049-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uharamu Kuomboleza Maiti kwa Kujipiga Mashavu, Kuchana Nguo, Kung'oa Nywele, Kunyoa na Kujiombea Maangamivu
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب تحريم النياحة على الميت ولطم الخد وشق الجيب
ونتف الشعر وحلقه والدعاء بالويل والثبور
049-Mlango Wa Uharamu Kuomboleza Maiti kwa Kujipiga Mashavu, Kuchana Nguo, Kung'oa Nywele, Kunyoa na Kujiombea Maangamivu
Hadiyth – 1
عن عمر بن الخطاب رضي الله عنه قال : قال النَّبِيّ صلى الله عليه وسلم : (( المَيِّتُ يُعَذَّبُ فِي قَبْرِهِ بِمَا نِيحَ عَلَيْهِ )) .
وَفِي روايةٍ : (( مَا نِيحَ عَلَيْهِ )) . متفق عليه .
Imepokewa kutoka kwa 'Umar bin Khattwaab (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Maiti anaadhibiwa kaburini mwake kwa kuliliwa."
Na katika riwaayah nyengine: "Kwa kuliliwa." [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhy na An-Nasaaiy]
Hadiyth – 2
وعن ابن مسعود رضي الله عنه قال : قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( لَيْسَ مِنَّا مَنْ ضَرَبَ الخُدُودَ ، وَشَقَّ الجُيُوبَ ، وَدَعَا بِدَعْوَى الجَاهِلِيَّةِ )) . متفق عليه .
Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Si miongoni mwetu mwenye kujipiga uso, na kuchana nguo zake na kuomba kwa duaa za kijahiliya anapopatikana na msiba." [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy]
Hadiyth – 3
وَعَنْ أبي بُرْدَةَ ، قال : وَجعَ أبو مُوسَى ، فَغُشِيَ عَلَيْهِ ، وَرَأسُهُ فِي حِجْرِ امْرَأَةٍ مِنْ أهْلِهِ ، فَأَقْبَلَتْ تَصِيحُ بِرَنَّةٍ فَلَمْ يَسْتَطِعْ أنْ يَرُدَّ عَلَيْهَا شَيْئاً ، فَلَمَّا أفَاقَ قَالَ : أنَا بَرِيءٌ مِمَّنْ بَرِىءَ مِنْهُ رسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم إنَّ رسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم بَرِيءٌ مِنَ الصَّالِقَةِ ، والحَالِقَةِ ، والشَّاقَّةِ . متفق عليه .
Amesema Abu Burdah: Abu Muwsaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) aliumwa sana na akazimia hali kichwa chake kiko pajani kwa mke wake. Kuona hali yake hiyo mkewe alianza kulia kwa sauti kubwa, naye Abu Muwsaa hakuweza kumzuilia wala kumwambia chochote kwa sababu ya udhaifu wake. Alipozinduka akasema: "Mimi siko pamoja na yule aliyemkataa mwanamke anayelia kwa mayowe; na anye nyoa nywele zake (kwa msiba) na anayechana nguo)." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na An-Nasaaiy]
Hadiyth – 4
وعن المغيرة بن شعبة رضي الله عنه قال : سمعتُ رسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يقولُ : (( مَنْ نِيحَ عَلَيْهِ ، فَإنَّهُ يُعَذَّبُ بِمَا نِيحَ عَلَيهِ يَومَ القِيَامَةِ )) . متفق عليه .
Amesema Al-Mughiyrah bin Shu'bah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mwenye kuliliwa, hakika yeye ataadhibiwa kwa alicholiliwa Siku ya Qiyaamah." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 5
وعن أُمِّ عَطِيَّةَ نُسَيْبَةَ – بِضَمِّ النون وفتحها – رضي الله عنها ، قالت : أخَذَ عَلَيْنَا رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم عِندَ البَيْعَةِ أنْ لاَ نَنُوحَ . متفق عليه .
Amesema Umm 'Atwiyyah Nusaybah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amechukua kwetu hatutalia kwa mayowe (wakati wa msiba)." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na An-Nasaaiy]
Hadiyth – 6
وعن النعمان بن بشير رضي الله عنهما ، قال : أُغْمِيَ عَلَى عَبدِ اللهِ بْنِ رَوَاحَةَ رضي الله عنه ، فَجَعَلَتْ أُخْتُهُ تَبْكِي، وَتَقُولُ : وَاجَبَلاهُ ، وَاكَذَا ، وَاكَذَا : تُعَدِّدُ عَلَيْهِ . فقالَ حِينَ أفَاقَ : مَا قُلْتِ شَيْئاً إلاَّ قِيلَ لِي أنْتَ كَذَلِكَ ؟! . رواه البخاري .
