَ لَبِالْمِرْصَادِ ﴿١٤﴾

Hakika Rabb wako bila shaka Yu tayari Anaziona nyenendo zao zote. [Al-Fajr: 14]

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( كُتِبَ عَلَى ابْن آدَمَ نَصِيبُهُ مِنَ الزِّنَا مُدْرِكُ ذَلِكَ لا مَحَالَةَ : العَيْنَانِ زِنَاهُمَا النَّظَرُ ، وَالأُذُنَانِ زِنَاهُمَا الاسْتِمَاعُ ، وَاللِّسَانُ زِناهُ الكَلاَمُ ، وَاليَدُ زِنَاهَا البَطْشُ ، وَالرِّجْلُ زِنَاهَا الخُطَا ، والقَلْبُ يَهْوَى وَيَتَمَنَّى ، وَيُصَدِّقُ ذَلِكَ الفَرْجُ أَوْ يُكَذِّبُهُ )) . متفق عَلَيْهِ . هَذَا لفظ مسلمٍ ، ورواية البخاري مختصرَةٌ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kwamba: "Binaadamu huandikiwa sehemu yake ya zinaa, hilo humpata bila ya matatizo: Macho mawili zinaa yao ni kuangalia; na masikio mawili zinaa yao ni kusikia; na ulimi zinaa yake ni mazungumzo; na mkono zinaa yake ni kushika (yaliyo haramu); na mguu zinaa yake ni kutembea (kuyaendelea yaliyo haramu); na moyo nao hutamani, na husadikisha hayo utupu wake au hukataa (kuyaendea)." [Al-Bukhaariy na Muslim, na hii ni tamishi la Muslim. Na Al-Bukhaariy ameipokea kwa muhtasari]. 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي سعيد الخُدريِّ رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إيّاكُمْ والجُلُوس فِي الطُّرُقَاتِ ! )) قالوا : يَا رسولَ الله ، مَا لَنَا مِنْ مَجَالِسِنَا بُدٌّ ، نَتَحَدَّثُ فِيهَا . فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( فَإذَا أبَيْتُمْ إِلاَّ المَجْلِسَ ، فَأَعْطُوا الطَّرِيقَ حَقَّهُ )) قَالُوا : وَمَا حَقُّ الطَّريقِ يَا رسولَ اللهِ ؟ قَالَ : (( غَضُّ البَصَرِ ، وَكَفُّ الأَذَى ، وَرَدُّ السَّلاَمِ ، والأمرُ بالمَعْرُوفِ ، والنَّهيُ عنِ المُنْكَرِ ))  متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nawatahadharisha nyinyi katika kukaa kwenu njiani." Wakasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Je, ikiwa hapana budi kukaa (katika sehemu hizo) kwani tunazungumza na kujadiliana ndani yake." Wakauliza: Rasuli wa Allaah: " Ikiwa ni hivyo basi ipatieni njia yake." Akawaambia: "Na haki za njia ni zipi ee Rasuli wa Allaah?" Akasema: "Kuinamisha macho chini, na kuondoa uchafu (pingamizi), na kurudisha salamu, na kuamrisha mema na kukataza maovu." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي طلحة زيد بن سهل رضي الله عنه قَالَ : كُنَّا قُعُوداً بالأفْنِيَةِ نَتَحَدَّثُ فِيهَا فَجَاءَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم فَقَامَ عَلَيْنَا ، فَقَالَ : (( مَا لَكُمْ وَلِمَجَالسِ الصُّعُدَاتِ ؟ اجْتَنِبُوا مَجَالِسَ الصُّعُدَاتِ )) فقُلْنَا : إنَّمَا قَعَدْنَا لِغَيْرِ مَا بَأسٍ ، قَعَدْنَا نَتَذَاكَرُ ، وَنَتَحَدَّثُ . قَالَ : (( إمَّا لاَ فَأَدُّوا حَقَّهَا : غَضُّ البَصَرِ ، وَرَدُّ السَّلاَمِ ، وَحُسْنُ الكَلاَمِ )) . رواه مسلم .

Kutoka kwa Abu Twalha Zayd bin Sahl (Radhwiya Allaahu 'anhu): Tulikuwa tumekaa na huku tunazungumza kwenye baraza mara Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaja na kusimama mbele yetu. Akauliza: "MUna nini nyinyi mbona munakaa kwenye njia? Jiepusheni na vikao vya barabarani." Tukasema: "Hakika sisi tumekaa kwa mambo yasiyo na matatizo na kwa nia nzuri. Tumekaa tunakumbuka na kuzungumza." Akasema: "Ikiwa hamuna budi mpaka mukae katika sehemu hizo basi ipatieni barabara haki yake: Kuinamisha macho chini, na kurudisha salamu, na kuzungumza maneno mazuri." [Muslim]

 

Hadiyth – 4

وعن جرير رضي الله عنه قَالَ : سألت رسول الله صلى الله عليه وسلم عن نَظَرِ الفَجْأَةِ فَقَالَ : (( اصْرِفْ بَصَرَكَ )) . رواه مسلم .

Amesema Jariyr (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu kumtizama mwanamke kwa bahati mbaya (bila ya kukusudia)? Akasema: "Geuza macho yako (upande mwingine)." [Muslim]

 

Hadiyth – 5

وعن أُم سَلَمَة رَضِيَ اللهُ عنها ، قالت : كنتُ عِنْدَ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، وعندهُ مَيْمُونَة ، فَأقْبَلَ ابنُ أُمِّ مَكْتُومٍ ، وَذَلِكَ بَعْدَ أنْ أُمِرْنَا بِالحِجَابِ فَقَالَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( احْتَجِبَا مِنْهُ )) فَقُلْنَا : يَا رسولَ اللهِ ، ألَيْسَ هُوَ أعْمَى ! لاَ يُبْصِرُنَا ، وَلاَ يَعْرِفُنَا ؟ فَقَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( أفَعَمْيَاوَانِ أنتُما أَلَسْتُمَا تُبْصِرَانِهِ !؟ )) . رواه أَبُو داود والترمذي، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Amesema Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Nilikuwa na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na Maymunah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) na mara akaingia Ibn Maktuwm. Tukio hili lilitokea baada ya kuwa tumeamriwa kuvaa hijabu. Akasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Jifinikeni kutokana naye." Tukasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Je, yeye si ni kipofu, hatuoni sisi wala hatujui?" Akasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Nanyi pia ni vipofu. Je, nyinyi hamumuoni?" [Abu Daawuwd an At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

Hadiyth – 6

وعن أَبي سعيد رَضِيَ اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لاَ يَنْظُرُ الرَّجُلُ إِلَى عَوْرَةِ الرَّجُلِ ، وَلاَ المَرْأَةُ إِلَى عَوْرَةِ المَرْأَةِ ، وَلاَ يُفْضِي الرَّجُلُ إِلَى الرَّجُلِ في ثَوْبٍ وَاحِدٍ ، وَلاَ تُفْضي المَرْأةُ إِلَى المَرْأَةِ في الثَّوْبِ الواحِدِ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Asiangalie mwanaume utupu wa mwanaume mwenziwe, wala mwanamke utupu wa mwanamke mwenziwe. Asijifunike mwanaume katika shuka moja na mwanaume mwenziwe wala mwanamke asijifunike na mwanamke mwenziwe ndani ya shuka moja." [Muslim]

 

 

 

Share