045-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Karaha ya Kustanji kwa Mkono wa Kulia na Kuishika Dhakari Yake kwa Mkono wa Kulia Bila Udhuru

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب كراهة الاستنجاء باليمين

ومس الفرج باليمين من غير عذر

045-Mlango Wa Karaha ya Kustanji kwa Mkono wa Kulia na Kuishika Dhakari Yake kwa Mkono wa Kulia Bila Udhuru

 

Alhidaaya.com

 

وعن أبي قتادة رضي الله عنه ، عن النبيّ صلى الله عليه وسلم ، قال : (( إذا بَالَ أَحَدُكُمْ ، فَلاَ يَأخُذَنَّ ذَكَرَهُ بِيَمِينِهِ ، وَلاَ يَسْتَنْجِ بِيَمِينِهِ ، وَلاَ يَتَنَفَّسْ فِي الإنَاءِ )) . متفق عليه .

Imepokewa kutoka kwa Abu Qataadah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapokojoa mmoja wenu asiishike dhakari yake kwa mkono wake wa kuume na asistanji kwa mkono wake wa kuume wala asipumue katika chombo (anapokunywa kinywaji)." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy].

 

 

Share