043-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uharamu wa Kuunganisha Nywele, Kuchanjwa na Kujaliza Meno
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب تحريم وصل الشعر والوشم
والوشر وهو تحديد الأسنان
043-Mlango Wa Uharamu wa Kuunganisha Nywele, Kuchanjwa na Kujaliza Meno
قال الله تَعَالَى :
إِن يَدْعُونَ مِن دُونِهِ إِلَّا إِنَاثًا وَإِن يَدْعُونَ إِلَّا شَيْطَانًا مَّرِيدًا ﴿١١٧﴾
Hawaombi badala Yake isipokuwa miungu ya kike na hawaombi isipokuwa shaytwaan muasi.
لَّعَنَهُ اللَّـهُ ۘ وَقَالَ لَأَتَّخِذَنَّ مِنْ عِبَادِكَ نَصِيبًا مَّفْرُوضًا ﴿١١٨﴾
Allaah Amemlaani. Na (shaytwaan) akasema: Kwa hakika nitashika katika waja Wako sehemu maalumu.
وَلَأُضِلَّنَّهُمْ وَلَأُمَنِّيَنَّهُمْ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُبَتِّكُنَّ آذَانَ الْأَنْعَامِ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلْقَ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَتَّخِذِ الشَّيْطَانَ وَلِيًّا مِّن دُونِ اللَّـهِ فَقَدْ خَسِرَ خُسْرَانًا مُّبِينًا ﴿١١٩﴾
Na hakika nitawapoteza, na nitawashawishi matamanio ya kulaghai, na nitawaamrisha. Basi watakata masikio ya wanyama (wawatukuze), na nitawaamrisha watabadili Uumbaji wa Allaah. Na atakayemfanya shaytwaan kuwa rafiki mwandani badala ya Allaah basi kwa yakini amekhasirika khasara bayana. [An-Nisaa: 117-119]
Hadiyth – 1
وعن أسماءَ رضي الله عنها : أنَّ امْرَأَةً سَأَلَتِ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَتْ : يا رسولَ اللهِ إنَّ ابْنَتِي أصَابَتْهَا الحَصْبَةُ ، فَتَمَرَّقَ شَعْرُهَا ، وإنّي زَوَّجْتُهَا ، أفَأَصِلُ فِيهِ ؟ فقالَ : (( لَعَنَ اللهُ الوَاصِلَةَ وَالمَوْصُولَةَ )) . متفق عليه .
وفي روايةٍ : (( الوَاصِلَةَ ، والمُسْتوْصِلَةَ )) .
Imepokewa kutoka kwa Asmaa (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba mwanamke fulani alimuuliza Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ee Rasuli wa Allaah! Binti yangu amepatwa na surua zikapuputika nywele zake, nami nimemuozesha; Je, niziunganishe?" Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamjibu: "Allaah Amemlaani mwenye kuunganisha nywele zake (au nywele za mwengine kwa nywele nyengine) na mwenye kuungwa (au kuvaa nywele hizo)." [Al-Bukhaariy, Muslim na An-Nasaaiy]
Na katika riwaayah nyengine: "Mwenye kuunganisha nywele na mwenye kumtaka mwengine amfanyie kazi hiyo (mwenye kutamani kuzivaa nywele hizo za bandia)."
Hadiyth – 2
وعن حُميدِ بنِ عبد الرحْمانِ : أنَّهُ سَمِعَ مُعَاوِيَةَ رضي الله عنه ، عامَ حَجَّ على المِنْبَرِ وَتَنَاوَلَ قُصَّةً مِنْ شَعْرٍ كَانَتْ في يَدِ حَرَسِيٍّ فَقَالَ : يَا أهْلَ المَدِينَةِ أيْنَ عُلَمَاؤُكُمْ ؟! سَمِعتُ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم ، يَنْهَى عَنْ مِثْلِ هذِهِ ، ويقُولُ : (( إنَّمَا هَلَكَتْ بَنُوإسْرَائِيلَ حينَ اتَّخَذَهَا نِسَاؤُهُمْ )) . متفق عليه .
Imepokewa kutoka kwa Humayd bin 'Abdur-Rahmaan kuwa alimsikia Mu'awiyah (Radhwiya Allaahu 'anhu), mwaka wa Hijjah, akiwa juu ya mimbari, akiwa ameshika nywele zilizokatwa katika mikono ya Harasiy (mtoto wa Amiri), akasema: "Enyi watu wa Madiynah! Wako wapi wanazuoni wenu? Nimemsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akikataza tabia hii (nywele za bandia) na alikuwa akisema: 'Hakika walihiliki Bani Israiyl pale wake zao walipo ichukua tabia hii (ya kuunganisha nywele).' [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy]
Hadiyth – 3
وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم لَعَنَ الوَاصِلَةَ والمُسْتَوْصِلَةَ ، والوَاشِمَةَ والمُسْتَوشِمَةَ . متفق عليه .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amemlaani mwenye kuunganisha nywele zake na mwenye kutaka mwengine amuunganishe nywele hizo na mchanjaji kwenye mwili na mwenye kuchanjwa. [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy].
Hadiyth – 4
وعن ابن مسعود رضي الله عنه قال : لَعَنَ اللهُ الوَاشِمَاتِ والمُسْتَوشِمَاتِ وَالمُتَنَمِّصَاتِ ، والمُتَفَلِّجَاتِ لِلْحُسْنِ ، المُغَيِّرَاتِ خَلْقَ الله ، فَقَالَتْ لَهُ امْرَأَةٌ في ذَلِكَ فَقَالَ : وَمَا لِي لاَ ألْعَنُ مَنْ لَعَنَهُ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، وَهُوَ فِي كِتَابِ اللهِ ؟ قالَ اللهُ تعالى : [ وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانْتَهُوا ] [ سورة الحشر : 7 ] . متفق عليه .
Amesema Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu): Allaah Amewalaani wenye kuchanja, na wenye kuchanjwa, na wenye kunyoa nyusi, na wenye kuchonga meno kwa urembo, na wenye kubadilisha umbile la Allaah. Akamuuliza yeye mwanamke kuhusu jambo hilo. Akamjibu kwa kusema: "Kwa nini nisimlaani yule aliyelaaniwa na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na aliyelaaniwa katika Kitabu cha Allaah. Amesema Allaah Ta'aalaa: 'Na lolote analokupeni Rasuli basi lichukueni, na analokukatazeni, basi jiepusheni' [Al-Hashr: 7]." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nisaaiy]