044-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kung'oa Mvi Kwenye Ndevu, Kichwa na Sehemu Nyengineyo na Kunyoa Ndevu kwa Kijana

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب النهي عن نتف الشيب من اللحية

والرأس وغيرهما ، وعن نتف الأمرد شعر لحيته عند أول طلوعه

044-Mlango Wa Kukatazwa Kung'oa Mvi Kwenye Ndevu, Kichwa na Sehemu Nyengineyo na Kunyoa Ndevu kwa Kijana

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن عمرو بن شعيب ، عن أبيهِ ، عن جَدِّهِ رضي الله عنه ، عن النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قال : (( لاَ تَنْتِفُوا الشَّيْبَ ؛ فَإنَّهُ نُورُ المُسْلِمِ يَوْمَ القِيَامَةِ )) حديث حسن ، رواه أبو داود، والترمذي، والنسائي بأسانيد حسنة ، قال الترمذي : (( هو حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa 'Amruw bin Shu'ayb kutoka kwa babake kutoka kwa babu yake (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Musing'oe mvi kwani hizo ni nuru ya Musliamu Siku ya Qiyaamah." [Hadiyth Hasan iliyopokewa na Abu Daawuwd, na At-Tirmidhiy, na An-Nasaaiy kwa Isnaad zilizo Hasan (nzuri). Na amesema At-Tirmidhiy kuwa hii ni Hadiyth Hasan]

 

Hadiyth – 2

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ عَمِلَ عَمَلاً لَيْسَ علَيْهِ أمْرُنَا فَهُوَ رَدٌّ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kufanya amali isiyokuwa na hukumu yetu, itakataliwa." [Muslim]

 

 

Share