Amesema Nu'maan bin Bashiyr (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Alipozirai 'Abdillaah bin Rawaahah (Radhwiya Allaahu 'anhu), dadake alianza kumlilia kwa sauti huku anasema: "Ee jabali langu (mwenye haiba ya hali ya juu miongoni mwa watu) na kadha na kadha, akihesabu sifa zake nzuri." Alipopata fahamu alisema: "Hukusema lolote katika hayo isipokuwa niliulizwa: Je, wewe uko hivo?" [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 7
وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قال : اشْتَكَى سَعْدُ بنُ عُبَادَةَ رضي الله عنه شَكْوَى ، فَأتاهُ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم ، يَعُودُهُ مَعَ عَبدِ الرَّحمانِ بْنِ عَوفٍ ، وَسَعْدِ بن أبي وقَّاصٍ ، وعبدِ اللهِ بن مسعودٍ رضي الله عنهم . فَلَمَّا دَخَلَ عَلَيْهِ ، وَجَدَهُ في غَشْيَةٍ فَقالَ : (( أقَضَى ؟ )) قالوا : لا يا رسول اللهِ ، فَبكَى رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، فَلَمَّا رَأى القَوْمُ بُكَاءَ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم بَكَوْا ، قال : (( ألاَ تَسْمَعُونَ ؟ إنَّ اللهَ لاَ يُعَذِّبُ بِدَمْعِ العَيْنِ ، وَلاَ بِحُزْنِ القَلْبِ، وَلكِنْ يُعَذِّبُ بِهذَا )) - وَأشَارَ إلَى لِسَانِهِ - أو يَرْحَمُ )) . متفق عليه.
Amesema Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Sa'ad bin 'Ubadah (Radhwiya Allaahu 'anhu) alikuwa anaumwa sana, hivyo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimtembelea akiwa pamoja na 'Abdur-Rahmaan bin 'Awf na Sa'as bin Abi Waqqaas na 'Abdillaah bin Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu). Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alilia kuiona hali yake na watu walipomuona Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akilia nao pia wakalia. Akasema: "Sikilizeni! Hakika Allaah hamuadhibu kwa kutokwa na machozi wala kwa huzuni ya moyo, anaadhibu kwa hili." Na hapo akaashiria mdomo wake, kisha akasema: "Au anawahurumia." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 8
وعن أبي مالك الأشعري رضي الله عنه قال : قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( النَّائِحَةُ إذا لَمْ تَتُبْ قَبلَ مَوْتِهَا تُقَامُ يَومَ القِيَامَةِ وَعَلَيْهَا سِربَالٌ مِنْ قَطِرَانٍ ، وَدِرْعٌ مِنْ جَرَبٍ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Maalik Al-Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwanamke mwenye kulia kwa mayowe ikiwa hatatubu kabla ya kufa kwake, atafufuliwa Siku ya Qiyaamah akiwa amevaa koto la lami na deraya iliyoshika kutu." [Muslim]
Hadiyth – 9
وعن أَسِيد بن أبي أَسِيدٍ التابِعِيِّ ، عن امْرَأةٍ مِنَ المُبَايِعاتِ ، قالت : كان فِيما أخَذَ عَلَيْنَا رسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، فِي المَعْرُوفِ الَّذِي أخَذَ عَلَيْنَا أنْ لاَ نَعْصِيَهُ فِيهِ : أنْ لا نَخْمِشَ وَجْهَاً ، وَلاَ نَدْعُوَ وَيْلاً ، وَلاَ نَشُقَّ جَيْباً ، وأنْ لاَ نَنْشُرَ شَعْراً . رواه أبو داود بإسناد حسن .
Imepokewa kutoka kwa Usayd bin Abi Usayd, Tadi'iy kutoka kwa mwanamke aliyechukua bay'ah kwamba: "Katika mambo ambayo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alichukua ahadi kutoka kwetu, ni kufanya mabo mema na kuwa hatutamuasi kabisa, nayo ni: Hatutakwaruza nyuso zetu, wala kuomba maangamivu wala kuchana nguo na kuwa pia hatutafumua nywele zetu (kwa sababu ya msiba)." [Abu Daawuwd kwa Isnaad iliyo Hasan].
Hadiyth – 10
وعن أبي موسى رضي الله عنه : أنَّ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم ، قال : (( مَا مِنْ مَيِّتٍ يَمُوتُ فَيَقُومُ بَاكِيهِمْ فَيَقُولُ : وَاجَبَلاَهُ ، واسَيِّدَاهُ ، أو نَحْوَ ذلِكَ إلاَّ وُكِّلَ بِهِ مَلَكَانِ يَلْهَزَانِهِ : أهكَذَا كُنْتَ ؟ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Muwsaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapofariki mtu akasimama wenye kumlilia kwa kusema: "Ee mlima miongoni mwetu, ee mtemi na bwana wetu', au mfano wake isipokuwa huwakilishwa Malaaikah wawili wanaompiga ngumi kwenye kifua chake na kumuuliza: 'Je, ulikuwa hivo'?" [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan].
Hadiyth – 11
وعن أبي هريرة رضي الله عنه ، قال : قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( اثْنَتَانِ فِي النَّاسِ هُمَا بِهِمْ كُفْرٌ : الطَّعْنُ فِي النَّسَبِ ، وَالنِّيَاحَةُ عَلَى المَيِّتِ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Watu aina mbili miongoni mwa watu wana ukafiri: Kusuta nasaba na kuomboleza juu ya maiti." [Muslim]