048-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Takilifu, Nayo ni Kufanya Kitendo na Kusema Maneno Ambayo Hayana Maslahi na Ndani yake Yapo Mashaka
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب النهي عن التكلف
وهو فعل وقول ما لا مصلحة فيه بمشقة
048-Mlango Wa Kukatazwa Takilifu, Nayo ni Kufanya Kitendo na Kusema Maneno Ambayo Hayana Maslahi na Ndani yake Yapo Mashaka
قال الله تَعَالَى :
قُلْ مَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُتَكَلِّفِينَ ﴿٨٦﴾
Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Sikuombeni ujira wowote juu ya hili, na wala mimi si miongoni mwa wenye kujidai kuzusha chochote kisichohusu. [Swaad: 86]
Hadiyth – 1
وعن عمر رضي الله عنه قال : نُهِينَا عَنِ التَّكَلُّفِ . رواه البخاري .
Amesema 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu): Tumekatazwa kupindukia (kuzidisha katika mambo). [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 2
وعن مسروقٍ ، قال : دَخَلْنَا على عبدِ اللهِ بْنِ مَسعُودٍ رضي الله عنه فقال : يا أَيُّهَا النَّاسُ ، مَنْ عَلِمَ شَيْئاً فَلْيَقُلْ بِهِ ، وَمَنْ لَمْ يَعْلَمْ ، فَلْيَقُلْ : اللهُ أعْلَمُ ، فَإنَّ مِنَ العِلْمِ أَنْ يَقُولَ لِمَا لاَ يَعْلَمُ : اللهُ أعْلَمُ . قالَ اللهُ تَعَالَى لِنَبِيِّهِ صلى الله عليه وسلم : [ قُلْ مَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُتَكَلِّفِينَ ] . رواه البخاري .
Amesema Masruwq: Tulimzuru 'Abdillaah bin Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) siku moja, naye akatuambia: "Enyi watu! Mwenye kujua kitu chochote, anaweza kuzungumza kukihusu hicho. Na asiyehua, basi aseme: Allaah Anajua, kwani ni katika ujuzi wa elimu kusema kwa asiyejua: Allaah Anajua zaidi. Hakika Allaah Ta'aalaa Alimwambia Nabiy Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Sikuombeni ujira wowote juu ya hili, na wala mimi si miongoni mwa wenye kujidai kuzusha chochote kisichohusu. [Swaad: 86]." [Al-Bukhaariy]