047-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kuacha Moto katika Nyumba Wakati wa Kulala na Mfano Wake Kama Taa
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب النهي عن ترك النار في البيت عند النوم
ونحوه سواء كانت في سراج أو غيره
047-Mlango Wa Kukatazwa Kuacha Moto katika Nyumba Wakati wa Kulala na Mfano Wake Kama Taa
Hadiyth – 1
عن ابن عمر رضي الله عنهما ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قال : (( لاَ تَتْرُكُوا النَّارَ فِي بُيُوتِكُمْ حِينَ تَنَامُونَ )) . متفق عليه .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Musiache moto katika nyumba zenu wakati munapolala." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أبي موسى الأشعري رضي الله عنه ، قال : احْتَرَقَ بَيْتٌ بالمَدِينَةِ عَلَى أهْلِهِ مِنَ اللَّيْلِ ، فَلَمَّا حُدِّثَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم بِشَأنِهِم ، قالَ : (( إنَّ هذِهِ النَّارَ عَدُوٌّ لَكُمْ ، فَإذا نِمْتُمْ ، فَأطْفِئُوهَا )) متفق عليه .
Imepokewa kutoka kwa Abu Muwsaa Al-Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: "IIiungua nyumba moja Madiynah juu ya wenyewe usiku mmoja. Alipoelezewa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu jambo hilo alisema: 'Hakika huu m oto ni adui kwenu, hivyo mukienda kulala uzimeni'." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن جابر رضي الله عنه ، عن رسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، قال : (( غَطُّوا الإنَاءَ ، وَأَوْكِئُوا السِّقَاءَ ، وَأَغْلِقُوا الأَبْوَابَ . وَأطْفِئُوا السِّرَاجَ ، فإنَّ الشَّيْطَانَ لاَ يَحُلُّ سِقَاءً ، وَلاَ يَفْتَحُ بَاباً ، وَلاَ يَكْشِفُ إنَاءً . فإنْ لَمْ يَجِدْ أَحَدُكُمْ إلاَّ أنْ يَعْرُضَ عَلَى إنَائِهِ عُوداً ، وَيَذْكُرَ اسْمَ اللهِ ، فَلْيَفْعَل ، فإنَّ الفُوَيْسِقَةَ تُضْرِمُ عَلَى أهْلِ البَيْتِ بَيْتَهُمْ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Finikeni vyombo vyenu, na fungeni viriba vya kuekea maji, na fungeni milango, na zimeni taa kwa sababu shetani hafunui viriba vilivyo fungwa wala hafungui milango wala hafungui vyombo vilivyo finikwa. Ikiwa mmoja wenu hatapata cha kufinikia vyombo isipokuwa kuweka kijiti juu ya chombo au kutaja jina la Allaah, afanye hivyo. Huenda wakati mwengine panya akaangusha kandili (taa au koroboi) na hivyo kuchoma nyumba watu wake wakiwa ndani." [Muslim].