050-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kuwaendea Makuhani na Wapiga Bao na Ramli

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب النَّهي عن إتيان الكُهّان والمنجِّمين

والعُرَّاف وأصحاب الرمل والطوارق بالحصى وبالشعير ونحو ذلك

050-Mlango Wa Kukatazwa Kuwaendea Makuhani na Wapiga Bao na Ramli

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن عائشة رضي الله عنها ، قالت : سأل رسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم أنَاسٌ عَنِ الكُهَّانِ، فَقَالَ : (( لَيْسُوا بِشَيءٍ )) فَقَالُوا : يا رَسُولَ اللهِ إنَّهُمْ يُحَدِّثُونَا أحْيَاناً بِشَيءٍ، فَيَكُونُ حَقّاً ؟ فقالَ رسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( تِلْكَ الكَلِمَةُ مِنَ الحَقِّ يَخْطَفُهَا الجِنِّيُّ فَيَقُرُّهَا فِي أُذُنِ وَلِيِّهِ ، فَيَخْلِطُونَ مَعَهَا مئَةَ كَذْبَةٍ )) . متفق عليه .

وفي رواية للبخاري عن عائشة رضي الله عنها : أنَّها سمعتْ رسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يقولُ : (( إنَّ المَلائِكَةَ تَنْزِلُ فِي العَنَانِ - وَهُوَ السَّحَابُ - فَتَذْكُرُ الأَمْرَ قُضِيَ فِي السَّماءِ ، فَيَسْتَرِقُ الشَّيْطَانُ السَّمْع ، فَيَسْمَعُهُ ، فَيُوحِيَهُ إلَى الكُهَّانِ ، فَيَكْذِبُونَ مَعَهَا مِئَةَ كَذْبَةٍ مِنْ عِنْدِ أَنْفُسِهِمْ )) .

Amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Aliulizwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na watu kuhusu makuhani, akasema: "Wao si chochote na hawana kitu." Wakasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Hakika wao wakati mwengine huzungumzia kitu na kikawa kweli." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Hiyo ni kalima ya kweli ambayo shetani huipata kwa bahati na hivyo kuifikisha kwa rafiki yake. Ukweli huu wanachanganya na uwongo mia moja." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Na katika riwaayah ya Al-Bukhaariy kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakika Malaaikah hushuka kwenye kiwingu na hutaja mambo ambayo yamepitishwa mbinguni. Shetani husikia hayo kibahati na baadaye kuyafikisha kwa makuhani, hivyo kuongeza pamoja nayo uwongo mia moja kutoka katika nafsi ao wenyewe." 

 

 

Hadiyth – 2

وعن صَفِيَّةَ بِنتِ أبي عُبيدٍ ، عن بعض أزواجِ النَّبيِّ  صلى الله عليه وسلم ، ورَضِيَ اللهُ عنها ، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم ، قال : (( مَنْ أَتَى عَرَّافاً فَسَأَلَهُ عنْ شَيْءٍ فَصَدَّقَهُ ، لَمْ تُقْبَلْ لَهُ صَلاَةٌ أرْبَعِينَ يَوماً )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa kwa Swafiyyah bint Abu 'Ubayd (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kutoka kwa baadhi ya wakeze Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)alisema: "Mwenye kwenda kwa mtu anayedai kuwa anajua kitu chake kilichopotea, akamuuliza kuhusu kitu chochote na akamsadiki haitokubaliwa Swalaah yake kwa siku arobaini." [Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعَنْ قَبِيصَةَ بنِ المُخَارِقِ رضي الله عنه قال : سمعتُ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم يقولُ : (( العِيَافَةُ ، وَالطِّيَرَةُ ، والطَّرْقُ ، مِنَ الجِبْتِ )) . رواه أبو داود بإسناد حسن .

Amesema Qabiyswah bin Al-Mukhaariq (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Kuangalilia (kupigana bao), na mkosi, na kuruka kwa ndege ni katika Jibt." [Abu Daawuwd kwa Isnaad iliyo Hasan] 

 

Hadiyth – 4

وعن ابن عباس رضي الله عنهما ، قال : قال رسولُ الله  صلى الله عليه وسلم : (( مَنِ اقْتَبَسَ عِلْماً مِنَ النُّجُوم ، اقْتَبَسَ شُعْبَةً مِنَ السِّحْرِ زَادَ ما زَادَ )) . رواه أبو داود بإسناد صحيح .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kujifunza sehemu ya elimu kuhusu nyota ni kama amejifunza sehemu ya sihiri (uchawi). Na kila anapozidi kuendelea kusoma ndio anazidi kuingia katika sihiri." [Abu Daawuwd kwa Isnaad iliyo Swahiyh]

 

Hadiyth – 5

وعن مُعاوِيَةَ بنِ الحَكَمِ رضي الله عنه قال : قلتُ : يا رسُولَ اللهِ إنِّي حديثُ عَهْدٍ بالجاهِليَّةِ ، وَقَدْ جَاءَ اللهُ تَعَالَى بالإسْلاَمِ ، وإنَّ مِنَّا رِجَالاً يَأتُونَ الكُهَّانَ ؟ قال : (( فَلاَ تأتِهِمْ )) قُلْتُ : وَمِنَّا رِجَالٌ يَتَطَيَّرُونَ ؟ قَالَ : (( ذَلِكَ شَيْءٌ يَجِدُونَهُ فِي صُدُورِهِمْ ، فَلاَ يَصُدُّهُمْ )) قُلْتُ : وَمِنَّا رِجَالٌ يَخُطُّونَ ؟ قَالَ : (( كَانَ نَبِيٌّ مِنَ الأنْبِيَاءِ يَخُطُّ ، فَمَنْ وَافَقَ خَطَّهُ ، فَذَاكَ )) . رواه مسلم .

Amesema Mu'awiyah bin Al-Hakam (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nilimuuliza: Ee Rasuli wa Allaah! Hakika mimi nimetoka hivi karibuni katika Ujahiliyah na hakika Allaah Ta'aalaa na Uislamu. Na wapo miongoni mwetu ambao bado wanawaendea makuhani." Akasema: "Musiende kwao." Nikasema: "Miongoni mwetu wako wanao ongozwa na bahati." Alisema: "Hilo ni jambo wanaolipata katika vifua vyao (na akili zao). Wasiwakataze hilo ule muono wao kwani jambo hilo halileti manufaa wala madhara." Nikasema na miongoni mwetu kuna watu wanachora? Akasema: Kulikuwa Nabiy miongoni mwa Manabiy anachora anae afikiana na mchoro wake itakuwa kama hivyo. [Muslim]

 

Hadiyth – 6

وعن أَبي مَسعودٍ البدريِّ رضي الله عنه : أنَّ رسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم نَهَى عَنْ ثَمَنِ الكَلْبِ ، وَمَهْرِ البَغِيِّ ، وَحُلْوَانِ الكاهِنِ . متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikataza kutumia thamani ya mbwa (baada ya kuuzwa) na pato la malaya na ada anayopatiwa kuhani. [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Share